UVCCM (Arusha) sasa wekeni CHAMA mbele na si MGOMBEA.......... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

UVCCM (Arusha) sasa wekeni CHAMA mbele na si MGOMBEA..........

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Meitinyiku L. Robinson, Feb 28, 2012.

 1. Meitinyiku L. Robinson

  Meitinyiku L. Robinson JF-Expert Member

  #1
  Feb 28, 2012
  Joined: Aug 29, 2011
  Messages: 412
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Katika kuelekea uchaguzi mdogo Jimboni Arumeru Mashariki vimbwenga vingi vimeshaanza kuonekana na vingi vinasikitisha kutokana na makundi yaliyojitokeaza mengi yakitamani yule wao wanaomtaka ndiye awe ama apitishwe ili kuipeperusha bendera ya Chama hasa CCM, jambo ambalo limepelekea uchaguzi kurudiwa ndani ya CCM.

  Msuguano mkubwa na fukuto kubwa limeonekana kutoka ndani ya Umoja wa Vijana wa CCM Wilayani Arumeru pamoja na Mkoani wakishinikiza yule wao wanaomtaka ndiye anayestahili ila katika hali ya kawaida ndani ya Jimbo, Mkoani na hata Taifa picha halisi inaonesha kuwa mawazo yao hayakubaliki na yule wao wasiomtaka ndiye anayetakiwa kukiwakilisha Chama kukiwa na imani kwamba atakiwakilisha Chama vyema katika kupambana na Vyama vingine vya Upinzani vitakavyosimamisha wagombea.

  Hivyo basi; mi nadhani katika hali ya namna hii na kwa wakati huu ni lazma ufikie wakati Vijana wa CCM waoneshe BUSARA na HEKIMA ya hali ya juu katika hili waoneshe ukomavu wao Kisiasa, waweke kando makundi, wakumbuke Chama ni kimoja, waoneshe mapenzi yao ndani ya Chama, waridhie kwa kauli moja kuwa wanataka ushindi Arumeru, waone na kutambua kuwa hakuna haja tena kuendelea kusema kundi letu litashinda na kundi flani litashindwa, wajue kwa dhati kuwa hata yule wao wasiomtaka nae ni kijana hivyo hakuna haja ya kutenga mkono wa kushoto na wa kulia kwa kuwa mikono yote ni ya mtu mmoja, waone na kutambua mahitaji ya CHAMA pamoja na kilio cha WANACHAMA ndani ya Jimbo lao, watazame mbele na kuamini kuwa wanakwenda kuingia ulingoni hivyo kuna kushinda na kushindwa, wajue wazi kuwa fikra za walio wengi ni juu ya mahusiano yaliyopo kati ya PM Mstaafu pamoja na yule wanaomtaka, wakubali kuwa nguvu na uwezo wa PM Mstaafu unatambulika vyema na si lazma yule wanaomtaka ashinde ndio hilo liendelee kudhihirika, wajue vile vile kuwa hayo wayafanyayo ni kuendelea kuwapa wananchi mwanya kuendelea kulitumia jina la PM Mstaafu kwa namna isiyofaa;

  Baada ya kutambua hayo sasa waamue haya;

  1. Chama kwanza mgombea baadae
  2. Wakubaliane kuwa Kijeshi kurudi nyumba si kushindwa bali ni kujipanga upya
  3. Uwanjani Mgombea vile vile hujinadi na si kunadiwa (Vigezo na Masharti kuzingatiwa)
  4. Kwamba mpambano unaweza kuwa mgumu basi atahitaji mwenye kujua kupambana

  Ningekuwa Kiongozi wa Vijana ningewaita Vijana wenzangu tungeyazungumza haya na kupitisha uamuzi mgumu ili kukisaidia Chama kama kweli tunakipenda na kwa kuwa namweshimu na nampenda PM Mstaafu (kwa kuweka kumbukumbu sawa binafsi namweshimu na nampenda kweli hili silifichi hata kidogo) vile vile ningezungumza naye hata kama yuko Nje ya Nchi ningemweleza ukweli ili kuepuka jina lake kuendelea kutumika visivyo na vile vile ningemwomba asaidie Kampeni katika Jimbo hili ili ushindi uwe mwepesi kwa kuunganisha nguvu za wote.

  Baada ya hapo kwa kauli moja tunapitisha kuweka kando tofauti zetu za kimakundi na kuamua kumpitisha yule tusiyemtaka sisi bali anayetakiwa na Chama chetu na Wananchi walio wengi.......... Viongozi hasa wale wahusika stand and act hapa ndipo busara za viongozi hupimwa muulizeni Suleiman atawaambie'

  I humbly submit!
   
 2. n

  nketi JF-Expert Member

  #2
  Feb 28, 2012
  Joined: Feb 15, 2012
  Messages: 555
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Pole kwa kutumia akili namuda wako mwingi kushauri chama kilichoishiwa! Kikwete tu hashauriki..................vijana wake watashaurika kweli.......subiri uone km ushauri wako wa maana au umeenda hewani tu
   
 3. M

  Molemo JF-Expert Member

  #3
  Feb 28, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  CCM hawawezi kushinda uchaguzi Arumeru katika hali yoyote.Wana makundi makubwa yaliyogawanyika kiasi kwamba watu hawasalimiani.Nadhani kwa hali niliyoshohudia si ajabu mgombea wa CDM akapata ushindi wa zaidi asilimia 80%
   
 4. J

  JACADUOGO2. JF-Expert Member

  #4
  Feb 28, 2012
  Joined: Dec 13, 2010
  Messages: 930
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Kwanza naomba utambue kuwa Edward Lowassa siyo waziri mkuu mstaafu! Vile utambue kuwa CCM kwa ujumla wake kimeoza kila idara na wala siyo UVCCM tu! Vile vile utambue kuwa 90% ya UVCCM wametekwa na Lowassa na wewe mwenyewe ukiwemo na wametekwa tu kwa sababu ya pesa chafu za Lowassa na si vingevyo! Kwaheri kwa sasa.
   
 5. Meitinyiku L. Robinson

  Meitinyiku L. Robinson JF-Expert Member

  #5
  Feb 28, 2012
  Joined: Aug 29, 2011
  Messages: 412
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
   
 6. Meitinyiku L. Robinson

  Meitinyiku L. Robinson JF-Expert Member

  #6
  Feb 28, 2012
  Joined: Aug 29, 2011
  Messages: 412
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Duh! sasa wewe mimi labda nifanye hivi moja niruhusu nikuite lofa kwa kukosa techniques lakini pili nikushukuru kwa kuaga kwa kugundua kuwa uko usikostahili kuwepo na mwisho nikupe pole kwa kujadili hoja kwa Mhemko.
   
 7. Bukanga

  Bukanga JF-Expert Member

  #7
  Feb 28, 2012
  Joined: Dec 13, 2010
  Messages: 2,863
  Likes Received: 714
  Trophy Points: 280
  Rated; ****
   
 8. Meitinyiku L. Robinson

  Meitinyiku L. Robinson JF-Expert Member

  #8
  Feb 28, 2012
  Joined: Aug 29, 2011
  Messages: 412
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Bwana Molemo;

  Matokeo kawaida ni lazma yawe "A" kashinda na "B" kashindwa ama "A" kashindwa na "B" kashinda na wenye mamlaka ya kuamua hivyo ama vinginevyo ni wale wapiga kura hivyo swala la makundi na swala la flani hasalimiani na flani sidhani kama yanaweza kuwa matokeo; hali uliyoshuhudia kama usemavyo iendelee kukupatia faraja
   
 9. TUJITEGEMEE

  TUJITEGEMEE JF-Expert Member

  #9
  Feb 28, 2012
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 10,787
  Likes Received: 2,684
  Trophy Points: 280
 10. DALLAI LAMA

  DALLAI LAMA JF-Expert Member

  #10
  Feb 28, 2012
  Joined: Jan 31, 2012
  Messages: 8,617
  Likes Received: 401
  Trophy Points: 180
  Sintofaham yote iyo inaongozwa na mbumbumbu Millya,kuwadi wa Mamvi aliyeahidiwa ubunge na uwaziri El ak├Čingia ikulu licha ya IQ yake kufanana na vijana wa shule za kata
   
Loading...