Utumiaji wa simu kwa muda mrefu

Flamegood

Senior Member
Oct 27, 2018
129
293
Habari za muda huu wapenzi wa JF,

Kama kichwa kinavyosema hapo juu, lengo la kiuzi hiki ni kutafuta jibu sahihi ili kama kuna madhara mengine niweze kubadili mwelekeo wangu.

Mimi nimejikuta nakuwa addicted kwenye matumizi ya cm kwa muda mrefu kwa siku hadi masaa 10 nikiwa naperuzi vitu mbalimbali katika internet, Huwa sifatilii udaku, kuchart wala kutizama video za ngono bali natumia internet kujifunza mambo mbalimbali haswa nisiyoyafahamu kwa mfano; Muda mwingi napenda kusoma Nyuzi mbalimbali za JF, kusoma quotes za watu juu ya hoja zinazohusiana na Habari na Hoja Mchanganyiko na ninashuhudia zikinijenga kiakili, pia napenda kufatilia kuwapo kwa ukweli juu ya imani tofautitofauti ikiwemo Freemasons na Illuminati.

Lengo la Uzi huu ni kutaka kufahamu kama kuna athari zozote za kiafya zinazoweza kunipata kwa kutumia cm kwa muda mrefu? Ni zipi ili niweze kupunguza matumizi haya.
 
Tafuta kazi ya kufanya, masaa 10 upo internet inaonesha huna kazi. Uraibu wa chochote ni baada ya kukosa shughuli muhimu ya kutumia muda na nguvu yako(physically or mentally). Tunaingia jf kujifunza, kuburudika na kuhabarishwa wakati wa mapumziko au baada ya suruba za kazi. Usikubali kuwa mtumwa wa simu, utaharibu macho, mgongo nk.
 
Seen ila kazi yangu pia ni ya online marketing

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwanga wa simu ni mbaya sana, utauwa nerves za uoni matokeo yatakuja kwenye macho.
Mwanga wa simu una kipimo chake. Ukiuzidisha ndio tatizo. Halafu watu wanunue simu original.
Screenshot_20201001-191128_Chrome.jpg
 
Hamna madhara kwenye mwanga wa simu, labda shingo, utafiti unasema mwanga wa simu au TV hauna madhara kwenye macho. Natumia simu mwaka wa 10 na laptop si chini ya masaa10 na nipo fresh.
Habari za muda huu wapenzi wa JF,

Kama kichwa kinavyosema hapo juu, lengo la kiuzi hiki ni kutafuta jibu sahihi ili kama kuna madhara mengine niweze kubadili mwelekeo wangu.

Mimi nimejikuta nakuwa addicted kwenye matumizi ya cm kwa muda mrefu kwa siku hadi masaa 10 nikiwa naperuzi vitu mbalimbali katika internet, Huwa sifatilii udaku, kuchart wala kutizama video za ngono bali natumia internet kujifunza mambo mbalimbali haswa nisiyoyafahamu kwa mfano; Muda mwingi napenda kusoma Nyuzi mbalimbali za JF, kusoma quotes za watu juu ya hoja zinazohusiana na Habari na Hoja Mchanganyiko na ninashuhudia zikinijenga kiakili, pia napenda kufatilia kuwapo kwa ukweli juu ya imani tofautitofauti ikiwemo Freemasons na Illuminati.

Lengo la Uzi huu ni kutaka kufahamu kama kuna athari zozote za kiafya zinazoweza kunipata kwa kutumia cm kwa muda mrefu? Ni zipi ili niweze kupunguza matumizi haya.
 
Kwani we unaonaje? Inakuletea madhara yoyote? Ratiba zako za kufanya mambo mengine ya msingi haivurugiki? Kama unaona inakuletea madhara download app inaitwa YourHour...hii itakutia adabu.. addiction yote itaisha..na kama haujaamua kuondokana na addiction yako lazima uta uninstall hiyo app..
 
Back
Top Bottom