MAHANJU
JF-Expert Member
- Aug 26, 2014
- 5,244
- 7,966
Ndugu zangu vijana wangu na wanaccm tuache unafki na ubishi usiokuwa na sababu. Hivi anayoyasema mwenyekiti Heri James kuna kipi kipya hapo? Tunabisha kitu gani kama kweli tunataka kulijenga taifa kwa pamoja?
Tuache ujinga, tusitake kulazimisha mambo wakati tunajua kabisa kuna uwezekano wa mfumo wetu wa uendeshaji wa Chama na serikali ukabadilika. Mama Samia ni Mwanaccm mwenzetu na ni lazima atekeleze ilani ya chama. Lakini tunachotakiwa kufahamu ni kila mtu na utashi wake na ni lazima uongozi wa Mama utofautiane na wa Magufuli maana huyu ni Samia na yule ni Magufuli.
Kwa sasa Mama ndiye mwenye power ndani ya Chama na serikali, tukijifanya jeuri kwa mamlaka ya ndani ya katiba ya chama na ile ya Jamuhuri mamama akiamua anapanga timu yake anayoitaka itakayomsaidia kutekeleza ilani ya Chama. Sisi tudipoeleweka atatafuta timu nyingine ya kufanya nae kazi tuache porojo.
Mwenyekiti wetu Heri James ni mtu mwenye akili nyingi sana, anajua fika kabisa mazingira ya siasa za sasa ni lazima yatofautiane na ya sasa. Kwani uongo kwamba tulitumia nguvu nyingi kuendesha siasa zetu nje na ndani ya chama? Tunapokumbuka pale tulipoharibu na kutaka tuishi vizuri na ndugu zetu tuliokwisha wakwaza kuna tatizo gani?
Kama Mama yetu nafsi yake itakua na na amani akiona anaongoza taifa lenye amani na upendo kuna tatizo?
Mwisho na Muhimu.Tusitake kuanza kujenga makundi yatakayotoa faida kwa wapinzani wetu.Tufungamane na mwenyekiti wetu wa Jumuiya yetu na wa chama taifa, tuache kua wanafiki.