UWAJIBIKAJI: Sugu aendelea na ziara Mbeya mjini!

Kiganyi

JF-Expert Member
Apr 30, 2012
1,242
765

Mbunge wa Mbeya Mjini akipokelewa na wananchi wa Kata ya Nsoho kabla ya kufanya mkutano mkubwa wa hadhara katika eneo hilo lililo nje kidogo ya mji wa Mbeya
Hapa Mbunge wa Mbeya mjini akiwaelezea wananchi wa kata ya Iziwa baadhi ya utekelezaji wa shughuli za maendeleo zilizofanyika mpaka sasa hapa Jimboni
Wananchi wakimsikiliza kwa makini Mh. Joseph Mbilinyi (Sugu) alipokuwa akiwahutubia wananchi katika ziara ya jimboni kwake Mbeya mjini

Sugu akisisitiza jambo kwa wananchi wa kata ya Iziwa wakati wa ziara yake ya kuzungukia kata zote za jimbo la Mbeya Mjini
Wananchi waki msikiliza Mbunge wao Joseph Mbilinyi (Sugu) wakati akiwahutubia katika kiwanja cha kilabu cha Iziwa
Mheshimiwa Sugu akikazia jambo ambalo Kamanda Kwame Elly Anangisye (pichani) alikuwa akilipigania kwa maendeleo ya wakazi wa jiji la Mbeya
Watu wa rika tofauti wa Kata ya Iziwa wakimsikiliza Mbunge wao Joseph Mbilinyi

Wananchi wa kata wa Ituha wakimsikiliza kwa makini Mbunge wao Joseph Mbilinyi (Sugu)

Mbunge wa Mbeya mjini akielezea shughuli za utekelezaji ahadi zilizofanyika mpaka kufikia kipindi hiki
Mheshimiwa Joseph Mbilinyi, Katibu CHADEMA wilaya Criss Mwamasiku (kushoto) na Kamanda Kwame Elly Anangisye (nyuma) wakisikiliza kero na maoni ya wananchi wa kata ya Ituha
Mwananchi wa Kata ya Ituha akitoa malalamiko yake mbele ya Mbunge wa Mbeya mjini

Wananchi wa Kata ya Ituha wakimsikiliza Mbunge wao Joseph Mbilinyi (Sugu) katika ziara yake ya kutembelea kata za Mbeya mjini
 
Kumbe mikutano ya Sugu inajaza watoto tu

Nyie si mmezoea wazee na vikongwe? Vingine vinatembea na mkongojo, hata timu za mpira zina under 20, under 17 na under 14. Huo ndo mtaji, nyie endeleeni na wazee.
 
Nyie si mmezoea wazee na vikongwe? Vingine vinatembea na mkongojo, hata timu za mpira zina under 20, under 17 na under 14. Huo ndo mtaji, nyie endeleeni na wazee.
Hata hao wazee na vikongwe wameanza kuwakimbia ndio maana siku hizi ukisikia chama cha mapinduzi kimefanya Mkutano basi ujue ni mkutano wa NEC au CC, au Mkutano wa Balaza la Mawazi, au mkutano wa wabunge wa CCM, sababu hawana watu wa kuwasikiliza hivyo kuondoa upweke wameamua kujikusanya wenyewe na kuhutubiana,
 
sugu anajua kazi ya ubunge sio kukaa mjini tu lakini alihahidi hawezi kukaa marekani wakati wananch wanaumia rejerea kipindi cha mchakato majimboni
 
Hata hao wazee na vikongwe wameanza kuwakimbia ndio maana siku hizi ukisikia chama cha mapinduzi kimefanya Mkutano basi ujue ni mkutano wa NEC au CC, au Mkutano wa Balaza la Mawazi, au mkutano wa wabunge wa CCM, sababu hawana watu wa kuwasikiliza hivyo kuondoa upweke wameamua kujikusanya wenyewe na kuhutubiana,

Kwa mamlaka niliyopewa na wanakijiji wenzangu wa busisya,ninakutunuku u dr wa heshima toka hapa kijijini kwetu Busisya kuanzia sasa utatambulika Dr Sangarara kwani jibu ulilolitoa hapa ni maridhawa kabisa na jibu hili litayajibu maswali yote yatakayo fanana na hili toka kwa wanamagamba FC
 
Back
Top Bottom