Uturuki kuijengea Tanzania Chuo Kikuu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uturuki kuijengea Tanzania Chuo Kikuu

Discussion in 'International Forum' started by Ngongo, Feb 24, 2009.

 1. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #1
  Feb 24, 2009
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280
  RAIS wa Jamuhuri ya Uturuki, Abdulah Gul, amesema nchi yake itajenga chuo kikuu nchini kuendeleza uhusiano kati yake na Tanzania.


  Akizungumza wakati wa kutia saini mkataba wa ushirikiano kati ya Uturuki na Tanzania, Gul alisema pamoja na mambo mengine waliyokubaliana vipaumbele vitakuwa katika elimu, kilimo, biashara pamoja na afiya.


  Mkataba huo ulitiwa saini jana na Waziri wa Kilimo na Chakula Steven Wasira kwa upande wa Tanzania, huku Waziri wa nchi Muastafa Saed Yavizicioglu akitia sahini kwa upande wa Uturuki.


  Utiaji saini huo ulishuhudiwa na rais Gul wa Uturuki pamoja na mwenyeji wake rais Jakaya Kikwete wa Tanzania.


  Rais Gul pia alisema shirika la ndege la uturuki litaanza safari kati ya Istanbul na Tanzania katika kuhakikisha maendeleo ya sekta ya anga.


  Alisema ili kuhimarisha uhusiano huo watafungua ubalozi wao nchini Tanzania katika kipindi cha mwezi mmoja na nusu.


  “Katika kuimarisha ushirikiano tatafungua Ubalozi wetu hapa, na nimeambatana na balozi wenu mtarajiwa, balozi hebu sisimama wakuone, anaitwa Dk. Sander Gurbuz” alisema Gul


  Mpaka sasa Tanzania inatumia ubalozi wa Uturuki uliopo nchini Kenya katika kufanya mambo yanayo zihusu nchi hizi mbili.


  Akitoa shukurani zake kwa rais Glu, rais Kikwete alisema hatua iliyofikiwa itaongeza kasi ya ushrikiano kati ya Tanzania na Uturuki ushirikiano ambao awali ulikuwa unakuwa polepole.


  Alisema ushirikiano huo utasaidia Tanzania kupitisha sauti yake katika nchi tajiri ulimwenguni kwa sababu uturuki ni moja ya nchi zinazo unda umoja wa nchi tajiri duniani (G8).


  “kuna vikao vingi vya nchi tajiri ambavyo hufanyika mara kwa mara, tunategemea Uturuki itakuwa sauti yetu hasa katika kipindi hiki ambapo kuna mtikisiko wa uchumi Duniani, kuziasa nchi nyingine zisipunguze misaada kwa Afrika” alisema Kikwete.


  Pia alisema anamatumaini kuwa Uturuki itasidia katika kulinda usalama katika nchi za kiafrika, akitolea mfano Somali.


  “Uturuki ni miongoni mwa nchi zilizo katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, japo haijapata uanachama wa kudumu, naamini wana nafasi kubwa katika kutusaidia kwenye usalama wa nchi zetu za kiafrika” alisema Kikwete


  Rais huyo wa Uturuki amemwalika rais Kikwete kufanya ziara katika nchi yake.


  Akizungumza mara baada ya kutia saini mkataba huo wa mashirikiano, waziri wa Kilimo na Chakula, Steven Wasira alisema makubaliano hayo yatasaidia sana kuinua sekta ya kilimo na chakula.


  Alisema makubliano hayo yatasaiia kwenye Utafiti, maunzo, pamoja na kuongeza thamani ya mazao ya kilimo.


  “Makubaliano haya yatasaidia sana katika kubadilishana taarifa za vituo vyetu vya utafiti kwa, kufundisha watalamu wetu nchini Uturuki, pamoja na wawekezaji kuja kuwekeza kwenye viwanda vya kuongeza thamani kwenye mazao ya kilimo na mifugo” alisema Wasira


  Ziara ya rais wa Uturuki nchini ilianza jana, ambapo aliambatana na ujumbe wa watu zaidi ya 150 wakiwemo wafanyabiashara.


  Wafanyabiashara wa Uturuki na Tanzania walikutana juzi katika hateli ya kempsiki jijini na kufanya mazungumzo.


  Rais Gul ambaye ambaye aliambatana na mkewe Hayrunnsa Gul, juzi alitembeleya shule ya Feza iliyopo jijini Dar es Salaam ambayo inamilikiwa na Uturuki.


  Gul baada ya kushuhudia utiaji saini wa makubaliano hayo ya ushirikiano alifanya mazungumzo na rais wa Mapinduzi ya Zanzibar Amani Abedi Karume katika hotel ya kempsiki, ambapo waandishi wa habari hawakuruhusiwa kuingia.


  Rais huyo wa Uturuki pamoja na ujumbe wake walimaliza ziara yao ya siku mbili jana, aliondoko katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julias Nyerere majira ya saa 9 kamili alasiri na Ndege aina ya Airbus.


  Alisindikizwa na mwenyeji wake rais Kikwete aliye ambatana na mkewe mama Salma Kikwete, Waziri Mkuu Peter Pinda pamona na badhi ya mawaziri.

  Source;Mwananchi

  Chuo kikuu kijengwe katika ile mikoa isiyokuwa na chuo kikuu.Kuna tabia iliyoshamiri siku hizi kila kitu cha kimaendeleo kinarundikwa Dar es salaam.
   
 2. Giro

  Giro JF-Expert Member

  #2
  Feb 24, 2009
  Joined: Feb 9, 2009
  Messages: 360
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Kwanini? kuna usiri gani? au ndio wanataka tuamini Scramble for Tanzania imeanza,Baada ya Bush ,juzi juzi tu hapa China,mara Meli la Kivita la Kimarekani na makomandoo kibao lilitia nanga katika bandari yetu ya Dsm,hatuja pumua vizuri Uturuki,kweli Tz ni tunda zuri lavutia kwa rangi na harufu yake.
  Hi misada itatufikisha pabaya,we need now to stand with our own feet.Tanzania sio masikini tunatatizo la umasikini wa kufikiri na kujituma.kila siku misaada wao walipata wapi misaada hii mpaka wakaendelea?

  Ukipata muda tafuta hili book and then lisome uwe mazalendo wa nchi yako:
  Confessions of an Economic Hit Man (ISBN 0-452-28708-1) is a book written by John Perkins and published in 2004. It tells the story of his career with consulting firm,

  Briefly Content:
  "Covertly recruited by the United States National Security Agency and on the payroll of an international consulting firm, he traveled the world—to Indonesia, Panama, Ecuador, Colombia, Saudi Arabia, Iran and other strategically important countries...Perkins reveals the hidden mechanics of imperial control behind some of the most dramatic events in recent history, such as the fall of the Shah of Iran, the death of Panamanian president Omar Torrijos, and the U.S. invasions of Panama and Iraq."[1]

  According to his book, Perkins' function was to convince the political and financial leadership of underdeveloped countries to accept enormous development loans from institutions like the World Bank and USAID. Saddled with huge debts they could not hope to pay, these countries were forced to acquiesce to political pressure from the United States on a variety of issues. Perkins argues in his book that developing nations were effectively neutralized politically, had their wealth gaps driven wider and economies crippled in the long run. In this capacity Perkins recounts his meetings with some prominent individuals, including Graham Greene and Omar Torrijos. Perkins describes the role of an EHM as follows:

  Economic hit men (EHMs) are highly paid professionals who cheat countries around the globe out of trillions of dollars. They funnel money from the World Bank, the U.S. Agency for International Development (USAID), and other foreign "aid" organizations into the coffers of huge corporations and the pockets of a few wealthy families who control the planet's natural resources. Their tools included fraudulent financial reports, rigged elections, payoffs, extortion, sex, and murder. They play a game as old as empire, but one that has taken on new and terrifying dimensions during this time of globalization.

  The epilogue to the 2006 edition provides a rebuttal to the current move by the G8 nations to forgive Third World debt. Perkins charges that the proposed conditions for this debt forgiveness require countries to sell their health, education, electric, water and other public services to corporations. Those countries would also have to discontinue subsidies and trade restrictions that support local business, but accept the continued subsidization of certain G8 businesses by the US and other G8 countries, and the erection of trade barriers on imports that threaten G8 industries
   
 3. omarilyas

  omarilyas JF-Expert Member

  #3
  Feb 24, 2009
  Joined: Jan 24, 2007
  Messages: 2,127
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Kama vigogo wa serikali za mitaa jijini Tanga wataacha ukiritimba hili dili la chuo kikuu linaelekea huko.

  omarilyas
   
 4. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #4
  Feb 24, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,867
  Likes Received: 115
  Trophy Points: 160
  Ajabu na Kweli sikuwahi husikia Chuo Kikuu Tanga pale mjini...ila kule Magamba Luth. Church wamefungua tawi la Tumaini

  Tanga kuna nini?
   
 5. omarilyas

  omarilyas JF-Expert Member

  #5
  Feb 24, 2009
  Joined: Jan 24, 2007
  Messages: 2,127
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Hii kali.......

  Katika dunia ya sasa kuna phenomenon inaitwa INTERDEPENDENCY....ama kuhitajiana katika masuala ya maslahi ya kila taifa....

  Uturuki ni taifa linaloendelea ambalo kama tukiwa makini tunaweza kupata soko kubwa la mazao yetu. Uturuki ni taifa ambalo lina nafasi kubwa ya kuwa Taifa kubwa hapo mbeleni na kama mchakato unaoendelea wa mabadiliko katika katika jumuiya za kimataifa yatafanikiwa ni wazi UTURUKI ina nafasi kubwa ya kuwa na kura ya turufu katika Umoja Wa Mataifa. Kamwe hilo halipo ndotoni mwa Tanzania. Hivi sasa hawa jamaa ni wadau muhimu katika kundi la mataifa 20 ambalo linajongea kuchukua nafasi ya Kundi la mataifa 7/8 ama G8 katika uongozi wa mfumo wa uchumi duniani.

  Hili ni taifa pekee lisilo la kizungu ukitoa CHINA lenye nafasi kubwa ya ushawishi katika Jumuiya na nchi za magharibi. Kuwa karibu nao kunatupa nafasi ya wa kutuzungumzia kwa sauti imara katika masuala ya kimataifa haswa maendeleo ya kiuchumi, kisiasa na kiusalama katika nadharia inayoendana na maslahi yetu.

  Hapa Tanzania tayari walishakuwa na ubalozi mdogo tangia mwanzoni mwa mwaka 2000 na wamewekeza katika sekta muhimu za kijamii kama mashule na viwanda vidogovidogo vinavyotoa ajira kwa vijana wenye elimu ya ufundi. Sasa wana mpango wa kuingia katika sekta ya afya ambako wamejijengea sifa kubwa katika nchi zingine zinazoendelea.

  Wakati tunatambua kuwa ni vigumu kuamini wanasiasa wetu haswa katika enzi hizi za UFISADI KUSHIKA HATAMU n ni muhimu pia kuwa open minded katika kuchanganua faida na athari za mipango na hatua mbalimbali zinazochukuliwa na serikali yetu....

  Naamini kuna umuhimu kwa Tanzania kuwa proactive katika kuboresha mahusiano na hawa jamaa (wakati huu ambao Taifa hili linapiga hatua kubwa) kwa kuzingatia nafasi ya mafanikio yetu kiuchumi na kiusalama kwa wakati huu na zaidi wakati ujao.

  Badala ya kuogopa kuanzisha na kuendeleza mahusiano na mataifa mengine ni muhimu kuwa proactive katika enzi hizi za mashindano ya kimaslahi ambayo yanaendelea katika misingi ya dunia mpya ya maendeleo kwa wote....Kujikwaa hapo kabala kusitufanye tujifungie ndani na kuogopa kutembea kujihakikishia maslahi bora.....

  Omarilyas
   
 6. K

  Kwame Nkrumah JF-Expert Member

  #6
  Feb 24, 2009
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 887
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45
  No, mimi nashauri kijengwe Lindi.
   
 7. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #7
  Feb 24, 2009
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Hapana kijengwe Kigoma , mwisho wa reli!
   
 8. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #8
  Feb 24, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,867
  Likes Received: 115
  Trophy Points: 160
  Kitajengwa Bagamoyo home kwa JK kama mradi wa maji wa China Chalinze
   
 9. M

  Mfumwa JF-Expert Member

  #9
  Feb 25, 2009
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 1,456
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Sidhani kuna haja ya kuingia mjadala wa wapi hicho chuo kitajengwa. Manake uwepo wa chuo sehemu sio sababu ya jamii ya waliohapo kuchukuliwa, huwezi pata chuo bila kuwa na vigezo vinavyofaa. Hivyo hata kikijengwa Kanyeye, Uyui, kule Tabora, ama Mitunduruni, Utemini kule Singida hiyo haisaidii jamii za pale kuchukua ajira zote, wengi wataomba kazi toka sehemu mbalimbali za TZ.

  Mjadala muhimu hapa ni mahusiano ya TZ na uturuki, vipi tunaweza kufaidika na Uturuki katika nyanja mbalimbali.
   
 10. Elusive

  Elusive JF-Expert Member

  #10
  Feb 25, 2009
  Joined: Nov 26, 2008
  Messages: 223
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Hatujaelezwa Chuo Kikuu hiki kikishajengwa kama watakiendesha wenyewe kama Feza Schools au watapewa Serikali kukiendesha? Mimi nafikiri kama watakiendesha wenyewe basi wao ndio wataona wapi kinafaa kijengwe kwa maslahi yao na pengine karibu na Jiji la Dar es Salaam karibu na shule zao.
   
 11. U

  Ubungoubungo JF-Expert Member

  #11
  Feb 25, 2009
  Joined: Jul 28, 2008
  Messages: 2,508
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  popote pale kitakapojengwa ni tz. hata wakijenga vyuo mia moja vyote Dar hamna shida. ni watz watakaosoma na kufaidika. kwanza Dar itapikuliwa sio muda mrefu. chuo kikuu cha Dodoma tu chenyewe ni tishio kubwa kwa DSM wale wanaojifanya kubania wanafunzi.
   
 12. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #12
  Feb 25, 2009
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,644
  Likes Received: 1,470
  Trophy Points: 280
  Hivi tunahitaji kujengewa chuo kikuu kingine au kuimarish vilivyopo?
   
 13. Mwana wa Mungu

  Mwana wa Mungu JF-Expert Member

  #13
  Feb 25, 2009
  Joined: Aug 14, 2008
  Messages: 1,007
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  kujengewa vingine na kuimarisha vilivyopo pia. kama kuna opportunity ya kujenga chuo, unataka tuipoteze ili kuimarisha vilivyopo? kenya kuna vyuo vingi tu vya marekani, vimeweka majengo yao pale na wakenya wengi wanaelimika. washington university ipo kenya and it is run by Americans. hivyo usione kama kitu cha ajabu.
   
 14. K

  Kwame Nkrumah JF-Expert Member

  #14
  Feb 25, 2009
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 887
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45
  It does matter wapi chuo kinajengwa. Mara nyingi ujenzi wa chuo kikuu unaendana na miundombinu na huduma kama vile barabara, benki, posta,mahoteli , masoko na maduka kwa ajili ya wanafunzi, walimu na wageni, shule za msingi na sekondari kwa ajili ya watoto wa walimu { au watoto wa wanafunzi], au shule za mazoezi pia. Pia kuna "drop down effects", mfano sehemu za burudani kupata wateja {i.e Mlimani na Silent In enzi zile }, wanafunzi kununua chakula nje kwa akina mama ntilie, ajira hata kama ni za kufagia, ulinzi n.k ni ndogo lakini zitasaidia wenyeji kidogo..
  Ndiyo maana watu wa Lindi, Singida, Mtwara au Kigoma wanaweza kufaidika zaidi kuliko Dar au sehemu zingine zenye ahueni.
  But then again, chuo chenyewe cha kupewa, and "beggars can not choose".
   
Loading...