Utozaji na Ongezeko la ada kwenye Private Schools

Patriote

JF-Expert Member
Jul 13, 2011
1,718
1,047
Kwa Mara kadhaa serikali yetu imekuwa ikibeep kudeal na suala la udhibiti wa ada za shule za sekondari. Lakini kwa bahati mbaya umaliziaji wa suala hili umekuwa ngumu sana. Sababu moja wapo ni huenda kwa vile ni wakubwa ndio wanaomiliki hizi shule.


Kama serikali imeweza kudhibiti bei ya Mafuta, Bei ya Nauli za mabasi ya mikoani n.k. Inashindikana nini kuweka shule katika madaraja na kuwapa bei/viwango elekezi vya kutoza ada?

Unakuta shule inatoa poor education, haina walimu, haina huduma nyingi tu za msingi. Ila ukija kwenye ada unakuta ndio kinara cha kutoa ada kubwa. Sasa unajiuliza, wanatumia criteria gani kupanga ada? Au unajiamulia tu kwa vile unamiliki shule basi unajipandishia tu??

Niiombe sana serikali, kuangalia hili suala. Ipange hizi shule katika madaraja km ilivyofanya kwenye Mabasi na kama ilivyo kwenye madaraja ya Hotel. Na serikali iseme, shule daraja LA kwanza ni lazma itoe huduma 1, 2, 3. Na iseme ratio ya Wanafunz kwa walimu iwe labda 1:30 or any how. Then iseme shule itayotoa huduma hizo itoze ada maximum isizidi TZS kadhaa.

Kwa utaratibu huu tunaoendanao elimu yetu itaendelea kudidimia mana kila kukicha gharama za elimu zinapanda bila uhalisia wowote. Kwa kweli kwenye elimu kuna false inflation serikali tunaomba muingilie kati au mna maoni gani wadau?
 
Back
Top Bottom