Uvumilivu huu mpaka lini?

Mangaline

JF-Expert Member
May 19, 2012
1,045
221
Katika hotuba ya msemaji mkuu wa kambi ya upinzani mheshimiwa vincent josephat nyerere (mb), kuhusu makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2012/2013 wizara ya mambo ya ndani ya nchi, imeonesha wazi kuwa upo upendeleo wa wazi wa vyombo vya dola kwa makusudi, kuonea, kunyanyasa na kudhulumu masilahi ya watu walio na msimamo ulio kinyume na matakwa ya utawala. Wapo wenzetu wengi wamepoteza maisha, na wengine wanashikiliwa na vyombo vyenye nguvu kwa dhuluma. Hata hivyo, umma unaendelea kuangalia na kuona kama kila anayefikwa madhara hayo, yeye hayamuhusu, bila kujua kesho ni zamu ya nani???? Fikiria yaliyo wapata wenzetu kwenye mkutano halali, kwa kufanyiwa fujo, na mwisho wa siku, wao ndiyo wanashikiliwa na polisi kwa mauaji. Fikiria yaliyompata Dr. uli, na bila aibu, vyombo vyenye nguvu vinatoa majibu ya kejeli na dharau kwa umma, kana kwamba wanaongea na watu wasio na fikira.
Hivi, uvumilivu huu, watanganyika tutaendelea nao hadi lini????????????????????????????????????????????????????


 
Back
Top Bottom