UVCCM: Gambo ana hila na Kihongosi

Hivi punde

JF-Expert Member
Apr 1, 2017
2,554
8,552
Jumuiya ya Vijana ya Chama cha Mapinduzi (UVCCM) wilayani Arusha imemkosoa mbunge wa jimbo hilo, Mrisho Gambo kumtuhumu hadharani Katibu mkuu wao, Kenani Kihongosi kujihusisha na vitendo vya rushwa.

Juzi Gambo alimtaja Kihongosi mbele ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kujihusisha na vitendo vya rushwa kinyume na maadili ya viongozi wa chama hata Serikali.

Kufuatia tuhuma hizo, Waziri Mkuu Majaliwa aliwasimamisha kazi watendaji sita wa Halmashauri ya Jiji la Arusha akiwamo mkurugenzi mtendaji.

Katika tuhuma hizo, Gambo alisema Kihongosi anashirikiana na baadhi ya viongozi wa halmashauri ya jiji hilo kutumia vibaya fedha za umma.

Hata hivyo, Kihongosi ambaye aliwahi kuwa mkuu wa Wilaya ya Arusha alisema Kamati ya Maadili ya CCM ndiyo yenye uhalali wa kuchunguza tuhuma hizo na kuzitolea ufafanuzi. Alipotafutwa jana, Kihongosi hakupokea simu.

Katika kuonyesha kuchukizwa na hatua ya Gambo, Katibu wa UVCCM wilayani Arusha, Saiopulan Abubakar alisema hatua ya kumtaja Kihongosi, huku akiwaacha baadhi ya watuhumiwa ni kuidhalilisha jumuiya hiyo.
 
Uzalendo hamna kabisa maslahi ya nchi n muhimu Sana mafisadi huwa yana mkono mrefu Sana Arusha wana mbunge anayejielewa hongera mrisho Gambo keep going
 
Back
Top Bottom