Baraghash
JF-Expert Member
- Dec 18, 2012
- 2,713
- 1,789
Wana Bodi nifahamisheni.
Kampuni ya Petrobras Tanzania Limited ikishirikiana na Shell zinashughulika na utafutaji wa mafuta na gesi katika kisiwa cha Latham, kinachojuulikana kama "Fungu Baraka au Fungu la Kizimkazi" ambalo liko kwenye eneo la Zanzibar na linatumiwa sana na wavuvi wa kusini ya kisiwa cha Zanzibar hususan wa Kizimkazi, kwa wavuvi kuweka Dago katika fungu hilo. Hivi karibuni kuna tetesi kuwa wavuvi hawa wazanzibar wanabughudhiwa wakiwa katika eneo hilo la Fungu.
Kipindi kirefu sasa vimejitokeza vikundi na kampuni kadhaa ( ambavyo sijui vimepata wapi usajili) vinavyo jishughulisha na biashara ya utalii kutokana uzuri wake wa asili, matumbawe na kuwepo na mkusanyiko wa ndege wa aina tofauti na sasa imeingia biashara ya gesi na mfuta .
Wakati wa utawala Dr. Salmini Amour(komandoo) alifanya ziara maalum kukitambua kisiwa hicho kuwa ni milki HALALI ya Zanzibar.
Lakini kutokana na harakati na shughuli nyingi zinazo fanywa kwa sasa na hasa na Kampuni ya Petrobras Tanzania Limited ikishirikiana na Shell, imenitia hamu na mshawasha ya kutaka kujua kama uwepo wao umeridhiwa na Zanzibar na kwamba harakati zao zinaeleweka au ndio " law of the Jungle" inaendelea kutumika?
Ni elimisheni