Lizaboni
JF-Expert Member
- Feb 21, 2013
- 33,894
- 20,390
Wadau, amani iwe kwenu.
Hapa ndipo tunapoona tofauti ya chama kama taasisi na chama kama mali ya mtu binafsi. Ukitaka kuona tofauti baina ya vyama vya aina hiyo, basi huna budi kuangalia jinsi CCM na CHADEMA wanavyofanya harakati za Kujenga chama.
Ka upande wa CCM, mara zote harakati za kujenga chama husimamiwa na Taasisi zake kama vile Umoja wa Vijana ( UVCCM), Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) na Umoja wa Wazazi. Tukiangalia harakati zinazoendelea sasa, UVCCM wamejipanga kimkakati zaidi na wamesambaa kila kona ya nchi hii kuhakikisha kuwa wanatumia vema muda huu wa vyama vya upinzani kuchanganyikiwa baada ya CCM kubadili aina ya siasa kutoka siasa za upole na kuvumiliana hadi siasa za kutumbua majipu. Kwa hakika aina ya sasa ya siasa imekijenga sana CCM na kinaungwa mkono na watu wengi ambao awali walikuwa upinzani.
Huko Morogoro, UVCCM imevuna wanachama wapya 100 na kwamba wimbi hilo linajitokeza katika mikoa kadhaa ya nchi. Hakika nimeipenda sana hii ya CCM kwani huwezi kuzunguka nchi nzima peke yako ama kwa kusaidiwa na Salum Mwalimu pekee then ukategemea unajenga chama. Haya ni maigizo na ni mazingaombwe.
Wanachofanya CHADEMA sasa ni kama wamesusa kushiriki harakati za kisiasa na kwamba wana mgomo baridi kutokana na chama hicho kuhodhiwa na Lowasa pamoja na kitendo cha Mbowe kumteua Mashinji kuwa Katibu Mkuu wa chama hicho mtu ambaye hafanani hata kwa sekunde na Dr Slaa. BAWACHA, BAVICHA and son wamepotea kabisa.
Lazima tuheshimiane.