UVCCM Wilaya ya Iramba wamvaaa Membe, wampa onyo kali

Kidugu

Member
Apr 19, 2020
23
38
Jumuiya ya umoja wa vijana WA CCM Wilaya ya Iramba mkoani singida Imemtumia salamu aliyekuwa mwanachama wa CCM Bernard Membe na baadae kufukukuzwa uanachama na Kamati Kuu.

Jumuiya hii kupitia kwa mwenyekiti wake comrade Joseph Mnemba imesema kuwa haitamvumilia mtu yeyote anaepingana na Mwenyekiti wa chama hicho Dr John Pombe Magufuli kwa gharama yeyote.

"Hatuwezi kuwa na watu wanaotaka kutuharibia nchi kama kina Membe, wamekitumikia chama, wametumikia serikali, imefika muda wanaenda tofauti na maelekezo ya chama ni lazima wakae pemben wamuache Rais wetu kipenzi cha Watanzania afanye kazi, tunampenda Sana Rais wetu. Kama wanatumika, wajitathmini upya. Vijana hatutakubali Rais wetu aayumbishwe na watu wachache wenye tamaa"

Alisema M/kiti huyo, CD Mnemba

 
Kwani Yesu wenu hana tamaaa si alisema urais ni kazi ngumu,sasa si awaachie wengine kwa nini mnazuia watu wasitumie haki yao ya kidemokrasia na kikatiba kugombea
 
Kidugu wani kutumile! Mamila makoo! Unatumika na Dkt. Mwigulu sio. Usije Simba lazima tukudeal wewe!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…