Boran Jakutay
Senior Member
- Apr 8, 2023
- 110
- 255
Kila siku zinavyozidi kwenda, baa zinazidi kuota maeneo ya Sinza na nyingi zipo kando kidogo mwa barabara.
Hivi karibuni kuna kiota kipya kimejengwa hapa Barabara ya Sinza Mori, ni mita chache kutoka Small Planet (zamani La Charlz).
Kiota hicho kipya kinaitwa Icons Lounge, kipo pale zamani kulikuwa na baa ya Uwoya.
Kwa ujumla baa nyingi za aina yake zinatukera sisi watembea kwa miguu tunaoitumia Barabara ya Sinza Mori.
Ukiangalia kutoka hapo Icons Lounge, unaenda mbele kuna Small Planet, kisha B-Max, halafu kule mbele ndio Kitambaa Cheupe.
Ukipita barabara hiyo hasa wikiendi kuanzia saa 12 jioni, utakuta gari zimepaki sehemu ya watembea kwa miguu.
Hapo watembea kwa miguu tunalazimika kupita barabarani kabisa yanapopita magari.
Yani usipokuwa makini, utashangaa shwaaa, umegongwa na gari au bodaboda.
Neno kwa wamiliki wa hizi baa, wekeni parking ya kutosha ili magari yasipaki sehemu ambayo watembea kwa miguu wanaitumia.