'Utumwa wa kisasa' unavyojitokeza kwa sura tofauti nchini Tanzania

FikraPevu

JF-Expert Member
Jan 2, 2010
303
236
Tanzania imetajwa kuwa miongoni mwa nchi 100 duniani zenye idadi kubwa ya watu ambao wanatumikishwa kwenye shughuli za ‘utumwa wa kisasa’ ambapo hali hiyo inatafsiriwa ni ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu.

Kulingana na ripoti ya utafiti iliyotolewa na taasisi ya Global Slavery Index (GSI-2017) imeitaja Tanzania kushika nafsi ya 22 kati ya nchi 167 zenye idadi kubwa ya watu wanaotumikishwa kwenye aina mbalimbali za utumwa wa kisasa (Modern Slavery).

Ripoti hiyo inaelezwa kuwa inakadiriwa kuwa hadi kufikia mwaka 2016, Tanzania ilikuwa na watu 341,400 ambao wanatumikishwa kwenye shughuli mbalimbali ambazo zinakiuka haki za msingi za binadamu. Idadi hiyo ni sawa na asilimia 0.638 ya wananchi wote waliopo nchini.

‘Utumwa wa kisasa’ unahusisha vitendo vya kulazimishwa kufanya kazi ngumu, kuwaweka watu rehani (bonded labour), usafirishaji watu, utumwa wa watoto, ndoa za kulazimishwa na ndoa za utotoni. Waathirika wakubwa wa utumwa huo ni wanawake na watoto ambao kutokana na hali zao hawawezi kujizuia na matendo maovu yanayofanywa na baadhi ya watu katika jamii.

Tanzania imewekwa nafasi ya 22 kwasababu ya ongezeko la mimba za utotoni na utumikishwaji wa watoto kwenye kazi ngumu za migodini, mashambani na biashara.

Zaidi, soma hapa => Tanzania yashika nafasi ya 22 kwa ‘Utumwa wa Kisasa’ duniani, mimba za utotoni , kusafirisha watu zaigharimu | FikraPevu
 
Back
Top Bottom