Utoaji mimba

Ricky Blair

JF-Expert Member
Mar 13, 2023
391
873
Kiinitete hakina haki. Haki hazitolewi na ambacho hakijaja bado bali kwa yule ambaye ameshafika. Mtoto hawezi kupata haki yoyote mpaka azaliwe. Yule anayeishi (Mwanamke) anamtangulia yule ambaye bado hajazaliwa kwenye haki kwani huyo mwanamke akiamua kujiua wote mmekosa.

Utoaji mimba ni haki ya maadili ambayo inabidi iachwe kwenye mikono ya mbeba mimba tu ambaye ni Mwanamke au msichana mdogo, kimaadili hakuna wazo lingine lolote lisipokuwa lake ambalo la kutiliwa maanani la kusikilizwa. Nani ana haki ya kumuambia au kumuamrisha afanye nini na mwili wake?

Wanawake wanawaambia wanaume wakiwa wanapiga punyeto? Ambayo na hao ambao hawawezi kutofautisha seli na mtoto hai kabisa hawawashtaki, kwani shahawa nyingi zinamwagika ambazo zingezalisha mamilioni au matrilioni tangia mtoto wa kiume aanze kupiga punyeto. Kwaiyo huu mjadala ni wa wanawake tu na sio wengine.

Usijali upumbavu utakausikia kwamba kiinitete kina haki ya maisha. Kipande cha sehemu hai za seli hazina haki and hakuna maisha kama binadamu hai anayepumua.

Ni kweli unaweza kutetea maisha ya mtoto aliyeanza kukua kwenye trimester ya pili au kuanzia zaidi ya miezi mitatu na kuendelea, na kwenye nchi zote ambazo utoaji mimba kihalali unaruhusiwa mimba zote hutolewa kwenye miezi mitatu ya kwanza na zaidi ya hapo ni kama kuna tatizo la huyo mtoto kwamba hatozaliwa na akawa salama au hatari kwa mama kiakili na kimaisha, lakini bado kuna mijitu sana sana wanaume ambao hawajui uzoefu wa mwili wa mwanamke iwe kwenye hedhi, mimba au kuzaa bado watabisha.

Nafikiri wangeweza kupata hedhi japo mara moja au kujaribu kuzaa haki ya kutoa mimba ingetetewa na mabomu na bunduki. Kwaiyo hapa tunazungumzia haki ya kutoa mimba ya miezi mitatu ya mwanzo. Kufananisha yule ambaye hajaja (Kiinitete) na yule ambaye anaishi tayari (Mwanamke) ni ukatili, kuazimia sadaka ya huyo mwanamke ambaye hataki kuendelea na iyo mimba pia ni ukatili.

Wasikilize vizuri kwa hao wanaopinga utoaji mimba hata kwa miezi mitatu ya mwanzo hata kama mwanamke amebakwa kwa kumpa fursa kiinitete au ambaye haishi bado wanateketeza haki zote za yule ambaye bado anaishi ambaye ni mwanamke na mwenza wake kama ni vijana ambao maskini na wanatafuta bado maisha.

Kulea mtoto ni shughuli nzito sana na ya kudumu na sio ya kuichukulia poa tu kama unanunua biskuti ivyo sio suala la kuchukuliwa bila idhini au mapenzi yako. Kuzaa sio wajibu, binadamu sio wanyama kama kuku broila wa kuzalishwa tu mpaka unakufa.

Kwa watu ambao wana akili timamu na wasio wakatili kubaki na mimba wasioitaka ni kimbembe na kukataza utoaji wa mimba iyo ni kutetea sadaka sio kwa manufaa ya mtu yoyote bali ni sadaka ya taabu kwa jili ya taabu, kwa ajili ya kuzuia furaha na kujitosheleza kama binadamu anavyotakiwa.

Kama kuna yoyote amechanganywa na hiyo mada kwamba seli za kiinitete ni seli za binadamu anayeishi, basi kumbuka kwamba seli zote za mwili wako ziwe za ngozi, nywele, tonsi/kifuko au appendix/kiambatanisho chako kilichopasuka au kujichua kwa kupiga punyeto pia na yote hayo ni mauaji kama tukifuatilia sheria au itikadi za hao wapinga utoaji mimba miezi mitatu ya mwanzo.

Tujikumbushe muda wote kwamba ambacho hakijaja sio sawa na ambacho kipo tayari na maisha ya binadamu yanaanza baada ya kuzaliwa.

Hawa watu wanaojidai kwamba uyo mtoto anakuwa salama akishazaliwa tu baada ya kumzuia uyo mwanamke kutotoa mimba, je kama ni mwanamke katili je mtoto mchanga ana uwezo wa kuishi mwenyewe bila kumtegemea mtu sana sana mama yake na pia inachukua juhudi yoyote kumuua kama umeridhia na kusingizia tu kitu chochote?

Swali la kutoa mimba linahusu vitu vingi sana zaidi ya kuitoa iyo mimba. Ni swali la maisha yote ya hao wazazi. Kama nilivyosema kabla, uzazi ni majukumu mazito sana na inahusisha sio pesa tu bali muda na busara za watu wanaotarajiwa kuwa wazazi.

Ni jukumu lisilowezekana kabisa kwa vijana wadogo ambao wamejaa tamaa ya maisha na maendeleo lakini bado wanahangaika au ndo wameanza maisha kwa mishahara yetu ya kubangaiza na nusu yote inaishia kwenye kodi, bado chakula na usafiri, au kwa vijana ambao masikini tu na wakisiliza jamii yao ya kifukara na iliyojaa dini wataambiwa zaeni tu mjaze dunia kama Mungu alivyosema wakristo kwa waislamu.

Ambacho hawaambiwi ni kwamba, Bwana Yesu au Mtume Muhammad hatoshusha pensheni kila mwezi kutoka mbinguni ili waishi vizuri ivyo watakazana kuzaa bila uzazi wa mpango au kufanya vasectomy kwa wanaume kisha umaskini unaongezeka na matokeo yake omba omba, watoto ambao wanabakwa au kuuzwa au kunyanyasika tu duniani hapa yote kuzuia kukiindoa kiinitete ambacho kitakuja kuwa mtu baadaye sana.

Kwa hiyo kuwalazimisha vijana hao wadogo uzazi utawafanya watolee sadaka maisha yao mazuri ambayo wangeweza kuyajenga na kuwalaani kwenye maisha yasiyo na matuamini zaidi ya kuwa mtumwa na mahitaji ya uyo mtoto iwe malezi, afya na baadaye shule na kwa uchumi wetu wa ovyo inawezekana hadi akifikisha miaka thelathini bado anaomba msaada kwa wazazi.

Suala la mwanamke ambaye ametengwa iwena mume wake, bwana wake au amebakwa na kupata mimba (hata akiwa amebakwa na ndugu wa damu kama Baba/Mjomba/Kaka ambayo kuna shida nyingi kuzaa watoto ambao wamepatikana kwa ndugu wa damu, hili pia wapingaji mimba watakataa isitolewe) ni kimbembe zaidi.

Sitaki kuwaza akili ya mtu ambaye anatamani ampitishe binadamu mwenzake kwenye kasheshe kama hii. Sitaki kuwaza chuki iliyowajaa ndani yao inaowafanya wazunguke na kupinga wanawake wasitoe mimba mapema.

Chuki ndo iliyowajaa na kama huamini zaa alafu wafuateuwaombe msaada ya uyo waliyokuwa wanadai wanamtetea kisha utashangaa wanasema hayawahusu ila yaliwahusu iko kiinitete kikiwa ndani ya mwili wako.

Hivyo basi chuki zao kama watu wengi wa dini ipo dhidi ya binadamu mwenye akili timamu na ambaye hapelekeshwi tu na imani kama zombi, dhidi ya akili, dhidi ya thamani, tamaa ya maendeleo, mafanikio katika maisha, mapenzi, dhidi ya thamani yoyote inayomletea furaha binadamu katika maisha. Kwenye uongo na unafki mwingi kwenye jamii hawa watu wanajiita wapenda Maisha eti.

Kwa haki gani mtu yoyote anayoweza kusema ana nguvu ya kuharibu maisha ya wenzie na kuwaamuria machaguo yao wenyewe katika maisha yao?

Hii pia kama suala la mapenzi ya jinsia moja hakuna mwanamke anayelazimishwa kutoa mimba tu ili mradi ambayo najua wapo wanawake kadhaa wanaolazimishwa na wanaume ambao hawataki kuwa na watoto au wapo kwenye ndoa tayari na hawataki watoto wengine na wanaume hawa hawa hawataki kuvaa kondomu au kufanya vasectomy kama ana watoto wa kutosha na kumgeuza mwanamke kama kiwanda cha kufanya naye ngono na kutoa mimba tu asizotaka, hawa kama madalali wa ngono wanaouza wanawake hawana haki ya kumlazimisha mwanamke kutoa mimba.

Kwa hiyo ieleweke mwanamke hata kama una watoto kumi unataka mwingine au umebakwa unataka kuendelea na mimba yako sawa na kuna hadi wengine maisha yao yapo hatarini lakini wanachagua mtoto wao azaliwe potelea mbali yeye akifa; uyu pia ni sawa mwache achague.

Tuache kuingiza Dini kila sehemu na kwa nchi hii ambayo Ukristo na Uislam umetawala, najua ni shida sana ila pia tukumbuke Ukristo ndio umepinga sana kutoa mimba toka mwanzo ilipotungwa siku ya kwanza iyo mimba na ndio maana nchi nyingi za Kikatoliki wabishi sana.

Ila kwenye Uislamu wapo huria kidogo kwenye hili swala, na wao wanaamini mpaka siku 120 ndio roho inaingia kwa hiyo hadi miezi minne unaruhusiwa kutoa mimba ila kwa sababu za msingi kama kubakwa, uzazi wa mpango, afya ya mama ikiwa kwenye hatari na vinginevyo.

Kwaiyo tunaona kwenye Dini Uislamu ina afadhali kuliko Ukristo, ndIo maana unakuta nchi ambayo ni liberi sana kama Brazil ambayo inaruhusu hadi ndoa za jinsia moja lakini utoaji mimba ni ngumu sana kuliko Saudi Arabia, ambayo nchi yenye sera kali sana za kiislamu ambayo mashoga wanauliwa kwa sheria lakini utoaji wa mimba ni rahisi.

Ila iwe dini imesema hivi au la bado nchi yetu ni sekula na haina dini hivyo binadamu ndio awe wa kwanza kumfikiria na sio matakwa ya dini au madhehebu yao na Mungu au miungu yao.

Falsafa ya maana ambayo inamtambua binadamu kama mwenye akili timamu na busara haiwezi kumruhusu mtu yoyote kuita Kiinitete kuwa ni mtu badala ya seli chache za binadamu.
 
Mimba sio Mtoto
Mimba haina Haki.
Hata hospitalini ikitokea upiganiaji wa Haki ya kuishi baina ya Mama na mimba, daktari watamuokoa Mama.

Ingawaje kimaadili sio vizuri Kupata mimba kama huna Mpango WA kuzaa
 
Yes
Mimba sio Mtoto
Mimba haina Haki.
Hata hospitalini ikitokea upiganiaji wa Haki ya kuishi baina ya Mama na mimba, daktari watamuokoa Mama.

Ingawaje kimaadili sio vizuri Kupata mimba kama huna Mpango WA kuzaa
lakini we have to take into account unique experiences za wanawake including kubakwa, au wanaume kujifanya kukataa kutumia kinga among other things
 
Yes
Mimba sio Mtoto
Mimba haina Haki.
Hata hospitalini ikitokea upiganiaji wa Haki ya kuishi baina ya Mama na mimba, daktari watamuokoa Mama.

Ingawaje kimaadili sio vizuri Kupata mimba kama huna Mpango WA kuzaa
lakini we have to take into account unique experiences za wanawake including kubakwa, au wanaume kujifanya kukataa kutumia kinga i
 
Utoaji mimba sio kitu kizuri mtu anaweza kupoteza maisha na pia sio kitu cha kupigania kipitishwe maana wazazi wetu wangetutoa tusingekuwepo hapa.Nina kisa cha kweli nakuelezea kwa ufupi.Kulikuwa na marafiki wawili mmoja alipata mimba ya mtoto wa kike akazaa na mwingine alipata mimba akafanya ultrasound akakuta wa kiume hakupenda.Akaitoa akabeba tena mimba akafanya ultrasound akakuta wakike akafurahi.Baada ya kujifungua mtoto yule wa kike ni mlemavu haongei hatembei anapaswa kulishwa,kuogeshwa,kuvishwa mama yake anajuta sana kwa uamuzi ule
 
That's why it has to be legal and safe sio unsafe and illegal na pia natetea utoaji mimba during the first trimester and the earlier the better pia while knowing all potential side effects Km nilivyoelezea. Na unavyosema mpiganie ipitishwe abortion is already illegal among many things na bado people do it
Utoaji mimba sio kitu kizuri mtu anaweza kupoteza maisha na pia sio kitu cha kupigania kipitishwe maana wazazi wetu wangetutoa tusingekuwepo hapa.Nina kisa cha kweli nakuelezea kwa ufupi.Kulikuwa na marafiki wawili mmoja alipata mimba ya mtoto wa kike akazaa na mwingine alipata mimba akafanya ultrasound akakuta wa kiume hakupenda.Akaitoa akabeba tena mimba akafanya ultrasound akakuta wakike akafurahi.Baada ya kujifungua mtoto yule wa kike ni mlemavu haongei hatembei anapaswa kulishwa,kuogeshwa,kuvishwa mama yake anajuta sana kwa uamuzi ule
 
Mungu atuponye na kuturehemu, huku ni kuhamasisha mauji kwa kutoa Mimba
 
Mpumbavu utamjua tu yni nyie mnoshabikia huu ujinga ni sawa na wenye kuuwa tu hmna tofauti yyte ile na muuaji

Ww mimba yko ingetolewa leo hii ungeandika huu upumbavu?
 
Nimependa hoja zako, nimejifunza kufikiri upyaa kuhusu slogan ya shirika letu la kijamii...
Naunga mkono Hoja, ila kama mwanamke unahisi uhitaji kuzaa basi Kuwa mwangalifu usishike mimba, kama umebakwa fasta wai hospital kachekiwe
 
Back
Top Bottom