Uthibitisho wa Jinsi Meya wa Ilemela Henry Matata anavyohujumu CHADEMA Mwanza....

Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,534
13,225
Ifuatayo ni ripoti maalum iliyoandikwa na gazeti la Raia Mwema kufuatia vitendo vya kuhujumu chama cha CHADEMA Inayofanywa Meya wa Ilemela Henry Matata ambaye yuko madarakani kwa Amri ya mahakama kufuatia kufukuzwa uanachama na CHADEMA.Meya huyo asiye na chama amekuwa akikihujumu CHADEMA waziwazi na pia amekuwa akimuandama kwa kila hali Kiongozi mkuu wa upinzani nchini Dr Wilbroad Slaa hasa baada ya kugundua kiongozi huyo ana nguvu kubwa hapa Mwanza...Endelea kufuatilia....


CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) mkoani Mwanza kimeonywa kuhusu mwenendo wake wa kumtumia Meya wa Halmashauri ya Ilemela, Henry Matata, kama turufu yao kisiasa dhidi ya wapinzani wao kwa kuwa hatua hiyo haikisaidii chama hicho na badala yake inazidi kukijengea chuki kwa wananchi.
Matata ambaye ametwaa umeya baada ya kuvurugana na chama chake (CHADEMA) na kufukuzwa uanachama na kisha kupinga mahakamani uamuzi huo wa kufukuzwa, amekuwa akitajwa kuwa karibu zaidi na CCM ama hadharani au kwa siri katika mipango ya chama hicho katika kile kinachodaiwa kuwa ni njia ya kuwakomoa CHADEMA.
Baadhi ya wanachama wa CCM na wachunguzi wa masuala ya kisiasa mkoani hapa wanaona mwenendo huo wa chama tawala unaweza kukigharimu katika uchaguzi wa serikali za mitaa mwakani na hata Uchaguzi Mkuu ujao, kwa kuwa wananchi wengi hawaungi mkono jinsi chaguzi za meya wa Jiji na Halmshauri mpya ya Ilemela zilivyofanyika.
Mmoja wa viongozi wa zamani wa chama hicho ambaye sasa ni mstaafu anayeishi Kata ya Kitangiri, ameeleza kusikitishwa kwake na jinsi CCM inavyojihusisha kwa karibu na meya huyo, akihusisha na tukio la Ijumaa wiki iliyopita ambapo katika kikao cha viongozi wa CCM Kata ya Kitangiri, alialikwa pamoja na wageni waalikwa wengine ili kupanga mikakati ya uhai wa chama katika kata hiyo lakini akashangaa meya huyo ambaye hatokani na chama chake akiwa mmoja wa wazungumzaji wakuu katika kikao hicho cha chama.
“Hiki kilikuwa kikao cha chama, lakini anaalikwa Meya wa chama kingine, hata kama wana migogoro yao huko, huyu siyo wa kumleta kuzungumza na sisi mambo aliyozungumza, kwa jinsi hali ya haya mambo ya umeya hapa mjini yalivyo CCM inajitengenezea matatizo tu, ukija uchaguzi itahusishwa na kila kitu alichokifanya huyu bwana na hatutaweza kujinasua katika hilo,” alieleza mwanaCCM huyo ambaye aliomba asitajwe gazetini.
Hata hivyo, uchunguzi wa Raia Mwema kuhusu kikao hicho unaonyesha kuwa viongozi wa kata hiyo walikuwa na baraka za chama kutoka viongozi wa ngazi ya wilaya na mkoa, na hivyo kuhudhuria kwa meya huyo katika kikao hicho ilikuwa ni sehemu ya mikakati ya muda mrefu ya kutafuta namna chama hicho kinavyoweza kujitokeza hadharani kuzungumza na wananchi.
Chanzo chetu cha uhakika kutoka ndani ya kikao hicho kilieleza kuwa Mwenyekiti wa CCM, Kata ya Kitangiri John Tegete aliwaomba wajumbe wampokee mgeni huyo kwa sababu ana maelekezo kutoka ‘juu’ kuhusu kufanikisha mipango ya kushirikiana na meya huyo kwa manufaa ya chama chao.
Chanzo chetu kimeeleza kuwa katika kikao hicho kilichofanyika Uwanja wa CCM Kirumba, meya huyo alifika na kupewa nafasi ya kuwaelezea wajumbe jinsi alivyohujumiwa na CHADEMA na jinsi Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Wilbroad Slaa, alivyokuwa hataki yeye awe meya tangu mwanzo na kuwaahidi wajumbe hao uhakika wa ushirkiano wake katika kila jambo.
Meya huyo ambaye pia ni Diwani wa Kitangiri, aliwaeleza wajumbe hao kwamba CCM ijipange vizuri ili yeye awasaidie kurejesha hadhi ya chama hicho jijini Mwanza ambayo imetetereka kwa kuhakikisha kuwa atawasaidia kurejesha kata zote tatu za madiwani aliowafukuza wa Kirumba, Nyamanoro na Ilemela.
“Alitueleza kuwa kama tukishirikiana naye vizuri atahakikisha kuwa wale madiwani wa kata tatu aliowafukuza atahakikisha zinarejea CCM, na akawaondoa wasiwasi wajumbe kuwa uamuzi wake haupingwi kokote, hata rufaa za madiwani hao wanahangaika tu kwa sababu alishawasiliana na waziri mwenye dhamana na serikali za mitaa na kinachosubiriwa ni taarifa kupelekwa tume ya uchaguzi ili nafasi hizo zitangazwe kuwa wazi na CCM lazima tushinde, ndivyo alivyosema,” kidai chanzo chetu cha habari kilichohudhuria kikao hicho.
Taarifa zaidi zinaeleza kuwa meya huyo ameahidi kuwafukuza madiwani wote a CHADEMA waliobakia kwa kuwa hata wao wanaendelea kukaidi kuhudhuria vikao, na kwa mujibu wa meya huyo wamebakiza vikao viwili wakiendelea kuingia na kumkataa na kususia vikao atawafukuza ili abaki na watu wanaoweza kufanya kazi za wananchi.
“Wiki ijayo (wiki hii) tutakuwa na ratiba ya vikao vingi kama wakiendelea na tabia yao hii na hata wao nitawafukuzia mbali, watakaoniheshimu ndiyo nitakaofanya nao kazi bila kujali wamepitia tundu gani hata kama ni Mahakama,” anadaiwa kusema meya huyo.
Ili kuonyesha mshikamano huo, mwenyekiti wa kata hiyo aliwataka wajumbe wote kwenda kuwahamasisha wanaCCM na wananchi wote katika maeneo yao ili wahudhurie mkutano wa kwanza wa hadhara wa meya huyo, tangu achaguliwe kuwa meya uliofanyika katika viwanja vya minazi mitatu Kata ya Kitangiri, huku wanaCCM wakisisitizwa kuvaa sare za chama chao katika mkutano huo.
“Katika kikao hicho pia viongozi wa matawi na mashina wa CCM walitakiwa kueleza kama wana shida ya usafiri ili utaratibu wa kuwasafirisha watu wao uwekwe, wengine walikuwa wanatoka maeneo ya karibu na mkutano kwa hiyo hawakuhitaji usafiri isipokuwa watu wa Mihama ndiyo walioandaliwa usafiri wa kuja mkutanoni na wa maeneo mengine ya mbali nje ya kata hiyo,” kilifafanua chanzo chetu.
Hotuba ya Meya huyo hata hivyo ilibidi isitishwe kwa muda baada magari ya waombolezaji waliokuwa wakienda kuzika katika makaburi ya Kitangiri yaliyo karibu na eneo la mkutano, kupita huku vijana waliokuwa ndani ya magari hayo wakiimba na kupiga kelele zilizowatambulisha kuwa ni mashabiki wa CHADEMA.
“Unaona aibu ya pale kwenye mkutano, hiyo inabebwa na CCM na ndiyo maana mimi tangu siku amekuja kutueleza kushiriki mkutano na sare zetu niliona hiyo hatari ya kuingizwa kwenye matatizo yasiyo ya kwetu, kila anachokifanya sasa hivi watu watajua kina mkono wa CCM, yeye hana cha kupoteza lakini chama, nadhani kwenye hili wamekosea,” alisema mzee huyo mstaafu na kukitaka chama kuepukana na kutangatanga kunakojionyesha sasa.
Akielezea kwa nini meya asiyekuwa wa chama chao alialikwa kwenye kikao cha chama, Mwenyekiti wa CCM Kitangiri John Tegete alisema ya kuwa Meya huyo ni kiongozi wa serikali na alikuwa anapita kwenye vyama vyote kuhamasisha shughuli za maendeleo na wao kama wapenda maendeleo walimwalika ili wamsikilize.
“Yule ni kiongozi wa serikali, sisi kama chama tunapenda maendeleo kwa kushirikiana wote bila kujali itikadi alipoomba kuja, tulimruhusu ili wajumbe wetu wamsikilize juu ya mipango yake ya maendeleo kwa kata yetu, ndiyo maana hata kwenye mkutano tulikuwapo sisi (CCM), TLP na vyama vingine” alisema.
Akizungumzia ahadi ya kuhakikishiwa kwamba viti vya udiwani wa kata tatu kurejea CCM, alisema wao wamejadili masuala ya kata yao na hayo mengine hayaelewi.
“Sasa hilo sielewi, sisi tulizungumza mipango ya kata yetu mambo ya kata zingine hayo kwa kweli siyaelewi” alisema.
Akizungumzia ushiriki wake wa kikao cha CCM na ahadi ya kuwarejeshea viti vitatu vya diwani kama alivyowaahidi katika kikao hicho, Matata alisema msimamo wake na hoja zake ni zile alizoeleza kwenye mkutano huo na ndiyo alizoeleza kwa wajumbe wale.
“Niliyoeleza kwenye mkutano ndiyo hayo, lakini suala la kumsaidia mtu mimi ninaweza kumsaidia yeyote awe CUF au CCM, ili mradi anachapa kazi ya kusaidia wananchi, mimi ni kiongozi wa wote kwa sababu hata mimi nimechaguliwa na wananchi wote wakiwamo wana CCM.”
Katika mkutano huo pamoja na mambo mengine alieleza mipango ya halmashauri yake kuwa ni kujenga barabara ambazo nyingi sasa zimebomolewa kwa mvua zilizonyesha Desemba na mwanzo wa Januari na kuwahakikishia wananchi kuwa zitajengwa muda si mrefu.
Katibu wa CCM, Joyce Masunga alipoulizwa kuhusu chama chake mkoani kujihusisha na meya huyo, alikanusha kufahamu kama kuna maelekezo hayo kutoka ngazi yoyote ya chama.
“Naomba nikwambie kitu, tangu tarehe 10 (Januari) niko Zanzibar kwa sherehe za Mapinduzi, hayo maagizo sikutoa mimi wala ofisi yangu mtafuteni aliyewapa,” alisema katibu huyo alipozungumza na Raia Mwema kwa simu.
 
Demokrasia hapa kwetu bado saana, waongoza dola wanafanya hivyo kama Miungu watu na hii ndiyo inayopelekea kulipiza visasi jambo ambalo sio zuri hata kidogo. Utawala wa sheria ni pamoja na kufuata sheria badala ya kutumia ubabe, hii ni mbaya sana tujifunze kwenye chaguzi za marekani na nchi nyingine duniani
 
Demokrasia hapa kwetu bado saana, waongoza dola wanafanya hivyo kama Miungu watu na hii ndiyo inayopelekea kulipiza visasi jambo ambalo sio zuri hata kidogo. Utawala wa sheria ni pamoja na kufuata sheria badala ya kutumia ubabe, hii ni mbaya sana tujifunze kwenye chaguzi za marekani na nchi nyingine duniani

Mkuu kwamagombe katiba mpya inabidi ieleze wazi wahalifu wa Demokrasia kama hawa wafanywe nini.Huyu Meya ni kama Mungu Mtu.
 
Last edited by a moderator:
mimi niko hapa mwanza naona huyu meya kwa jinsi anavyochukiwa na wananchi anazidi kuichimbia kaburi ccm,lakini cha ajabu eti ccm wao wanaona kuwa huyu meya ndiye wa kuisambaratisha cdm.Sijui nani anayepanga hii mipango ya ccm
 
Huyo meya wa kichina nyie hamumjui vizuri! Kwanza ni jambanoka na hata washirika wake wa kibiashara ( kirumila&zacharia) wameisha mtenga kibiashara kwasababu ya vitendo vyake ktk jamii kuwa havifai.na hapo alipo amefirisika kimali na kiakili.
 
CHADEMA inapitia wakati mgumu sana. Ina wasaliti kuanzia ngazi ya taifa mpaka kijiji. Kweli CCM wameamua. Ninaamini Mbowe na Slaa wanafanya kazi katika mazingira magumu sana wakati huu. Wanahitaji maombi ya Watanzania !
 
CHADEMA inapitia wakati mgumu sana. Ina wasaliti kuanzia ngazi ya taifa mpaka kijiji. Kweli CCM wameamua. Ninaamini Mbowe na Slaa wanafanya kazi katika mazingira magumu sana wakati huu. Wanahitaji maombi ya Watanzania !

Nakuunga mkono mkuu Richard Mlangi,Dr Slaa na Mbowe wapo hapo walipo kwa nguvu za Mungu.
 
Last edited by a moderator:
Huyo meya wa kichina nyie hamumjui vizuri! Kwanza ni jambanoka na hata washirika wake wa kibiashara ( kirumila&zacharia) wameisha mtenga kibiashara kwasababu ya vitendo vyake ktk jamii kuwa havifai.na hapo alipo amefirisika kimali na kiakili.

Lakini yote yana mwisho mkuu Nyamwaga.Nani alikuwa na nguvu kama Farao enzi hizo?
 
Last edited by a moderator:
Tulishasema , Huyu Matata iko siku atahama Mwanza hata kama amezaliwa hapo , Kwanza ukimchunguza kwa Makini haonekani kama ana akili timamu , anatumika kirahisi sana kuliko hata anavyoweza kutumika chizi .
 
mimi niko hapa mwanza naona huyu meya kwa jinsi anavyochukiwa na wananchi anazidi kuichimbia kaburi ccm,lakini cha ajabu eti ccm wao wanaona kuwa huyu meya ndiye wa kuisambaratisha cdm.Sijui nani anayepanga hii mipango ya ccm

Mkuu wangu democratic anadhani utawala wake hauna mwisho!
 
Last edited by a moderator:
Huyo meya wa kichina nyie hamumjui vizuri! Kwanza ni jambanoka na hata washirika wake wa kibiashara ( kirumila&zacharia) wameisha mtenga kibiashara kwasababu ya vitendo vyake ktk jamii kuwa havifai.na hapo alipo amefirisika kimali na kiakili.
Zacharia huyu huyu tunayemjua ?
 
Back
Top Bottom