UVCCM wameionya BAVICHA, yasema itapambana nao kama vita vya Maumau kenya

Kakke

JF-Expert Member
Dec 4, 2010
1,883
1,482

Monday, July 4, 2016

Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM, Shaka Hamda Shaka

Umoja wa Vijana CCM (UVCCM) umeingia katika mvutano mkubwa na Baraza la Vijana wa CHADEMA (BAVICHA) kuhusu Mkutano Mkuu Maalum wa chama hicho tawala uliopangwa kufanyika Julai 23 mwaka huu mjini Dodoma.

UVCCM wameionya BAVICHA kuhusu mpango wao wa kutaka kukusanyika mjini Dodoma siku hiyo kwa lengo la kuzuia mkutano huo kwa madai kuwa unakiuka amri halali ya polisi ya kupiga marufuku kufanyika kwa mikutano yote ya kisiasa nchini.

Onyo hiyo limetolewa na Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM, Shaka Hamda Shaka ambaye aliwaambia waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam kuwa watawakabili kwa nguvu zote BAVICHA endapo wataamua kuendesha siasa zinazolenga kuvuruga amani na kuleta hofu katika jamii na kutishia maisha.

Alisema umoja huo hautaona shaka kutumia mbinu zilizotumiwa na wapiganaji wa Maumau miongo kadhaa iliyopita nchini Kenya.

“Hatutaona muhali kupita njia zilizotumiwa na wapiganaji wa Maumau wa Kenya ili kukihami chama, kulinda viongozi wake na kupigania hadhi na heshima yetu,” alisema Kaimu Katibu Mkuu huyo wa UVCCM.

CCM inatarajia kufanya mkutano mkuu maalum Julai 23 mwaka huu ambapo Rais John Magufuli atakabidhiwa rasmi uenyekiti wa chama hicho kutoka kwa mtangulizi wake, Dk. Jakaya Kikwete.

Advertisement

Mpekuzi Blog
==

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Mpekuzi Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

kakosea sana kuongelea mambo ya maumau, bora angetafuta neno lingine, manake hiyo ni kauli ya vitisho sana, na kauli hizo ndio wanasema zinachochea uvunjifu wa amani kama tundu alivyosema wakasema ni lugha ya kuvuruga amani, bora wangekaa kimya tu kuliko kutoa kauli hiyo, hebu jamani mnaposema maneno, muwe mnaweka na akiba ya maneno, msibwatuke, kauli ya uvccm sijaipenda kama ni kweli imetamkwa hivyo leo,
 
Hili nalo bhana, wapi BAVICHA wamesema wanataka kupigana, mijitu mingine ina akili za ajabu kweli kweli aiseeee dah, eti ndio wasomi wa CCM hao, wakizeeka si watakua wachawi hawa
 
CHADEMA hawa n tabu sana? Yaan jamaa kama kawaida yao kaamua kujitoa akili na kuongea utumbo mtupu, xaxa iyo Vita anamtangazia nan? Kwan BAVICHA wametangaza vita lin? Kama sio uchochez
 
Msisubutu kuja kutuzuia bavicha .. Tutawatandika kweli mkashitaki vizuri kwa mwenyekiti wenu
 
Monday, July 4, 2016

Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM, Shaka Hamda Shaka

Umoja wa Vijana CCM (UVCCM) umeingia katika mvutano mkubwa na Baraza la Vijana wa Chadema (BAVICHA) kuhusu Mkutano Mkuu Maalum wa chama hicho tawala uliopangwa kufanyika Julai 23 mwaka huu mjini Dodoma.

UVCCM wameionya BAVICHA kuhusu mpango wao wa kutaka kukusanyika mjini Dodoma siku hiyo kwa lengo la kuzuia mkutano huo kwa madai kuwa unakiuka amri halali ya polisi ya kupiga marufuku kufanyika kwa mikutano yote ya kisiasa nchini.

Onyo hiyo limetolewa na Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM, Shaka Hamda Shaka ambaye aliwaambia waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam kuwa watawakabili kwa nguvu zote BAVICHA endapo wataamua kuendesha siasa zinazolenga kuvuruga amani na kuleta hofu katika jamii na kutishia maisha.

Alisema umoja huo hautaona shaka kutumia mbinu zilizotumiwa na wapiganaji wa Maumau miongo kadhaa iliyopita nchini Kenya.

“Hatutaona muhali kupita njia zilizotumiwa na wapiganaji wa Maumau wa Kenya ili kukihami chama, kulinda viongozi wake na kupigania hadhi na heshima yetu,” alisema Kaimu Katibu Mkuu huyo wa UVCCM.

CCM inatarajia kufanya mkutano mkuu maalum Julai 23 mwaka huu ambapo Rais John Magufuli atakabidhiwa rasmi uenyekiti wa chama hicho kutoka kwa mtangulizi wake, Dk. Jakaya Kikwete.

Advertisement

Mpekuzi Blog
==

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Mpekuzi Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )

Home
View web version

LEARN MOREGOT IT

Kwani huyu jamaa si ndo walisema kahamia Mombasa??
 
Am keep watching these Series of Movies ktk nchi ya Kusadikika,ngoja tuone Intelijensia ya uvunjivu wa amani...itachukua hatua gani na hapa ndiyo mbivu na mbichi kujulikana na Double standards.
 
kakosea sana kuongelea mambo ya maumau, bora angetafuta neno lingine, manake hiyo ni kauli ya vitisho sana, na kauli hizo ndio wanasema zinachochea uvunjifu wa amani kama tundu alivyosema wakasema ni lugha ya kuvuruga amani, bora wangekaa kimya tu kuliko kutoa kauli hiyo, hebu jamani mnaposema maneno, muwe mnaweka na akiba ya maneno, msibwatuke, kauli ya uvccm sijaipenda kama ni kweli imetamkwa hivyo leo,
Ila ya bavicha umeipenda
 
Back
Top Bottom