UTIs (Urinary Tract Infections) - Tahadhari kwa wanawake

mwengeso

JF-Expert Member
Nov 27, 2014
9,227
6,666
Kuongezeka kwa ugonjwa wa UTI umeleta hisia tofauti katika jamii kiasi wengine kukwepa kutumia vyoo.

Kama wewe ni mwanamke, uwezekano wa kupatwa maambukizi ya njia ya mkojo, au UTI iko juu sana; baadhi ya watafiti wamegundua kwamba uwezekano wa kupata ambukizo maishani mwako iko pia juu kama mara 1 hadi 2 - na wanawake wengi huwa na maambukizi ya kurudia, wakati mwingine kwa miaka ya mwisho.

Sababu kuu ya UTIs kwa Wanawake ni jinsi wanavyojitawaza, hasa nyakati hizi kwa kuwa matumizi ya maji imekuwa ndiyo njia kuu ya kujitawaza. Wengi hujitawaza kutoka nyuma kwenda mbele na hivyo kuchafua sehemu za haja ndogo kwa maji ya kinyesi. Mwanamke unapaswa kujisafisha kwa mbele kurudi nyuma, kwa kuwa njia ya mkojo iko karibu na mlango wa haja kubwa.

Bakteria kutoka utumbo mkubwa, kama vile E. coli, hupata nafasi kubwa kutoroka haja kubwa na kuvamia njia ya mkojo. Kutoka huko, wanaweza kusafiri hadi kibofu cha mkojo, na kama maambukizi hayajatibiwa mapema, huendelea kuambukiza figo.

TAHADHARI CHUKUA HATUA
 
Miili ya wanawake ni kama mabomu,hatari sana.ila wanavyoringa sasa.mjilinde na uti
 
Jitihada za makusudi zinahitajika kufanywa na serikali kuweza kugundua hasa nini kinasababisha ongezeko la ugonjwa huu,kama ni swala la kutawaza kutoka nyuma kwenda mbele mabibi zetu huko nyuma walikuwa wanafanyaje na walikuwa hawapati,ninahisi hata vyakula tunavyokula vinahusika kwa namna moja au nyingine.
 
Good post.

Ila siyo kweli kuwa incidence ya UTI imeongezeka. Hapana. Kilichoongezeka ni udanganyifu wa hospitali, hasa za binafsi. Udanganyifu huu ni wa makusudi ili kuongeza kipato kwa kuwalazimisha "wagonjwa" kununua dawa. Udanganyifu mwingine unatokana na ignorance ya laboratory technicians. Kuna uhaba mkubwa wa trained technicians. Pia private hospitals hupendelea kuajiri poorly trained techs ili wawalipe kiduchu.

Nimependa comment ya mmoja hapo juu aliyesema kama sababu ni kutawaza kwa nini mabibi zetu hawakuwa na UTI zaidi ya wadada na wamama zetu? Ni kweli kutawaza kwa kuanzia mbele kwenda nyuma kunapunguza uwezekano wa kupata UTI kwa wanawake.

Kuchangia toilet seats hakuchangii kupata UTI wala fungus (Candida albicans), ni imani potofu.

Mara nyingi sana UTI na fungus vinasababishwa na wadudu wanaoishi kwenye uke wakiwa normal flora. Wakipata fursa ya kuingia kwenye urethra wanapanda hadi kwenye kibofu na kuleta UTI.

Samahanini.
 
Kuanzia Leo nimeanza practice ya kukojoa huku nimeasimama
Kusimama sio issue cha muhimu hapo ni je utaweza kulenga sehemu husika,maana ni bora uende pembeni kuliko kama utaingia ndani ya viatu!
 
Usipende kutumia kila maji unayokuta toilet,haswa public toilets mf za stendi nk
 
Kuanzia Leo nimeanza practice ya kukojoa huku nimeasimama
Jitahidi kuwa mwangalifu unapojitawaza ni kwa kurudi nyuma, hasa kama unatumia maji. Vyoo haviambuzi UTI kama vinakuwa safi muda wote. Dhana yako ya kukojoa kwa kusimama si jawabu la kutokuambukizwa UTI
 
Jitahidi kuwa mwangalifu unapojitawaza ni kwa kurudi nyuma, hasa kama unatumia maji. Vyoo haviambuzi UTI kama vinakuwa safi muda wote. Dhana yako ya kukojoa kwa kusimama si jawabu la kutokuambukizwa UTI
Najitahidi mkuu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom