Uvutaji Sigara Afrika Mashariki na Kati | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uvutaji Sigara Afrika Mashariki na Kati

Discussion in 'JF Doctor' started by MziziMkavu, Jan 29, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jan 29, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  [​IMG]  Uvutaji sigara Afrika Mashariki na Kati ni tabia ambayo imekuwa ikipungua katika baadhi ya maeneo na kuongezeka katika sehemu nyinginezo. Kwa miaka kadha sasa wanaharakati wamekuwa wakipiga vita tabia hiyo kutokana na athari zake katika afya ya mtu na jamii kwa jumla.
  Nchini Kenya serikali imechukua hatua kadha kupunguza tabia ya uvutaji ikiwa ni pamoja na kuweka masharti makali katika matangazo ya sigara na bidhaa nyingine za uvutaji na pia kuzuia uuzaji wa sigara moja moja kwa lengo la kufanya tabia hiyo iwe ya gharama kubwa mtu anapolazimika kununua paketi nzima. Hata hivyo, ingawa kuna dalili za upunguaji wa uvutaji wasiwasi upo hasa kwa vijana wanaoanza kuvuta sasa. Imedhihirika pia kuwa idadi kubwa ya wanawake wanavuta sigara tena hadharani kuliko ilivyokuwa katika ya nyuma.
  Huko Tanzania wanaharakati waliandamana mbele ya ofisi za jiji la Dar es Salaam na Wizara ya Afya Novemba mwaka jana kuwasilisha madai ya kutaka serikali ichukue hatua kali zaidi katika masharti ya utangazaji wa bidhaa za tumbaku. Uganda pia imepiga hatua kubwa katika masharti ya matangazo ya bidhaa za tumbaku lakini uvutaji sigara ungali katika kiwango cha juu. Sikiliza makala hii maalum kuhusu uvutaji Afrika Mashariki na Kati.


  http://www.voanews.com/swahili/2010-01-15-voa3.cfm
   
Loading...