Uwakilishi wetu si uwakilishi

TAWA

JF-Expert Member
Jun 23, 2013
3,673
1,571
Nasema hivyo kwa kuwa nchi yetu haina uwakikishi ulio sahihi. Haiingii akilini pale mbunge wa jimbo la Morogoro vijijini (mfano) anatokea na anaishi jijini Dar es salaam.

Huyu hatakuwa mwakilishi sahihi kuwawakilisha watu hao anaowaita wananchi wake. Katiba yetu isitambue kuwa ubunge ni ajira, bali iwe tu nafsi ya uwakilishi tofauti na inavyochukuliwa kwa sasa.

Haya yafanyike kwenye kuboresha hili:

1. Mbunge lazima awe mkazi halisi wa eneo analowakilisha. Awe ameishi katika eneo husika miaka mitano mfululizo kabla ya kugombea.

2. Mgombea wa nafasi ya ubunge lazima adhaminiwe na WANANCHI katika jimbo husika walau watu hamsini kutoka kila kata.

Mawazo tu, nikosolewe kwa staha.
 
Hakika hilo ni wazo la msingi maana unakuta mbunge nyumba na familia yake vyote viko dar halafu akiwa bungeni anatokwa na povu eti wananchi wangu wamenituma khaaa!! Wamekutuma saa ngapi nawakati umetoka dar ukaenda Dodoma bungeniiii???
 
Inatia hasira sana aseee
 
mfano mzuri ni wameru huchaguliwi kama we huna historia hapo jimboni itakula kwako lazma mbunge awe anjua vizuri jimbo siyo maeneo mengine unayajua msimu wa kampeni
 
Mmh kwahiyo kassim majaliwa akaishi lindi? Au kwa ile katiba ambayo mbunge anatakia asiwe waziri?
 
Mmh kwahiyo kassim majaliwa akaishi lindi? Au kwa ile katiba ambayo mbunge anatakia asiwe waziri?
Siyo tu akaishi Lindi ila hakuwa na sifa za kuwa mgombea ubunge jimbo la luangwa, kama tungefuata taratibu za uwakilishi halisi.
 
Back
Top Bottom