Uti wa mgongo wa tanzania ni nini? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uti wa mgongo wa tanzania ni nini?

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Zing, Mar 8, 2011.

 1. Zing

  Zing JF-Expert Member

  #1
  Mar 8, 2011
  Joined: Jun 24, 2009
  Messages: 1,780
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  Napenda tuulizane swali hili

  Maana nadhani hata sisi kwa ssis wenyewe, wanasiasa wetu, rais wetu na mawaziri wake . hatuna commo na understanding juu ya ni nini hasa ni uti wa mngongowa taifa letu.

  Tukiweka siasa pembeni Uti wa mgongo wa taifa la tanzania ni nini.?
  Je ni

  • kilimo
  • Madini
  • Utalii
  • Viwanda
  • etc
  Nawasilisha kwa mjadala
   
 2. m

  masssaiboi JF-Expert Member

  #2
  Mar 8, 2011
  Joined: Feb 10, 2009
  Messages: 637
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 33
  etc!!!!!!!!!
   
 3. Edward Teller

  Edward Teller JF-Expert Member

  #3
  Mar 8, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 3,818
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  ni kilimo-ila hakuna mtu mwenye mpango nacho-serikali imeleta blah blah tu kwenye kilimo bila postive outcomes zozote-
   
 4. Halfcaste

  Halfcaste JF-Expert Member

  #4
  Mar 8, 2011
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 973
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 45
  ccm!!!
   
 5. Kamkuki

  Kamkuki JF-Expert Member

  #5
  Mar 8, 2011
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 1,067
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 145
  Ni Utaliiiii. maana Mmhh hata pato la Taifa inaongoza au ndo wizi haujashamili nin? Maana hata celewi!!?
   
 6. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #6
  Mar 9, 2011
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  Unauliza uti wa mgongo? acha mzaha ni kiungo gani cha mwili cha nchi yetu ambacho nchi tunacho. Hatuna macho, hatuoni wananchi wanavyoteseka na tunavyoibiwa. Hatuna masikio kusikia wananchi wanasema nini. Hatuna ubongo kufikiria tulifanya nini jana, tufanye nini leo na kesho tufanye nini. Pua zetu hazinusi kujua nani ni adui na nani ni rafiki wa kweli. Midomo yetu haina sauti ya kugombeza watu wanaoiba na kudhulumu. Hatuna mikono wa kuwashika na kuwadhibiti watu wanaotudhulumu. Hatuna miguu ya kusogea hatua moja mbele, miaka 50 ya uhuru hatuna cha kusherekea zaidi ya kutaka "kutunga katiba mpya".

  Aibu kubwa sana.

  Uti wa mgongo wa nini ndugu yangu???????
   
 7. N

  Nenetwa Member

  #7
  Mar 9, 2011
  Joined: Jan 16, 2011
  Messages: 14
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Nakushukuru kwa fikra nzuri Zing!
  1.Kilimo ndicho tumekuwa tukiambiwa ni uti wa mgongo wa Taifa hili tangu enzi! japo bado njaa inazidi kutishia amani! Wakati mwingine tunaagiza vyakula toka nje ya nchi kufidia upungufu! na mfumuko wa bei ya vyakula unatesa wananchi wengi! NACHANGANYIKIWA KAMA KWELI HUU NDIO UTI WA MGONGO WA TAIFA HILI.
  2.Madini yetu yamekuwa yakichakachuliwa kwa mikataba mibovu yenye maslahi duni kwa wazawa wazalendo. Gawiwo la faida halikidhi hata upungufu wa Bajeti na bado tunaenda omba misaada kwa hao hao wanaochukua madini yetu!!!!!!!! NACHANGANYIKIWA KAMA KWELI HUU NDIO UTI WA MGONGO WA TAIFA HILI.
  3.Utalii haujatangazwa vya kutosha kuwavutia watalii wa ndani na nje katika vivutio vyetu, Na Utalii huu umejikita ktk Mbuga za Wanyama tu na kusahau vivutio vingine kama makumbusho. Japo wanajitahidi kutangaza lakini bado NACHANGANYIKIWA KAMA KWELI HUU NDIO UTI WA MGONGO WA TAIFA HILI.
  4.Viwanda bado ni vichache sana na vimejikita zaidi katika kuzalisha bidhaa za mlaji (Consumer goods) mfano biskuit, soda, majani ya chai nk, na kusahau sana Kuzalisha bidhaa za Mzalishaji (Producer goods) mfano Mashine za kusaga, injini mbalimbali nk. Hii inawafanya wajasiliamali wazalishaji kuagiza mitambo toka nje kwa gharama kubwa na kusababisha Unfavourable balance of Payment/ Trade. Yaani Tunalipa zaidi kwa Ku-import kuliko tunachopata ktk ku-export, bado NACHANGANYIKIWA KAMA KWELI HUU NDIO UTI WA MGONGO WA TAIFA HILI.

  INATUBIDI KUFIKIRIA UPYA AU KUWEKA MSISITIZO NA BAYANA JUU YA NINI UTI WA MGONGO WA TAIFA HILI
   
 8. Zing

  Zing JF-Expert Member

  #8
  Mar 9, 2011
  Joined: Jun 24, 2009
  Messages: 1,780
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  Mkuu kwa elimu ndogo ya biolojia niliyonayo ukiondoa ubongo viungo vyote ulivyotaja haviwezi kufanya kazi kam huo uti wa mgongo umepinda.

  Nimeleta hii mada kutaka kujua kama ufahamu wetuwote ni sawa?
  Maana kisiasa tunaimba kilimo ni uti wa mgongo. Kwenye siasa tunasema tanzania ina vivutio vya kiipkee africa. Kwa hiyo inbidi tulinganishe nyimbo za siasa na maamuzi wanayofanya wanasiasa kama vinaendana

  Nani
  ataathirikana na ni kwa kiasi gani tutahtrika kama

  • Nchi nzima Tusipokuwa na umeme wiki mbili mfululizo
  • Wakulima wote wa pamba kahawa, mahindi waiamu kuchoma mazao yao yote
  • wawekezaji wakubwa na wadogo wa madini wakisitisha uzalishaji
  • Nchi za nje zikazuia raia zao kuja tanzania kwa utalii.
  Nchi kama UK tunaambiwan Financial driven japo wana viwada roho yao ipo kwenye finance economy Nchi kama Germany na , Japan ni Industrial japo zina finance institutions lakini roho yoiko kwente manufacturing.

  Sasa kama mtanzania unaulizwa waht is the core sector tujibu nini?
   
 9. Zing

  Zing JF-Expert Member

  #9
  Mar 9, 2011
  Joined: Jun 24, 2009
  Messages: 1,780
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  Mkuu wewe na kama umeingia kwenye ubongo wangu.
  ukweli ni kwamba Tunachoaminishwa au tunachoamini ni tofauti na vitu tunavyowekea msisitizo kwa utekkelezaji.

  • Ndioo maana hata utalii Tanzania inapokea watalii waliotoka South africa na kenya . wengi sio watalii wanaokuja moja kwa moja Tz. kwa nini ? Sababu serikali yetu na sisi wananchi tunakalia kwenye ngonjera za kusem serengti ni mbuga kubwa sijui ngorongoro bila kufanya mambo ya maaana

  • Ndio maana iadadi ya watalii na mapato ya zoo ya UK inaweza kuzidi idadi ya watalii na mapatoya serengeti. Tunawagawia wanyama wetu tunapoteza mapatao. hatuna haki na wale wanyyama. Kwa nini wasingekuwa wanawakodisha . Kila simba aliyepelekwa nje kwenye zoo agweza kuinga dola hata 50 kwa siku
  Hapa naongea mambo mengi lakini kama ulivyosema bila kujua na kuweka msisitizo na priority sahihi mhhhh. Tanzania itapata maendeleo ya kisiasa tu kama ilivyo sasa . amabyo ni ya wacahache na si maendelo ya uchumi, kilimo, utalii jamii etc
   
 10. L

  LAT JF-Expert Member

  #10
  Mar 9, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  mkuu zing umefikiria kitu ambacho haswa kinatakiwa kizungumziwe katika jukwaa hili .... tunapozungumzia uti wa mgongo wa nchi ni lazima tutazame katika perspective ya taifa ....yaani wananchi .... je ni kitu gani wananchi wengi wanakitegemea katika kuweza kuendeleza maisha yao especially kukidhi mahitaji muhimu kama vile chakula, malazi na mavazi ..... ukiangalia asilimia kubwa ya watu katika nchi yetu wanaishi vijijini ... hivyo basi kilimo ndicho wanachotegemea kujiingizia kipato chao pamaja na kupata hitaji la chakula kwa wakati ulele ule ..... atakayelima mahindi atauza kidogo na fedha zile kununua sukari, nguo kulipia matibabu na kugharamia ada za watoto za shule .... hii ni kama ilivyokuwa zamani barter trade ..... hizi sector nyingine zipo tu kwa ajili ya kukidhi kuendesha serikali kuu na sector nyingi sasa zimegeuzwa miradi ya ufisadi.....
   
 11. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #11
  Mar 9, 2011
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,936
  Likes Received: 2,086
  Trophy Points: 280
  Uti wa mgongo ni kilimo ambao ulikwisha kuwa na magonjwa ya mgongo - ufisadi!
   
 12. Zing

  Zing JF-Expert Member

  #12
  Mar 9, 2011
  Joined: Jun 24, 2009
  Messages: 1,780
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  Kweli kilimo ni uti wa mgongo ulipinda. Kuna jamaa aliyewai kunimbia watanzania tunalishwa na wazee. yaani ukiangalia

  • age ya silimia kubwa ya hao tunawaita wakulima
  • elimu na utaaalamu wa kilimo unaotumiwa na wakulima wengi
  • Zana zinaztumiwa kwenye kilimo
  Bado haingii akilini kuwa kilimo ni uti wa mgongo kivitendo. Ni maproffssoer wangapi wa SUA wana spend japo miezi miwili kwenye miradi au tumradi tudogo twa kilimo vijijini? Shame kwa maproffesor wote wa vyuo vikuu walokubali kuleweshwa na serikali kwa kupewa vinono na hivyo hawtoki mjini.

  This is my conlsuion

  Hapa Tanzania Kilimo ni uti wa mgongo kisiasa na kinadharia but kivitendo Siasa ndio hasa uti wa mngongo wa taifa letu
   
Loading...