Utii wa amri za kijeshi! Hii ni sawa?

MAHANJU

JF-Expert Member
Aug 26, 2014
5,244
7,970
W'salaam a'laykum wakuu!

Ninataka kujua hivi jeshi lolote lile linaweza kutii amri yeyote hata kama inakiuka utaratibu wa misingi ya kikatiba? Je, kama ni hivyo inamaana hakuna nafasi kwa ofisa wa kijeshi ya kumshauri mkuu wake kwamba amri anayomuagiza ni nje ya taratibu na maelekezo ya kisheria wakakaa na kushauriana kabla ya kuitekeleza?


Nijuavyo mimi katika shule zangu ambazo nimepitia mimi ni kwamba afisa yeyote wa kijeshi anayo nafasi pia kushauriana na mkuu wake endapo ataona jambo analomwagiza linaweza kua nje ya utaratibu wa kisheria kabla ya kufikia maamuzi ya utekelezaji. Kimsingi jeshi lolote duniani hutekeleza maagizo ambayo yapo kikatiba na yanaweza kua kinyume endapo ikibidi au ikilazimu kulingana na hali halisi ya mazingira ya tukio.


Nizungumzie hasa jeshi la polisi ambalo kimsingi kazi yake ni kulinda usalama wa raia na mali zao. Nina imani kabisa nchini tunao maafisa wa polisi ambao ni wabobezi wazuri katika shule za sheria, sitaki kuamini kwamba hata hawa maafisa wa polisi wabobezi na wasomi wa sheria mbali mbali wanaweza kutii maagizo ili mradi maagizo tu hata kama ni kinyume na katiba au sheria.


Afisa wa polisi msomi anayeifahamu vizuri taaluma ya sheria kwanza kabla hajafikia maamuzi ya kutekeleza maelekezo ya mkubwa wake hupokea maelekezo hayo kwa unyeyekevu mkubwa na kisha kuyachuja vizuri, kama kuna ushauri anaweza kuutoa kwa mkuu wake endapo ataona inafaa. Anayo haki kiutaratibu kumshauri mkubwa wake kama ataona jambo lenyewe ni kinyume cha sheria na linaweza kuleta sintofahamu ndani ya jamii.


Nimejaribu kulizungumzia jeshi hili ambalo ndio liko katika jamii muda wote kuhakikisha usalama wao unalindwa. Ni jeshi ambalo limekua likituhumiwa sana na raia kutii na kuzitumia amri za baadhi ya viongozi wa kisiasa nje na maelekezo ya katiba ya nchi na viapo vyoa, wengi husingizia kwamba kazi ya polisi ni kutii amri za wa wakubwa zao na si vinginevyo! huenda ni kwa makusudi au kutokulielewa jambo hili kwamba kama jambo liko nje ya utaratibu wa kisheria polisi anao wajibu wa kumshauri mkuu wake kwa kujadiliana kabla ya utekelezaji.


Nijuavyo mimi ni kwamba kiongozi au msomi yeyote anapokua masomoni hufundishwa busara,hekima na utii ili atakapohitimu shule yake aweze kuiongiza jamii kwa weledi mkubwa, mahali popote busara,utii na hekima vinapotamalaki hua kunakuwepo matokeo maziri na hii ndio maana ya mtu kuitwa msomi. Kwahiyo kama kuna askari ambaye ni msomi kufikia kiwango cha shahada ya Uzamili na kazi yake inakua ni kutii amri ya mkuu wake tu hata kama iko nje ya katiba na sheria basi usomi wake hautumii vema na hatakua na msaada wowote katika taifa.



Binafsi hua napenda kumpongeza sana askari msomi IGP mustafuu mzee wangu Saidi Mwema ambaye niliwahi kukaa nae karibu sana kama ndugu, ni askari ambaye alikua mwerevu sana aliyekua akipokea amri za wakubwa zake kisha kuzichuja kwanza kwa kushauriana na wakuu wake hao kabla ya kuchukua uamuzi, hii ilikua ni tabia yake hata wakati alipokua askari wa kawaida! Aliitumia taaluma yake vizuri kuamua kwa kutumia busara na hekima kufanya maamuzi na ndio maana alimaliza majukumu yake akiwa ameliacha jeshi katika sura mpya kabisa tofauti na nyakati za nyuma.


IGP Mwema alitumua muda mwingi kukaa na viongozi wa kisiasa kufanya mashauriano nao akitanguliza busara zaidi alipoona kuna viashiria vya sintofahamu. Walikaa pamoja na kupena maelekezo ili tu kuhakikisha raia wako salama naali zao.
 
Back
Top Bottom