Uvumbuzi wa kurunzi iletayo giza

Wasalaam,

Ndugu zangu msione ukimya mwingi umetamalaki kuhusiana na "Theory of Mbenge Effect". Ni shughuli pevu na yenye kuweza kuleta dhana mpya kabisa katika ulimwengu wa sasa wa sayansi, na hata kuweza kubadilisha mtazano mzima pamoja na kanuni nyingi za msingi zilizopo nyuma ya nishati ya mwanga.

Nasikitika sana kusema kuwa katika kundi letu lililokuwa lenye waatalamu wa kisayansi wapatao 12 kwa pamoja tuliuanza mchakato huu, mmoja wetu amegeuka kuwa Yuda Eskaroti na kuleta madhara kwa kiwango cha kadiri ya 15% na kuweza kuharibu "original plan & deadlines"

Kumbuka namba 12 ina maana kubwa sana katika ulimwengu wa kiroho ili kuweza kukamilisha jambo fulani. Ni lazima tufanye replacement ili timu iwe kamilifu kupitia namba hii.

"Damage control" imekwisha kufanyika, na kanuni mpya ya kimahesabu ipo tayari na nitakuja kuweka dokezo lake hadharani hivi karibuni. Mimi na timu yangu tunalazimika kufanya mabadiliko hayo ili tuzidi kuhifadhi na kuweka usiri mkubwa katika kazi yetu ya msingi


Lakini kabla hata hatujafanikiwa kuiweka kazi yetu katika "live state" ya majaribio, yaani tukiwa bado tupo katika "demo" tunaona kuna kila dalili za uwepo wa tishio la shambulizi la kimtandao kutoka kwa mahasimu wetu, .Ahadi ni deni, kila kitu kitakuwa katika mikono salama, mpaka dhamira yetu itimie.
 
Dunia ya sasa inaendeshwa kupitia kanuni za sayansi na teknolojia ambazo zilivumbuliwa na wanasayansi katika karne zilizopita. Kanuni hizi siamini kuwa zinazima ndoto ya uvumbuzi wa kanuni mpya ambazo zinaweza kuja na majibu katika maeneo mengine mapya ambayo uvumbuzi mpya bado haujafanyika mpaka hivi sasa.

Eneo mahususi ambalo mimi binafsi nataka kulifanyia kazi ni kupata sayansi ambayo itakuwa kinyume na hii ya sasa katika nishati ya mwendo wa mwanga pamoja na chanzo chake. Ni lazima nitoe pongezi zangu kwa TANESCO kupitia mgao wao usioisha wa umeme, jambo ambalo limemiwezesha kuja na wazo hili kuhusu uvumbuzi huu wa kisayansi ninaotegemea kwenda kuufanya.

Nikianza na nadharia ya kifaa hiki kipya, kitafanya kazi kinyume kabisa na vile ambavyo kurunzi za kawaida zinazotoa mwanga zinavyofanya kazi. Kwa kuanzia, mimi na timu yangu ya wataalamu tutaingia chaka ili kujifunza kuhusu nishati hasi ambapo endapo ikiachiwa itatengeneza nguvu hasi na kupelekea giza ama kivuli kutokea mara moja, kwa hiyo basi mwanga kutoweza kupita hali itakayopelekea giza kutokea na kutawala "automatically on the surface under influence"

Athari ya kanuni ya nishati hii hasi dhidi ya mwanga itaitwa "mbenge effect" na ili iweze kufanya kazi zake kwa ukamilifu uliokusudiwa itabidi itegemee "formular" ya kimahesabu na kiithibati ili kukidhi mfumo mpya wa kanuni ya vichochezi hasi yaani "mbe" ambacho kitawakilishwa na alama ya na "nge' ambacho alama yake itakuwa ni

Kwa hiyo ukitaka ku "generate
"mbenge effect" itabidi kanuni ifuatayo itumike

1/+2/+3/

Kwa leo basi tuishie hapa, kwa kuwa sina "background" ya sayansi, ngoja kwanza nitafute jopo la baadhi ya wanasayansi ili niuze wazo hili kwao na tuanze kulifanyia kazi mara moja. Stay tune kwa mrejesho.
Mawazo yetu mazuri hudumazwa na serikali yetu. Niliwahi kufikiria mambo mengi nikiwa mdogo, mfano umeme usioisha wala kuzima. Nikagundua sina akili ya kusoma fizikiq na hesabu kulingana na idadi ya mambo niliyowaza. Nikawaza pia taa zinazoweza kuleta giza totoro japo niliwaza hili kwa usiku pekee kwasabbu kuna muda giza totoro linahitajika yaani hata mbalamwezi isionekane
 
"Nikawaza pia taa zinazoweza kuleta giza totoro japo niliwaza hili kwa usiku pekee kwasabbu kuna muda giza totoro linahitajika yaani hata mbalamwezi isionekane* - Nukuu.
Mawazo yetu mazuri hudumazwa na serikali yetu. Niliwahi kufikiria mambo mengi nikiwa mdogo, mfano umeme usioisha wala kuzima. Nikagundua sina akili ya kusoma fizikiq na hesabu kulingana na idadi ya mambo niliyowaza. Nikawaza pia taa zinazoweza kuleta giza totoro japo niliwaza hili kwa usiku pekee kwasabbu kuna muda giza totoro linahitajika yaani hata mbalamwezi isionekane
You have nailed it.
 
Ugumu unakuja ni kwamba giza sio energy,ni matokeo tu ya kukosa mwanga.
Kwahiyo nguvu ielekezwe ktk kuondoa mwanga,sijajua tochi yetu itazalisha wingu,kivuli,ama nini!!!
 
hii
Screenshot_20240327_223643_YouTube.jpg
 
Back
Top Bottom