UVCCM janga la kitaifa

Mizizi

JF-Expert Member
Mar 8, 2008
1,271
390
Nimeshangaa kusikia, Makamo mwenyekiti UVCCM bara Beno Malisa na Yule wa Zanzibar Jamal Ally, kufika Arusha na kutaka kufanya kazi za umoja huo bila uongozi wa huko kufahamu na kupewa taarifa. Hata hivyo, zoezi la viongozi hao kutaka kufungua matawi ya Umoja huo huko Arusha ulikwama baada ya viongozi wa maeneo hayo akiwemo Mwenyekiti wa wilaya ya A. mjini kukataa kutambua shughuli hiyo
Kama kweli hawa ndio viongozi wanaondaliwa kutuongoza hapo baadaye basi Tanzania bado tuna safari ndefu sana.

Huyu kijana Malisa huwa anapenda kufanya vitu anavyofikiria yeye na maslahi ya kundi analolisupport bila kujali maslahi ya vijana anaowaongoza!
Kwenye kipindi hiki cha uongozi wake tumeshuhudia UVCCM ikiwa kwenye mgawanyiko mkubwa sana, kila kijana kwenye umoja huo ni kama anamamlaka yake mwenyewe, kila kijana ni msemaji wa umoja huo, na kila kijana ana mtazamo wake na msimamo wake.

Hakuna tena ile spirit ya Youth League, hakuna tena mshikamano, hakuna tena nidhamu. Vijana wamegawika kwenye makundi ya wasaka madaraka, wakiwemo viongozi wenyewe.

Hii ni UVCCM ya Malisa
 

alex50

JF-Expert Member
Jan 28, 2008
217
114
uvccm is falling from a cliff in slow motion. it has reached a point of no return
 

dhahabuinang'aa

Senior Member
Aug 10, 2011
134
28
Ni zaidi ya msiba wa kitaifa kwani ni zaidi ya mafisadi!
wapo kwa maslah ya nani kwa ufupi wanatumia kodi za walalahoi
kunufaifa matumbo yao tuu
kwani ccm hata kazi za chama hutumia mali za serikali ni lini ccm watajua
kutenganisha kazi za chama na za serikali
hata haya malipo ya dowans tukilainika na kuwalipa zinaenda ccm
wameila nchi imebaki mifupa bila huruma bado wanaikamua hadi damu
chama hichi ni haramu kwa nchi changa kama hii tufike wakati


tuseme ccm noooooooooooooooooooo!
 

Mzee

JF-Expert Member
Feb 2, 2011
13,536
5,642
Ni mfumo umejengwa na ukajengeka. Chanzo si UVCCM chanzo ni CCM kwa kuwazeesha vijana wao kifkra.
 

Sangarara

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
13,100
5,635
Huyu Beno Malisa alijichomeka kwenye familia ya Jakaya kwa malengo binafsi, hakuwahi
kuwa na fikira za kuwa kiongozi, yeye mwenyewe hawezi uongozi, ni bora jakaya
angemfanyia mpango akawa hata kwenye department ya sheria BOT kuliko kuendelea
kushika wadhifa alio nao UVCCM.

sasa UVCCM na Babu CCM wamekuwa kama watoto wanaokimbia huku wameshikana
mikono, wanatumia nguvu nyingi ila hawaendi mbele, mwishoni kabisa wataanguka.

wanaanguka hawa
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom