Utumishi wa umma msalabani

mwanaapolo

JF-Expert Member
Mar 14, 2014
256
78
Ndugu watumishi wa umma,

Tunaendelea kupita katika kipindi cha kheri na shari, Heri ya Mwaka Mpya! Kama inavyoonekana kuna wanaopata ubatizo wa maji na wengine ubatizo wa moto. Ni usawa wa kulimia meno. Tujikaze.



Tuko katikati ya vita vya shetani, ibilisi na zimwi. Kila kundi likishangilia ushindi. Hatuna muda sana, mshindi atapatikana. Iwapo shetani atashinda, ibilisi na zimwi hawana budi kusujudu na vile vile iwapo ibilisi atashinda shetani na zimwi shurti nao kufanya vivyo hivyo. Na ilitokea zimwi kutangazwa mshindi basi ndio hivyo. Tujikaze.

Utumishi wa umma ni huduma, ni kuwa mtumwa kwa wananchi. Ni kujitoa kutumika kwa kumenyeka kweli kweli. Wengi wetu tulizembea, tulikiuka dhamana, tuliwakosea wananchi. Ubatizo wa moto tuliowapa wananchi kwa miongo kadhaa sasa ni zamu yetu. Tuwaache nao washangilie maumivu yetu. Tujikaze.

Ndugu zangu, chururu, si ndondondo

Tumepambana vilivyo kutetea maslahi yetu. Tuko imara, tunaamini vita hivi havitaacha majeruhi pekee bali maafa ya wengi. Wale wateule wapo karibu kabisa wakishangilia, hofu ni kuwa wamegawanyika, Kusi na Kaskazi wakituhumiana kuuana ila wao wakipendekeza kuua si kosa. Tujikaze.

Kusi na Kaskazi hizi ni pepo mkabala, zina kawaida ya kung’ang’ana kuchana tanga. Tufani inanguruma na nahodha amekaa vyema kwenye kiti chake. Taarifa zinasema nanga imesahaulika kule tulipoanzia safari. Tujikaze

Wamebariki kamchezo ka kusema ukweli, hivyo sasa ni mwendo wa ukweli kwa ukweli, piga nikupige, sema nikuseme, jibu nikujibu, chapa ni kuchape, fumua ni kufumue, vua nikuvue. Wakitukwaza hawawezi kuomba msamaha maana ndio vichaa tunaohangaika nao. Tujikaze

Nimepita pale hospitali nikawaona wenzetu wakiwa wodini. Uzuri hadi sasa wodi ile inaongozwa na waliomchagua wao. Vichaa shurti waongozwe na kichaa mwenzao. Hii ndio demokrasia. Tujikaze

Ndugu,

Taharuki ni nyingi, ile ngoma ya sukari na saruji ilikwenda kwenye mkole wa umeme kukiwa bado kuna mirindimo ya tetemeko. Manju amekwenda kupoza koo akirudi atakuja na remix. Tujikaze

Bado wanaendelea kulima wamepiga magoti kwenye mazulia na kuwatwisha wanawake ndoo za maji vichwani huku wakiimba wimbo wa wanyonge. Mnyonge msaada wake jembe la mota na kumtua ndoo kichwani ubebe wewe mwenye mabaunsa, usafiri, miguvu na nguo za kubebea. Tujikaze

Turudi kwa yule Mungu orijino tumwangukie kama tulivyofanya mwaka ule. Tuliomba mvua ya ukali na nabii wa kutunyoosha. Tulisahau kuomba kwa kiasi na sasa yamekuja mafuriko ya pilipili na ndimu yenye chumvi kwenye jeraha bichi. Tujikaze.

Kila mmoja ajenge ujasiri, ajiamini, ajitoe, atumikie, aondoe hofu kwani habari kuu ni kuwa zoezi la kutengeneza majeraha na madonda hadharani ni endelevu. Inaosemekana waliokula vinono na kuishi kama malaika watamkoma. Tujikaze.

Ndugu watumishi wa umma,

Mtumishi wenzetu aliyetukuka Comandante Fidel Castro amekwenda. Hatukumsindikiza. Tumesahau upendo na utu wa Fidel kwa taifa letu. Kama unamthamini mnyonge, Fidel ndio kamaradi wako. Tujikaze

Vile tume Zika kama Faru Jo basi, tusubiri kudra na majaaliwa ya pepopunda yatuponye. Sio akili zetu. Tujikaze

yaiya

Imeandikwa na Vicensia Shule, PhD.

Utumishi wa Umma Msalabani | Vicensia Shule
 
Moja ya vitu ambavyo eidha nilisahau au nilikuwa sijui in kuhusu Tanzania kutokwenda kumsindikiza kamanda Fidel Casto !!

Licha ya mahusiano ya nchi hizi tangu enzi ! Jamani hivi in kweli.
 
Utumishi wa umma haujawahi kuwa sifa njema tangu uhuru,kujikaza ndiyo nguzo yetu ,Heri utumishi wa imani msikitini au kanisani,kama siasa hukujaliwa utumishi ni utumwa fadhila kutegemea.Ukishidwa kote huko kilinge ufungue kipato cha mangungu ni mara mia ya daktari wangu.
 
Maneno mengi ya nini..

Chanzo ni POMBE

Tena ile ya kienyeji
 
Back
Top Bottom