Utoroshwari wa Twiga na Meno ya Tembo

Utoroshwari wa Twiga na Meno ya Tembo

Patriote

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2011
Posts
1,718
Reaction score
1,047
Nimekuwa nikifwatilia mara kwa mara pale ninapopata taarifa kuwa maliasili zetu zimekamatwa huko ng'ambo, lakin nikagindua kuwa. Sisi kama watanzania hatupaswi tu kusikitikia uvushwaji wa rasilimali hizi kinyemela, bali tunapaswa kusikitikia udhaifu wa vyombo vyetu vya ulinzi na usalama pamoja na wakusanyaji wetu wa kodi. Hivi kama Twiga wanaweza kuvushwa hadi kufika ng'ambo bila polisi kuwaona na wala TRA kukusanya kodi sasa hapo tunauhakika gani kuwa polisi wanazuia uhalifu au wanatulinda na TRA wanakusanya kodi maeneo mengine pia???

Imagine meno yamepitishwa bandarini bila Polisi kuyaona na TRA kutoza kodi hilo Container sasa TRA wanafanyaje kazi???Mbona napata mashaka hapa na Utendaji wa Polisi na TRA achilia mbal watendaji wa exit points zetu, Mfano mwingine unaonifanya niwe na wasiwasi na TRA ni pale taarifa za polisi na wamiliki wa mgodi zilipotofautiana baada ya majambazi kutaka kukwapua Gold iliyokuwa kwenye hatua za mwisho kuvushwa kwenda ng'ambo. Hivi katika sakata lile, TRA ilitoza kodi kubase wap??au ndo haikutoza kabisa???

Swali kuu ninalojiuliza, uzembe huu wa TRA kutokukusanya kodi kikamilifu katika deals hizi kubwa ni wa bahati mbaya au na wao wanajua kinachoendelea??? Uzembe huu wa Polisi wa kutokulinda mali zetu ni bahati mbaya au wao ndo wanazisindikiza had zivuke mipaka??? Mbona Polisi wanakomaaga sana kwenye kudhibiti maandamano ya CDM???inakuwaje wanashindwa kuelekeza nguvu hizoo kwenye kulinda mali zetu kazi ambayo ni ya msingi kwao???

Nina mashaka sana na the way TRA wanavyokusanya kodi mana wangekuwa makin kwenye ukusanyaji wa kodi nadhan wangekuwa wanafungua macontainer kuangalia kilichokuwepo ndani ya container ili wafanye Tax evaluation na ndipo watoze kodi stahiki. Na kama wangekuwa wanafanya hivyo naimani container za meno ya tembo zingekamatiwa hapa hapa Tanzania. Lakin kwa kuwa hawafanyi hivyo ndo maana mizigo haramu inapita mbele yao bila kuiona. Nadhan TRA huwa wanauliza tu (Humo kwenye container umebeba nini???kilo ngapi?je tukutoze kodi Tsh gani???). Kama wangekuwa wanakomaa kama wanavyokumaa kwenye uingizaji wa magari naimani wangetusaidia sana kwenye kudhibiti wizi wa rasilimali zetu.TRA na Polisi Badilikeni mnatucost!!!


Mimi nadhan next time tukisikia meno ya Tanzania yamekamatwa nje ya nchi wa kwanza kudeal nao wawe ni Polisi wa exit point mzigo ulipopita??? Watendaji wa TRA mzigo ulipopita na ikibid wakuu wa vyombo hivyo na wafunguliwe kesi za uzembe na uhujumu uchumi. maana mzigo utakuwa ulipita mbele yao either kwa wao kutojua(uzembe) au kwa wao wakijua (uhujumu uchumi).
 
Back
Top Bottom