Utumishi Moshi Manispaa kwafukuta

Utumishi Moshi Manispaa kwafukuta

Baada ya kuweka habari hii (Rushwa yatumika kupandisha watumishi madaraja Manispaa ya Moshi) sasa ofisi ya utumishi Manispaa ya Moshi kunafukuta. Tangu habari hii isomwe na maafisa wa ofisi ya utumishi Grace na Mary sasa wanahaha. Ili kujiokoa:

1) Ndani ya wiki moja wamewashusha madaraja watumishi wote waliopandishwa daraja hivi karibuni (evidence ya nakala za barua za kushushwa madaraja zipo ila naomba leo nisiziweke kuwahifadhi). Maswali yanayozuka ni kwamba kama kweli hawakuwapandisha kwa Rushwa kwa nini wawashushe baada ya makala hii?

2) Sasa Grace na Mary wamekuwa wakiwatishia walimu wanaohisi kuwa ndio wameandika habari hizi. Tayari wamewatishia waalimu kadhaa. Wamesahau kuwa habari za madudu ya Mary kwa mfano tumeanza kuyaandika toka zamani. Mfano harakati za Mary tuliziandika miaka mingi nyuma sana. Mfano Marrystela afisa utumishi moshi(manispaa) na ombwe la uongozi.

3) Siku mojawapo ndani ya wiki moja iliyopita nimefika ofisi ya utumishi na Grace akawa anawatuhumu walimu kadhaa huku akijiapiza kuwakomoa. Audio ya maneno yake ipo na kwa sasa namstahi ila akiendelea nitaiweka.

Ushauri wangu kwa Grace na Marry ni kwamba tulieni dozi iwaingie. Tupo hapa kumuunga mkono mheshimiwa Rais wetu John Pombe Magufuli anayehimiza uchapa kazi bila kuonea wananchi ama watumishi. Ni vema wajirekebishe na watende haki. Vinginevyo tutaendelea kuanika vitendo vyao vya rushwa na upendeleo.

Ndimi mtumishi wenu huru.

Jamani tuache uzushi tufanye kazi.. hizo stress zako nenda hospitali.. kuna miongozo na vigezo vya mtu kupanda cheo...
Kama sisi walimu unatakiwa kuwa na oprass kama 4 na anaenza leo kazi ndan ya miaka 5atapanda..
Ungesema tujiunge kusisitiza miongozo kandanizi kwa watumishi ilekebishwe sawa na sio wew uwe unazurula tu huna opras alafu unataka kupata daraja..
Wajibu na HAKI Ndg... Pia acha kutumia jina la Mzalendo wetu mh. Rais kwan yeye anataka wachapa kazi sio walalamikaji kwenye mitandao kama wew
 
Nikushukuru kwa mchango wako walau umechangia kwa staha sana. Nikusaidie tu kwamba nimeshajaza OPRAS kama sita na nipo kazini kwa zaidi ya miaka 7 labda huyo unayemfikiria ni mwingine. Anyway, walau malalamiko yetu yanafanyiwa kazi japo ni kwa kuwashusha waliopandishwa badala ya kuwapandisha ambao hawajapandishwa. Kikulacho ki nguoni mwako!
 
Back
Top Bottom