Naomba kuulizia, kuunganisha solar panels mbili mfano panels za wat 50, na kuweka panel moja ya wat 100, katika nguvu ya ujazaji wa betri. Je, Kuna utofauti?
Kuna namna mbili ya kuunganisha solar panels, series na parallel. Ukilinganisha kwa njia ya series unakuwa ume double volts na Amps zinabaki vile vile.
Ukiunganisha kwa njia ya parallel, una double Amps na Volts zinabaki vile vile.
Jibu la swali lako ni kubwa; ukiunganisha panel mbili za 50w unapata 100w, uwezo sawa sawa na panel moja ya 100w.
Kiutendaji ukifunga panel moja ya 100w inaweza kukupa matokeo mazuri kuliko mbili za 50.
Kwa sababu zinapounganishwa mbili, moja ikiwa na itirafu itasababisha uzalishaji wa nishati kushuka, ila hii utegemeana na ubora wa vifaa ulivyo vitumia.
Ushauri:
1. Ili kusuka mfumo wa solar power wenye matokeo chanya, unahitaji kumtumia fundi mwenye ujuzi mzuri kwenye hili eneo.
2. Tumia vifaa vyenye ubora, vitakugharimu pesa zaidi ila vitakupa matokeo mazuri na kudumu kwa muda mrefu.
3. Ukimpata fundi mzuri fuata ushauri wake usiwe mbishi kana kwamba wewe ndiye fundi.
4. Kamwe usifunge moja kwa moja nyaya kutoka kwenye panel kwenda kwenye battery bila kupitia kwenye charger controller. Hata kama fundi atakushauri hivyo, kataa maana battery yako itakufa mapema sana.
5. Tumia tu battery za deep circle, isitumie battery za gari, hazitakupa matokeo mazuri.
Karibu kwenye ulimwengu wa Renewable Energy.