Habari zenu,
Mara nyingi wanandoa huambiwa au hushauriwa swala zima la UVUMILIVU huenda ikawa kabla ya kuingia kwenye ndoa au hata baada ya kuingia kwenye ndoa.
Lakini nimeona kama watu hawa wenye busara zao kama wazee/wazazi au viongozi wa dini huwa hawasemi huu UVUMILIVU UWE TO WHAT EXTENT.
Mfano unakuta mwanamke anapigwa na mumewe au mwanaume anapigwa na mkewe lakini akienda kwa viongozi wa dini au wazee/wazazi wanamwambia avumilie tu ndio ndoa zilivyo.
Ndipo nilipopata hili swali HUU UVUMILIVU HAUNA KIKOMO humu ndani najua kuna watu wenye busara na hekima najua tutapata cha kujifunza.
Ni hayo tu.
KARIBUNI..........
Kwani haujui mvumilivu hula mbivu???
Kikomo cha uvumilivu ni pale utakapo tokwa na uhai, lakini " UVUMILIVU HAUNA MIPAKA, MIPAKA HULETWA NA MAADUI WA UVUMILIVU" . Na ili uitwe uvumilivu ni lazima iwe kwenye mambo magumu na mazito
Kumbuka katika kila jambo unatakiwa uwe na kiasi
ndugu yangu
kwenye ndoa huko uvumilivu usio na kikomo na ukikoma bas ndo mwisho wa kila kitu
Hakuna kiongozi wa imani anayetoa nasaha kwa mwanandoa anayeumia kuwa na uvumilivu hususani linapokuja suala lolote ambalo ni tatizo ndani ya ndoa...
La hasha, endapo kutakuwa na matumizi ya neno 'vumilia' basi ujue ni katika harakati za kupata usuluishi...
Hivyo basi mtu huambiwa avumili kwa mantiki kuwa uvumilivu na usubiri suluhisho la kadhia inayoendelea...
Kikomo cha uvumilivu ni pale utakapo tokwa na uhai, lakini " UVUMILIVU HAUNA MIPAKA, MIPAKA HULETWA NA MAADUI WA UVUMILIVU" . Na ili uitwe uvumilivu ni lazima iwe kwenye mambo magumu na mazito
Kwani kuna asie jua kua mvumilivu hula mbivu
kwa upande wangu kuna mambo ya kuvumilia lakini kipigo sio mojawapo.....