UVCCM Zanzibar wamwashia moto Makamba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

UVCCM Zanzibar wamwashia moto Makamba

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by oyoyoo, Jan 13, 2011.

 1. o

  oyoyoo Member

  #1
  Jan 13, 2011
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 55
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Waungwana, nina kipande cha taarifa kilichonifikia punde kikionyesha kuwa hali ya UVCCM bado si shwari na safari hii uongozi wake uliopo Zanzibar umempiga barua Katibu kilaza Makamba ili ahakikishe wanafanya uchaguzi wa Mwenyekiti na kuziba nafasi ya Naibu Katibu Mkuu Zanzibar.

  Soma taarifa hii: Source Intelejensia cables


  Mhe. Rajab Yussuf Makamba,
  Katibu Mkuu CCM,
  Dar es salaam.
  12/01/2011
  YAH: HALI YA KISIASA NDANI YA JUMUIYA YA UMOJA WA VIJANA WA CCM (UVCCM)
  Kwa heshima na taadhima, sisi wajumbe wa Baraza Kuu la UVCCM na Wenyeviti wa Wilaya wa Mikoa yote mitano ya Zanzibar pamoja na baadhi ya Wenyeviti wa Mikoa ya Tanzania Bara ambao majina na sahihi zetu zimeorodheshwa, tumeamua kwa pamoja na kwa niaba ya vijana walio wengi wa CCM Tanzania nzima kuwasilisha waraka huu kwako ili uwasilishe kwa Mwenyekiti wa CCM Taifa na wajumbe wote wa Kamati Kuu watambue msimamo wetu kuhusu hali inavyoendelea ndani ya Jumuiya yetu ili waweze kuchukua hatua stahili kwa maslahi mapana ya Chama chetu kwa ujumla wake.
  Kwanza kabisa tunaomba kuchukua fursa hii kutoa shukurani na pongezi zetu za dhati kabisa kwa Mwenyekiti wetu mpendwa wa CCM Taifa, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na wajumbe wote wa Kamati Kuu kwa busara waliyotumia kutoa maamuzi yaliyopelekea nafasi ya Mwenyekiti UVCCM Taifa kwenda Zanzibar. Tunaimani kuwa nia hii njema ya viongozi wetu imesaidia sana kuimarisha muungano wetu kwa maslahi ya nchi zetu mbili zilizoungana na kuzaliwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mnamo tarehe 26/04/1964. Sote tunaamini kuwa hikma na busara alizozionesha Mwenyekiti wetu wa CCM kupitia uamuzi huu zinatokana na mapenzi makubwa aliyonayo kwa nchi yetu. Sisi vijana wa CCM tunaahidi daima kuwa watiifu kwake na kuwa tutaendelea kuenzi juhudi na falsafa za viongozi kama Mhe. Kikwete, Hayati Mwalimu Nyerere, Hayati Sheikh Karume na wengineo za kusimamia misingi ya udhati na uwajibikaji.
  Kwa masikitiko makubwa leo hii kwa pamoja tumeamua kuleta kwenu malalamiko yetu baada ya kubaaini mapungufu makubwa ya kiuongozi ndani ya Jumuiya yetu, pamoja na ukiukwaji mkubwa wa Kanuni yetu ya UVCCM kama ambavyo inafafanuliwa chini:
  1. Kwa mujibu wa Kanuni ya UVCCM Ibara 91 (i) Kamati Tekelezaji inatakiwa ikae mara Moja kila baada ya miezi minne, tokea Makamo Mwenyekiti kuanza kukaimu nafasi ya Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Kamati Tekelezaji ilipaswa iitishwe mara mbili lakini tokea wakati huo mpaka sasa hakuna kikao hata kimoja cha kikanuni kilichoitishwa chini ya uongozi wa sasa;

  1. Ibara 100(1) inasema kuwa Naibu Katibu Mkuu mmoja ataishi na kufanya kazi zake Zanzibar, lakini mpaka sasa hakuna jina la mtu yoyote kutoka Zanzibar aliependekezwa kukaimu nafasi hiyo na Jumuiya. Kwa upande wa Zanzibar UVCCM inaendeshwa bila kuwa na mtendaji mkuu, hali iliyosababisha UVCCM iingie uchaguzi mkuu wa 2010 ikiwa haina kiongozi wa juu kati ya Mwenyekiti na Naibu Katibu Mkuu;

  1. Kwa mujibu wa Ibara 91(d). Kamati ya Utekelezaji ya Taifa ndio itakuwa na mamlaka ya kuidhinisha na kudhiti matumizi na malipo yote ya fedha za Umoja wa Vijana wa CCM, kwa kuwa hakuna kikao hata kimoja cha kinanuni kilichoitishwa kwa maamuzi, matumizi ya fedha na rasilimali za Jumuiya yamekuwa yakitumika bila mpangilio wala usimamizi, hasa wakati wa mchakato wa uchaguzi mkuu uliopita;

  1. Ibara ya 107 (a) Baraza la Udhamini ndio lenye mamlaka ya kusimami mali za Jumuiya, lakini katika hali ya kushangaza kuna baadhi ya miradi ikiwemo mradi wa Jengo la Darajani umekuwa ukiendelea bila idhini ya Baraza la Wadhamini huku mpango mkakati wa muda mrefu wa kuliendeleza eneo lote la Darajani ulioasisiwa na vikao halali vya Kamati Tekelezaji na Baraza Kuu vilivyopita vikitiwa kapuni;


  1. Ibara ya 95 Inasomeka endapo Mwenyekiti atatoka Tanzania Bara, Makamu atatoka Tanzania Zanzibar au kinyume chake. Kuna wazanzibari wengi wenye uwezo na sifa ya angalau kukaimu nafasi ya Mwenyekiti. Makamo Mwenyekiti anahofu ya kuitisha kikao cha Baraza Kuu Taifa, ambacho ndicho pekee chenye mamlaka ya kukaimisha nafasi ya Mwenyekiti Taifa mpaka sasa;

  Hivyo basi, sisi wajumbe wa Baraza Kuu Taifa na Wenyeviti wa Wilaya tunaona kuwa kuna umuhimu na uharaka wa kuitishwa Baraza Kuu la UVCCM Taifa ili hatua ya kwanza ikiwa ni kuchagua Mwenyekiti wa UVCCM haraka sana kabla ya ajenda nyengine yoyote kuwekwa mezani.

  Tunaamini kuwa Chama ndicho chombo pekee chenye uwezo wa kuingilia kati pale panapotokea uvunjifu wa taratibu na kanuni za Jumuiya kwa makusudi, kwa kumshinikiza Makamo Mwenyekiti asiendelee kuzuia kikao cha Baraza Kuu Taifa ili kujadili masuala yenye mustakabali mwema kwa Jumuiya na Chama kwa ujumla wake.

  Tunaomba kuwasilisha.
  Nakala: Mheshimiwa Mwenyekiti wa CCM Taifa
  Waheshimiwa Makamo Mwenyekiti Bara na Zanzibar
  Waheshimiwa Wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM

  Wajumbe wa Baraza/Wenyeviti wa Wilaya Sahihi

  1.
  2.
  3.
   
 2. Najijua

  Najijua JF-Expert Member

  #2
  Jan 13, 2011
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 1,029
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Mbona majina na sahihi hayapo kama yanaukweli?inawezekana umeandika wewe, verify beyond reasonable doubt
   
 3. Joseph

  Joseph JF-Expert Member

  #3
  Jan 13, 2011
  Joined: Aug 3, 2007
  Messages: 3,527
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Ukitaka tuamini ukweli wa habari hii ungetuletea na sahihi zao ili tuelewe kuwa barua hii imefika,inawezekana iliandaliwa tu tena katika mazingira ambayo hayakuwa ya kiofisi ndio maana hata wewe umeweza kupata nakala.
   
 4. The Hunter

  The Hunter JF-Expert Member

  #4
  Jan 13, 2011
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 1,049
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Malisa anaogopa kivuli chake, aitishe uchaguzi aone kama atabaki
   
 5. PMNBuko

  PMNBuko JF-Expert Member

  #5
  Jan 13, 2011
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 971
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni vigumu kuamini jambo hili. Japokuwa inaawezekana maana CCM sasa imeparanganyika.
   
 6. o

  oyoyoo Member

  #6
  Jan 13, 2011
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 55
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Subiri usome magazeti kesho ndio ujue kuwa Oyooyoo ni mtu wa kufunua nyeti
   
 7. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #7
  Jan 13, 2011
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  ah inachosha kusoma hata kama ni nzuri,so long as inahusu ccm tupa kule usichafue jamvi
   
 8. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #8
  Jan 13, 2011
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,865
  Likes Received: 11,980
  Trophy Points: 280
  Mbwa anambwekea mwenye mbwa kazi kweli kweli.
   
 9. Bantugbro

  Bantugbro JF-Expert Member

  #9
  Jan 13, 2011
  Joined: Feb 22, 2009
  Messages: 2,684
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Si unajua mi-mbwa mingine huwa inakuwaga na kichaa [kifaduro] haikawii hata ku-muuma mwenyewe....
   
 10. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #10
  Jan 13, 2011
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,865
  Likes Received: 11,980
  Trophy Points: 280
  Dawa yake ni kumnyima chakula na mnyororo juu.
   
 11. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #11
  Jan 13, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  Mbona hizo bullet zote ni tarakimu moja (1); hau ndio UVcCM Zenji hawakuakiki barua yao kabla ya kuyuma
   
 12. o

  oyoyoo Member

  #12
  Jan 14, 2011
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 55
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nipashe front page have covered this story. I think there are things moving lets wait and see. Wakifa wao CDM tunatoka na CDM tunatakiwa kuwafatilia kwa ukaribu zaidi na kuwaacha wachanganyane kisha tunapita katikati yao na kushika dola, Slaaa oyeeeeee!
   
 13. BIN BOR

  BIN BOR JF-Expert Member

  #13
  Jan 14, 2011
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 752
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Wanasema hawana kaimu mwenyekiti! Si Riz1 yupo!
   
Loading...