Duniani kote vijana wenye uwezo mkubwa wa kujenga hoja na kufikiri sahihi ndio wamekuwa msaada mkubwa sana kwa mataifa yao.
Marakadhaa vijana wamekuwa mstari wa mbele kupinga aina yeyote ya ukandamizaji na uvunjwaji wa katiba za nchi zao jambo ambalo lisipokemewa linaweza kupelekea uvunjifu wa amani kwa nchi zao.
Hivi karibu kumekuwa na tabia mbaya isiyoweza kuvumilika na mtu yeyote yule mpenda haki na usawa katika taifa lake, miezi michache iliyopita Serikali ya Ccm chini ya Raisi Magufuli imepiga marufuku mikutano ya vyama vya siasa, lakini katazo hilo linaonekana limelenga zaidi vyama vya upinzani na Mabara yake,ile hali Ccm na mabara yao ya vijana,wazee na wanawake wanaendelea kufanya mikutano ya hadhara na vikao vya ndani.
Ni kukosa haya kwa kiongozi kama Shaka A Shaka Kaimu Katibu wa UVCCM taifa,kukana kuwa hajawahi kufanya mikutano ya hadhara, ile hali amefanya hivyo Katavi,Tabora,Bagamoyo na kwingineko .
Hoja ya Shaka kuwa vyama vya upinzani na Mabaraza yake wanashindwa kufanya vikao vya ndani kwa kuwa hawana ofisi ni hoja dhaifu na niyamtu alievimbiwa madaraka, anatakiwa kujua kikao cha ndani sio lazima kifanyike katika ofisi ya chama husika na kama tafsiri yake ya vikao vya ndani inamtuma ni katika ofisi tu , wanaojua maana ya vikao vya ndani wanapata picha pana ya uwezo wa akili yake ilivyo ndogo na nafasi aliyonayo kisiasa.
Katika mazungumzo yake shaka amegusia mikutano ya hadhara kuzuiliwa kwamba anaunga Mkono na akatolea mfano wa nchi kama marekani, hii pia ni dalili nyingine ya uvimbe kwenye ubongo alionao Shaka, maana amesahau kabisa kuwa Katiba ya nchi yetu na sheria ya vyama vya siasa inaruhusu vyama vya siasa kufanya siasa wakati wote bila kuzuiliwa.
Aina hii ya vijana wasiojua misingi ya sheria na utawala bora ni hatari kubwa sana kwa taifa, vijana tunanafasi kubwa sana kulitumikia taifa hivyo ni vyema tukasimama imara kusimamia katiba ili kuandaa nchi itakayoongozwa kwa kufuata Katiba.
Imetolewa na,
*Edward Simbeye*
Katibu Mwenezi *BAVICHA* Taifa.