Uvimbe!!

Bepari

JF-Expert Member
Feb 17, 2011
904
329
Wakuu nina tatizo. Kuna uvimbe umejitokeza chini ya shavu la kulia.

Nilienda hospitali wiki mbili zilizopita wakaniambia ni aleji na kunipa ethromaizin kutumia kwa wiki mbili, niliambiwa lengo ni kuuivisha upasuke kama jipu.

Dozi nimemaliza na hakuna dalili ya kupasuka japo uvimbe umepungua, tatizo jipya ni kwamba kwa sasa ni kama uvimbe una ganzi yaani nikiugusa siwezi kuhisi.

Mtu yeyote mwenye aidia ya tatizo langu anisaidie tafadhali...
 
Mkuu upo wapi? Umewahi kupaka dawa ya meno kwenye uvimbe? Au uliwahi kupaka unga wa choroko? Hizi dawa husaidia kuivisha jipu upesi.ila kama ni jipu kweli.
 
Wakuu nina tatizo. Kuna uvimbe umejitokeza chini ya shavu la kulia. Nilienda hospitali wiki mbili zilizopita wakaniambia ni aleji na kunipa ethromaizin kutumia kwa wiki mbili, niliambiwa lengo ni kuuivisha upasuke kama jipu. Dozi nimemaliza na hakuna dalili ya kupasuka japo uvimbe umepungua, tatizo jipya ni kwamba kwa sasa ni kama uvimbe una ganzi yaani nikiugusa siwezi kuhisi. Mtu yeyote mwenye aidia ya tatizo langu anisaidie tafadhali...

Hiyo ndiyo dawa gani?cha msingi nenda hospitali(siyo za vichochoroni).

Daktari ata identify huo ni uvimbe gani.Kama ni jipu watalifanyia drainage kisha watakupa antibiotics na mchezo utakuwa umekwisha.
 
Maelezo waliokupa ya tatizo na dawa waliyokupa yanapishana!!! Allergy hutibiwa kwa kutumia antihistamine (kama chlorphenamine aka PIRITON) au wanaweza kukupa steroid kama Prednisolone ....Erythromycin ni antibiotic (dawa ya kuua bacteria) si dawa ya kuivisha jipu!! ---Lakini antibiotics inaweza kutumiwa kutibu jibu kwani mara nyingi majipu husababishwa na bacteria!!! >>>>Daktari inabidi atofautishe katika ya uvimbe unaosababishwa na allergy na ule unasababishwa na bacteria!!!

Uvimbe upo kwa ndani (ya mdomo) au nje!

Dawa ya kuivisha jipu kama ni jipu kweli ni Magnesium Sulphate Paste ambayo unapaka halafu unafunika na bandage (vizuri ufanye hivi usiku wakati unalala!!) nafikiri ndani ya siku moja au mbili jipu litaiva/ pungua!
 
Back
Top Bottom