Uvuvi haramu Temeke ni changamoto - Mjimwoge

Uvuvi haramu Temeke ni changamoto - Mjimwoge

Eddie Juma

Member
Joined
Mar 22, 2016
Posts
16
Reaction score
5
Tarehe 20/04/2016 vikundi vya kusimamia fukwe ( Beach Management Unit – BMU) vya Gezaulole, Mjimwema na Mwongozo viliungana na kuunda ( Collaborative Fisheries Management Area - CFMA ) umoja wa kusimamia maeneo yao ya uvuvi unaojulikana kama “MJIMWOGE”, bado kuna changamoto kubwa ya kuzuia uvuvi haramu ambao wilaya ya Temeke inaongoza kwa uvuvi wa baruti kulinganisha na wilaya zote nchini Tanzania kutokana na takwimu za WWF.

Kinachosikitisha ni kuwa je ni kweli idara zinazotakiwa kusimamia uvuvi haramu zimeshindwa na zimeamua kuziachia BMUs na CFMA ambazo hazina vitendea kazi na wala hawavijui pa kuvipata kwani kazi nzima au mazingira mazima ya vikundi hivyo ni ya kujitolea, kwa pamoja kupitia CFMA ya MJIMWOGE ina changamoto zifuatazo ambazo ingependa kupitia makala hii kuwajuza wananchi kwa kuamini watasaidia kupiga kelele au kushauri kwa vyombo vilivyo na uwezo navyo, kwani hali ni mbaya inatisha na kwa kuamini Mheshimiwa Rais John Pombe Magufuli ni mmoja wa wapiganaji namba moja wa uvuvi haramu basi naye anaweza kufikishiwa taarifa hii kwani tunaamini kwa kuzuia uvuvi haramu tutakuwa tumeweza kuchangia katika kuinua uchumi wa nchi yetu ambayo tunafahamu tuna kila aina ya utajiri, MJIMWOGE haioni tofauti ya ujangili wa wanyama pori na uvuvi haramu tunatoa wito kwa Serikali yetu kuweka nguvu kama inayotumika ya kuzuia ujangili basi itumike na huku kwenye bahari yetu ili wananchi wafaidike na rasilimali hiyo: Changamoto zetu zimegawanyika katika sekta kuu nne :

1. Afya .

Uvuvi wa kutumia baruti au mabomu una madhara makubwa sana ya afya kwa wavuvi, walaji na watumiaji wa kawaida wa fukwe zetu. Kuna visa vingi vya wavuvi waliofariki kutokana na kuripukiwa na miripuko hiyo wakati wa kutengeneza na wakati wa kupiga samaki, wapo waliofariki na wengine kupoteza viungo vyao kama mikono au miguu. Pia samaki wavuliwao kwa kutumia mabomu wanasababisha ugonjwa wa saratani kwa walaji ambao ni “MIMI NA WEWE” na kwa kukosa utaalamu kutambua tofauti basi tujijue walaji samaki wa” LEO” ni wagonjwa wa saratani wa “KESHO”. .
Aina ya uvuvi wa mabomu upo wa maji madogo ambao wavuvi hutumia maboti madogo madogo na kuogelea wakati wa kuchukua samaki na kuna uvuvi wa mabomu wa maji mengi ambapo wavuvi hutumia gesi za oxygen kwa ajili ya kwenda kuchukua samaki wanaozama baada ya kupigwa mabomu, utumiaji huo wa gesi hizo hufanywa bila ya kufuata taratibu za kuzamia na hapo hutokea vifo au wavuvi kupatwa na ugonjwa wa kiharusi, bila ya kuchukua hatua za haraka vifo na ulemavu kwa wavuvi una athari ndogo kuliko mfumuko wa wagonjwa wa saratani kutokana na kula samaki wanaovuliwa kwa mabomu watakapotokea. Sisi MJIMWOGE tunaamini “ Uvuvi bila ya mabomu unawezekana”.

2. Uchumi .
Katika hali ya kawaida ni kuwa nyenzo mojawapo ya uchumi kwa wananchi waishio pembezoni mwa bahari ni uvuvi, lakini pia kuna harakati nyingine katika fukwe zetu kwa ajili ya wananchi hao kujiingizia kipato. .
Matokeo ya uharibifu wa nyumba za kuzalia samaki na vifaranga kwa uvuvi wa mabomu, kokolo na uvuvi wa maji haba ni mkubwa sana ambao unatishia samaki kupungua kwa kasi katika bahari yetu kwani uvuvi huo pamoja na kuua vifaranga pia huharibu mazalia yake. Hali hiyo inapelekea kupunguza ajira na hata mazao ya baharini ambayo pamoja na samaki kuna mwani, majongoo na kadhalika. .
Biashara za kuzamia na kuelea baharini ( Diving and Snorkeling) huchangia ajira kwa wananchi waishio pembezoni mwa bahari na kuongeza pato la Taifa letu, lakini uharibifu huo wa kuvunja miamba ya baharini na kuua viumbe vyake ambapo athari yake ni kupoteza uasilia wake husababisha sekta hiyo kudumaa na kukosa soko athari ambayo hupunguza pato la Taifa kwa ujumla. .
Kukubali kuua kiwanda cha rasilimali za bahari yetu ni kukubali kudumaza uchumi wa nchi yetu kitu ambacho sisi wana MJIMWOGE hatukikubali kwahiyo tunaomba kwa pamoja kushirikiana katika harakati za kupiga vita uvuvi haramu wa mabomu, uvutaji kokolo na uharibifu mwengine wa bahari yetu. .

3. Mazingira .
Uharibifu wa Mazingira ya Bahari nchini unaosababishwa na Uvuvi haramu wa kutumia mabomu ni mkubwa sana, hali ambayo imekuwa ni kichocheo cha kupungua kwa mazalia ya samaki baharini pamoja na mazao mengine. Mazingira huharibika sana sehemu unapotumika uvuvi haramu, uvuvi wa kokolo, uvuvi wa maji haba na upigaji wa mabomu, Uvuvi huo huvunja maeneo ya miamba iliyojijenga kwa miaka mingi iliyopita ambayo ni kitu haba sana kukipata mara kinapoharibiwa, miamba hiyo inahitaji zaidi ya karne iweze kujiumba tena kutokana na asili ya baharini ilivyo. Uvuvi haramu husababisha jangwa chini ya bahari ambapo madhara yake ni kuleta mmomonyoko na kuongeza hali ya joto duniani ambalo ni janga kwa maisha ya viumbe wa baharini na nchi kavu kwa ujumla. .
Katika kuliona hili MJIMWOGE ipo katika kampeni kubwa ya kupiga vita uvuvi haramu kwa ajili ya kulinda mazingira, kampeni ambayo inahitaji kuungwa mkono na sekta zote zinazohusika katika kukuza uchumi wetu na kufanya nchi yetu iwe na vivutio asilia vya utalii siku zote.

4. Utalii .
Bahari ni mojawapo ya kivutio kikubwa cha utalii chini mwetu, hali iliyopo katika maeneo ya fukwe zetu hayapo rafiki wa utalii, kukua kwa utalii wa baharini kunategemeana sana kwa kuwepo na utunzaji, usimamizi wa bahari pamoja na usalama wa mali za watalii, vitendo vya upigaji wa mabomu usio na kikomo unaathiri sana mazingira mazuri yaliyopo chini ya bahari ambayo watalii hupenda kwenda kuzamia au kuelea juu ya maji na kujionea uzuri wa bahari yetu na viumbe vyake, ukabaji na wizi wa mali za watalii umepunguza sana nguvu za kukua kwa utalii katika fukwe tukilinganisha na jirani zetu wa Zanzibar.
Hivyo basi katika kuhakikisha tunapambana na changamoto hiyo MJIMWOGE imebuni mradi wa Fukwe Salama “Salama beach” , mradi ambao ukikamilika utaweza kurudisha hamasa na moyo kwa watalii kwani mradi huo unahusika na kuweka ulinzi wa masaa 24 kulinda fukwe na kukabiliana na uhalifu wa aina yoyote unaoweza kufanywa na watu wasiolitakia mema taifa letu la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

MJIMWOGE katika ujenzi wa Taifa.
 
Wadau naomba tupige kelele kuhusu tatizo hili la uvuvi haramu kwani limekuwa tatizo sugu katika wilaya yetu ya Temeke, na kutokana na takwimu zinaonyesha wilaya ya temeke ndiyo inaongoza kwa upigaji mabomu kuliko maeneo yote ya pwani ya Tanzania, Je ni kweli vyombo vya usalama vimeshindwa kuchukua hatua ya dhati ya kuzuia tatizo hili sugu na la muda mrefu??! Mabomu yanatoa mlio ambao unasikika maeneo mengi yaliyo karibu na pwani yetu, ni kweli viongozi wa maeneo hayo wameshindwa kupanga mikakati ya kuzuia suala hili ??!
 
kama mmoja wa wanaharakati wa kuzuia uvuvi haramu Tanzania, naomba kila asomaye ajitahidi ku mtag mwenzake ili ujumbe huu ufike mbali labda wahusika watastuka, nikiamini Jamii Forums ina mchango mkubwa katika Taifa hili naomba msaada wenu wa kusambaza taarifa hii.
 
Hivyo basi katika kuhakikisha tunapambana na changamoto hiyo MJIMWOGE imebuni mradi wa Fukwe Salama “Salama beach” , mradi ambao ukikamilika utaweza kurudisha hamasa na moyo kwa watalii kwani mradi huo unahusika na kuweka ulinzi wa masaa 24 kulinda fukwe na kukabiliana na uhalifu wa aina yoyote unaoweza kufanywa na watu wasiolitakia mema taifa letu la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

MJIMWOGE katika ujenzi wa Taifa.


Moderator Hili nadhani kama mtaipachika hapo juu kabisa mwa thread hii itapendenza na kuongeza dhamani !



Captain Kudra and Blast-fishing around Makatube Island, Tanzania

MwambaoNetwork
 
Moderator Hili nadhani kama mtaipachika hapo juu kabisa mwa thread hii itapendenza na kuongeza dhamani !



Captain Kudra and Blast-fishing around Makatube Island, Tanzania

MwambaoNetwork

Nimeipenda sana hii, jamani moderator naomba kwa uwezo wenu muipe nafasi ya juu habari hii ili ionekane na wadau kwani habari hii imepotea sana, moderator kwa uwezo wenu tunaomba hii habari ipate nafasi ya kuonwa zaidi.
 
Back
Top Bottom