Utumishi, Utumishi, Utumishi! Sekretariat ya Ajira Utumishi nimewaita mara tatu

mats_

JF-Expert Member
Apr 9, 2017
398
296
Habari za wakati wakuu,

Mimi nina jambo dogo kwa upande mmoja ila kwa upande mwingine ni kubwa na linaathiri sana mtazamo wangu na wa vijana wengi sana wasaka ajira za serikali kupitia Sekretariat ya utumishi kupitia ajira portal. Wao wanaweza ona ni jambo la kuselect option fields (zile select buttons / option buttons) na kujaza wanachokiona ni cha kawaida lakini kwa sisi tunaosaka hizi ajira ni jambo linalotukata stim sana.

Kuna post kadhaa zilitoka kipindi fulani hapa kati (Ministry of Lands). Yani mtu unakataliwa kuitwa interview kwa petty issues, na huenda hata hazikuepo kwenye tangazo la ajira, na hata kama zilikuepo kuna ambao hua tunaingia ajira portal tukikuta nafasi zinazoendana na taaluma zetu basi tunasoma details pale then tunasuka barua tuna attach tunatuma, huenda zile details zinazowekwa pale zikawa hazijatimiza matakwa ya details zilizowekwa kwenye tangazo la pdf (maybe), sasa unaweza soma details ukaona kabisa hii naweza itwa ila ukaomba na ukakataliwa (Not Shortlisted).

Sasa tufanye hivi, Nyie Sekretariat ya Ajira kupitia Ajira Portal tunawataka mnapoweka post za ajira, kwenye site pale pale kwenye ku view details za hiyo post, basi mu attach na pdf file ya hilo tangazo la ajira husika ili iwe rahisi kusoma vigezo vyote, na kama vigezo havitakuepo vingine tujue kabisa kama hua tunakua eliminated kwa vigezo ambavyo mnaamua tu kuvitunga baada ya watu kuomba ilimradi tu muweze kupunguza watu mapema wasije kwenye interview.

Kiukweli Mnatukata Stim Sana, Mnaua matumaini ya vijana wengi sana, Huku Mtaani sio kama uko mlipo kwenye viyoyozi na per diem mnazokula huku mme relax mnakuna matumbo.

IMG_0392.jpg
 
Mkuu,sasa uliomba ya nini kama uko employed tayari?

Huoni kama ulitaka kuzibia nafasi wenzio wenye uhitaji?
 
Kwa jinsi nlvokuelewa, nadhan ww ndo hufahamu. Ajira portal wanaweka tangazo pamoja na vigezo pale pale pia ukienda kwenye tovuti ya Ajira pia utaona pdf yenye ajira zote zilizotoka kwa kipindi hicho pamoja na vigezo
 
Au yupo kwa contract ....so hawez omba hyo nyingine

Sent from my TECNO CC6 using JamiiForums mobile app

hii kazi hakuna sehemu walisema kama una contract popote uwezi omba..
hivi unafkiri kwanini watu wanataka serikalini, af kitu kingine ukijichanganya tu ukawa umesahau ku change employment details baada ya contract yoyote ujue kuna mahali utaliwa panga..

Na nasisitiza, pdf wala details hazikueka wazi kama hawataki watu wenye contracts ama nini, hii imekua mbinu ya kuwaondoa watu bila kuweka bayana restriction kwa mara ya kwanza
 
Mkuu,sasa uliomba ya nini kama uko employed tayari?

Huoni kama ulitaka kuzibia nafasi wenzio wenye uhitaji?

Mkuu, kamwe kwenye hii life usikae kizembe.

Uhitaji upo kwa kila mtu, regardless of circumstances.. ao wenye kazi kila siku wana fight wapate kazi zenye ujira mzuri zaidi ili watimize ndoto
 
hii kazi hakuna sehemu walisema kama una contract popote uwezi omba..
hivi unafkiri kwanini watu wanataka serikalini, af kitu kingine ukijichanganya tu ukawa umesahau ku change employment details baada ya contract yoyote ujue kuna mahali utaliwa panga..

Na nasisitiza, pdf wala details hazikueka wazi kama hawataki watu wenye contracts ama nini, hii imekua mbinu ya kuwaondoa watu bila kuweka bayana restriction kwa mara ya kwanza
Umeajiriwa serikalini au private?
 
Back
Top Bottom