Utoaji wa risiti za efd kariakoo

Utoaji wa risiti za efd kariakoo

kiss9

Member
Joined
Nov 24, 2013
Posts
55
Reaction score
34
Maduka kadhaa naona yameitikia wito wa kutoa risit za efd,lakini mbona ukinunua vitu vya gharama ya juu wao hukuomba wakukatie risiti yenye gharama ndogo! Mfano unanua meza ya kioo ya Tsh 200,000 ila muuazaji anakuomba akupe risiti ya Tsh 100,000!
Tunamfaidisha nani?
 
mwambie na yeye akurudishie elfu 50
[emoji121]
HII NDIO DAWA YAO,
TENA HUA WANAKUITA FARAGHA KIDIGO
WASHENZI HAWA!!!

MIMI HUWA NAWAKAZIA HASA IKIWA WALIKATAA KUTOA DISCOUNT WAKATI WA MAUZIANO.

[emoji377] [emoji124] [emoji469] [emoji469] [emoji469] [emoji469] [emoji469] [emoji469] [emoji469] [emoji469] [emoji469]
 
Maduka kadhaa naona yameitikia wito wa kutoa risit za efd,lakini mbona ukinunua vitu vya gharama ya juu wao hukuomba wakukatie risiti yenye gharama ndogo! Mfano unanua meza ya kioo ya Tsh 200,000 ila muuazaji anakuomba akupe risiti ya Tsh 100,000!
Tunamfaidisha nani?
Hamna anaefaidika sema hiyo ni njia mojawapo ya wao kujipunguzia kodi mwisho wa siku kutokana na mauzo yao..ina maana ww hama huitumii hiyo receipt kwa namna yyte unaweza ukamsaidia ila kama utaenda kuitumia kwenye shughuli zako unamwambia tu ina matumizi..maana kama kodi ya laki ni 18,000..unaweza muomba akuounguzie io ela kwenye amount ya hela uliyonunua io bidhaa.then akuandikie io receipt ya 100,000 iliyobaki..mjini timing.
 
Hahaha mimi nikinunua kitu kwa bei iliyooelekezwa nataka risiti ya thamani ya pesa niliyonunulia. Risiti ndiyo itaonyesha thamani ya kitu hicho. Mfano hiyo meza Tsh 200,000/= wewe unalipa laki mbili anakupa risiti ya Tsh 100,000/=. Ukiibiwa hiyo meza ukitoa taarifa polisi na ushahidi wa umiliki ni hiyo risiti itaonyesha thamani ya meza yako ni laki moja. Na ikiwa una bima(insurance) wao watakulipa laki moja ndiyo ushahidi wa thamani ya manunuzi iliyoonekana.
Wewe ndio utapunjika kwa kutaka kumsaidia mwenye duka.
Risiti inamaana kubwa zaidi ya kuwa karatasi tu. Kwanza ni ushahidi wa umiliki halali wa mali(ownership)husika, pili ni uthibitisho wa thamani halisi ya mali uliyomiliki kutoka kwa muuzaji.
Usikubali ukanunua mali ya Tsh 200,000/= halafu risiti ionyeshe umelipia Tsh 100,000/=. Huo ni ujinga sio ujanja. Onyesha wewe mnunuzi pia unajali thamani ya pesa yako. Acha kudanganywa na wafanyabiashara. Jiulize ikiwa umenunua mali yenye thamani ya Tsh 10,000/= ukamuomba mwenye duka akupe risiti inayoonyesha umelipia Tsh 100,000/= ili ukarudishiwe ofisini, yeye atakubali?! Ikiwa hatokubali nawewe kataaa katakata. Umfaidishe yeye kwa madhumuni yapi?! Bora pesa yako ukamlipie mgonjwa hospitali aliyeshindwa kulipia gharama za matibabu,labda utapata thawabu toka kwa mungu. Kuliko kupoteza thamani ya pesa yako kwa kuwasaidia wafanya biashara. Dai risiti ionyeshe thamani ya pesa uliyolipia, kataa ujinga.
 
Mimi nakubakiana nao , kwani najua ugumu na mazingira ya biashara hapa tz,
Ukilipa Kodi na ushuru nje ya kodikwa asilimia zote lazima ufunge duka au biashara
 
Hizo risiti zikikaa muda zinafutika maandishi yote,
Nini kifanyike ili kutunza maandishi hayo?
 
Wakuu kuna hii risiti unapewa imeandikwa
Not registered hivi hii ina maana yeyote Kwa mlipa kodi?
 
Napata wazo hapo,kuna wakati unakuta mali uliyonunua haijakidhi viwango flana inakulazimu kurudisha dukani na utaratibu wao ni wewe kuonyesha risit,Je ukikuta yule aliyekuuzia hayupo dukani ? Atakubali kukuhudumia?
 
Tena kuna wakati unapodai risit wanaanza kujizungusha then anakuita pembeni!
Na kuna maduka mengine yana bei mbili ya bidhaa kwa wanaotaka risit na wasiotaka
 
Ni asilimia 13 cheza hapo mwambie akupe asilimia saba hatokata kamwe
 
Lipa kodi kwa maendeleo ya Taifa lako.
Kulipa kodi sio issue. Ila ujiongeze tu kidogo kuwa ukiona hivo ujue kuna jambo haliko sawa. Na kwa mtu yeyote ambaye hajawahi Fanya biashara hawezi elewa. Ni kama mtu ambaye hajawahi kujenga nyumba , ukimuelezea jinsi Nyumba inavyotafuna hela hawezi elewa.

Sheria ya ukadiriaji kodi niliwahi ambiwa na afisa wa TRA kuwa ilitungwa na mkoloni, baadae hii miaka ya hivi karibuni waliifanyia marekebisho lakini bado kwa kiwango kikubwa sheria ilibaki kikoloni.

Wewe angalia Bidhaa moja inaweza kulipiwa kodi zaidi hata ya Mara 5.
 
Back
Top Bottom