UVCCM Yataja Sifa Za Mgombea Urais Ajaye!

UVCCM Yataja Sifa Za Mgombea Urais Ajaye!

chakii

JF-Expert Member
Joined
Sep 15, 2013
Posts
21,565
Reaction score
28,475
UMOJA wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) umetaja sifa za mgombea urais, anayetakiwa kugombea kupitia chama hicho katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu.

Akizungumza jana, Katibu Mkuu wa Taifa UVCCM Taifa, Sixtus Mapunda alisema "Mbali na sifa 14 za miaka yote tunazozifahamu, sifa kuu kwa mazingira ya siasa za sasa ni CCM kuwa na mgombea anayekijua chama vizuri, ndani na nje."

Alisema CCM inahitaji mgombea wa aina hiyo, kwa sababu mbali na kwamba ndiye atakayekuwa Rais wa Tanzania, lakini pia atakuwa Mwenyekiti wa CCM wa Taifa.

Alitaja sifa nyingine kuwa ni lazima awe mchapakazi, anayekubalika na kupendwa na watu, mpenda watu, mpenda amani na muungano na asiwe na ubaguzi wowote.

Alisema pamoja na sifa hizo, CCM inahitaji mgombea atakayekubali Tanzania ianze na moja kwa kuwashawishi wananchi wakubali kujifunga mkanda kwa kuanza kufanya mambo machache, lakini yatakayosambaza neema katika maeneo mengine kwa muda mfupi.

"Ni lazima ayapunguze au asitishe matumizi yote yasiyo ya lazima ili kuimarisha matumizi yanayoweza kuongeza tija katika maeneo yanayoweza kufungua neema nyingine," alisema.

Mapunda alisema CCM inahitaji mgombea ambaye ni rafiki wa vijana, anayezijua changamoto zao na mwenye mipango inayoelezeka ya namna ya kuzishughulikia.

"Zipo changamoto kubwa mbili zinazowakabili vijana wa Tanzania, nazo ni elimu na ajira. Kwa upande wa elimu ni lazima aje na mikakati itakayotoa fursa kwa vijana wengi kupata elimu ya msingi hadi chuo kikuu na kwa upande wa ajira ni lazima aje na mipango itakayowezesha kuzalisha ajira nyingi hasa katika sekta binafsi," alisema.

Alisema matarajio ya CCM katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu ni kuunda serikali ya awamu ya tano, kwa sababu bado ni chama imara, kinachokubalika na watu na kina idadi kubwa ya wagombea wenye sifa lukuki katika nafasi mbalimbali.

Chanzo: Habari Leo
 
kwa sifa hizo wote waliotangaza nia kwa upande wa chama cha mapinduzi hakuna hata mmoja
 
Kila kiongozi ndani ya hivi vyama anataja sifa za Rais amtakaye. Ukiziangalia sifa hizo zinamwelekea mtu wa kundi lake...au yeye mwenyewe!
 
kwa sifa hizo wote waliotangaza nia kwa upande wa chama cha mapinduzi hakuna hata mmoja

mkuu huwa napata shida sana kufahamu hizi sifa huwa zinajificha sisi hatuzioni au huwa zinashushwa kwa mtu kama zilivyoshushwa amri kumi.

Ndani ya ccm kuna miujiza mingi sana inatokea.
 
Hamna mtu wa namna hiyo ccm... labda mkaombe mgombea nje ya nchi...shenz
 
mwelekeo wa maneno ya huyo kiongozi wa uvccm unaonesha wazi yeye ni mtu wa lowasa
 
Ni hao hao UVCCM mwaka 2012 kupitia tamko lao kuu la taifa kutokea kwenye kikao chao cha Bagamoyo walisema mgombea urais wa CCM 2015 kamwe hawezi kutokea kaskazini.

WanaUVCCM wengine wakaja na sifa zao mwaka huu mwanzoni na kusema wanataka mgombea kijana.

Juzi pia kiongozi wao mmoja wa juu alikuja na kusema UVCCM tunataka mgombea urais awe na Afya njema na asiwe mgonjwa anayesafiri mara kwa mara kwenda nje kutibiwa.

Leo huyu Sixbat Mapunda anasema wanataka mgombea wa CCM awe mtu wa kufunga mikanda kiuchumi(Bahili).

Sasa kwa majumusho yangu, UVCCM kwa ujumla na kifupi kabisa wanasema wanataka mgombea wa CCM awe
1/Mtu asiyetokea mikoa ya Kaskazini.
2/Mwanasiasa kijana.
3/Mwanasiasa asiye mgonjwa.
4/Mwanasiasa Bahili.
 
Usiwe unatumia akili ya kukodi
 
Sixtus mapunda yeye timu nani?

Mkuu kwa maneno hayo naona jamaa ni timu Lowasa, labda urudie kuyasoma tena vizuri.....hapo kwenye ajira,elimu na vijana ni mambo anayoyasimamia Lowasa kwa uwazi kabisa, kuchapa kazi na kukijua chama, kukubalika na mengineyo ndani ya ccm.....kwa hayo naona hakuna mwingine zaidi ya LOWASA, bado ni muendelezo ule ule wa Makundi.
Jamaa kanifurahisha aliposema atufungishe mkanda tuanze, niwazi anajua wa sasa kaboronga so inabidi tuanze upya.
 
Ni hao hao UVCCM mwaka 2012 kupitia tamko lao kuu la taifa kutokea kwenye kikao chao cha Bagamoyo walisema mgombea urais wa CCM 2015 kamwe hawezi kutokea kaskazini.

WanaUVCCM wengine wakaja na sifa zao mwaka huu mwanzoni na kusema wanataka mgombea kijana.

Juzi pia kiongozi wao mmoja wa juu alikuja na kusema UVCCM tunataka mgombea urais awe na Afya njema na asiwe mgonjwa anayesafiri mara kwa mara kwenda nje kutibiwa.

Leo huyu Sixbat Mapunda anasema wanataka mgombea wa CCM awe mtu wa kufunga mikanda kiuchumi(Bahili).

Sasa kwa majumusho yangu, UVCCM kwa ujumla na kifupi kabisa wanasema wanataka mgombea wa CCM awe
1/Mtu asiyetokea mikoa ya Kaskazini.
2/Mwanasiasa kijana.
3/Mwanasiasa asiye mgonjwa.
4/Mwanasiasa Bahili.
Uchambuzi umetulia sana huu
 
Back
Top Bottom