nikweli ndoa inahitaji uvumilivu ila uvumilivu lazima uwe na mipaka ikizingatia lengo la kuamua kuoana. mimi binafisi najua lengo la ndoa ni kuishi pamoja ili muweze kuijenga familia na maisha yenu pamoja na familia munayoijenga kwa pamoja lakini pia muweze kutuliza hamu ya matamanio yenu. sasa ili muweze kuish kwa msing huu na maisha yaende ni lazima kwanza kila mtu ajitambue kwa nafasi yake kwamwenzake kila aish kwa kulinda heshima ya mwenzake.yani kama nimume ulinde heshima ya mkeo mbele ya jamii inayowazunguka na mkepia hivyohivyo.lakini pia kujua kua kila mtu anawajibu wakuleta maendeleo hata kama.hana kipato lazima kila munachofanya kiwe ni mawazo ya wote hapa munaweza kuish kwa kuvumiliana yale matatizo madogo madogo. sasa yapi hayavumiliki nitatoa mifano michache. mume anaamka asubuh karusha buku mbili mezani haitosh hata mwanamke ungepiga bajeti ya kula ugali na chumv kutwanzima alafu jioni akirudi yuko tilalila tena muda huo anakuja usiku mkali nakupigwa upigwe.umetumia njia zote mpaka kwa wazazi imeshindikana unakas hapo huna kwenu?hata kama unawatoto beba wanao nenda kwenu tafta kibaru ulishe wanao.au mume unaenda kuhangaika huko ukija ndani kile kidogo ulichopata unamkabidh mkeo mke wangu fanya matumizi kidogo nyingine tuweke akiba kuna leo na kesho mke anachukua zile hela anazitumia atakavyo tena bila kukujali tens ukiongea ndo kwaanza umemfungia spika akukoromee vizuri.huyu mh mimi siwezi kumvumilia.mwanamke asiyekua na mawazo ya maendeleo au mume ni shids kubwa.lamwisho na kubwa tena lenye madhara zaidi michepuko maisha ya kila kukicha unakutana na sms za michepuko yake kila unavyomueleza hakuelewi.unakaa usubiro nini?ukimwi au watoto wa kambo? tena ambao hawezi kuwalea