Uwajibikaji wa serikali yetu ya JMT

Uwajibikaji wa serikali yetu ya JMT

Inqusitor

Member
Joined
Sep 27, 2012
Posts
29
Reaction score
8
Habari wadau

Ninawazo la kuanzisha web application itakayokua inahusika na uwajibikaji wa serikani ikijumuisha baadhi ya mambo yafuatayo:-

1. Uwezo wa viongozi walioteuliwa. Kuanzia rais mpaka viongozi atakao wateua

2. Kutimizwa kwa ahadi walizofanya wakati wa kampeni

3. Uwazi na uwajibikaji wa viongozi wa serikali

4. Kuangalia mambo ya siasa yanayofanyika nchi (faida na hasara zake)

5. Kuweka mezani nini kifanyike ili kuboresha serikali iliyopo madarakani na mashirika yake (Ushauri na mawazo). Mfano, Nimesikiwa watu mtaani wana point nzuri kuhusu nini kinaweza fanyika kuiboresha tanesco nk

6. Kuwaunganisha wasomi wa nchi hii ili wawe watetezi kwa wanyonge na wasio na elimu ya vyeti. Mambo mengi yanatendeka laiti kama wasomi wangeweza kupinga yasinge fanyika. Mf MB 8 za mitandao ya simu, network ya kusubiri sms kwa masaa 24 nk

7. Na mawazo kutoka kwako

Mdau wewe unasemaje ? Nakaribisha mawazo na ushauri.

NB: Fikiri kabla ya kuandika comment yako
 
utapimaje kazi za management?

Unaweza kupima kwa kuangalia jinsi gani kiongozi ameweza kushirikiana na team yake kufikia malengo. Kama wameshindwa the key players kwenye management hawana uwezo
 
Back
Top Bottom