UTEUZI: Rais Magufuli amteua Dk. Mduma kuwa Mwenyekiti wa CMSA

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,266
Rais John Magufuli leo Ijumaa amemteua Dk John Kedi Mduma kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA)

Taarifa iliyotelewa leo na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi imeeleza kuwa uteuzi wa Mduma umeanza Februari 23, mwaka huu

Dk Mduma anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Grace Rubambey ambaye amemaliza muda wake
d75854bca1a687346933f91a4dcbd5c1.jpg
 
Lipumba anakeshaga katika ofisi za wakuu wa nchi.....ni kama kuna kitu aliahidiwa,sasa anaona kinachelewa au anaona dalili za kutotimiziwa.

Naona wanampigisha mapicha tu ili baadae yatumike kama ushahidi
 
Ngoja na mie nisomeee hadi nipate PHd, wanapeta sana awamu hii: Mie niliyeishia darasa la saba ngoja nikomae tu kwenye key board kuchat JF
 
Hata angekuwa na Phd nne hatafanikiwa kukuza mitaji, mazingira ya kisiasa kwa sasa sio rafiki wa wawekezaji.
 
Vipi sheria inasemaje juu ya uteuzi wa huyo mtu? Anasifa kama sheria inavyosema, Maana huyu Magu teuzi zake zinamashaka kisheria kidogo.
 
uwezo ktk Tanzania ya viwanda umezingatiwa hata angalau kuzungusha cherehani tupate nguo licha ya kisomo stadi za kazi ktk Tz ya viwanda ???
 
Back
Top Bottom