UTEUZI: Latifa Mohamed Khamisi ateuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu TANTRADE

Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Latifa Mohamed Khamisi kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Biashara Tanzania (TANTRADE)

Anachukua nafasi ya Edwin Rutegaruka aliyeteuliwa kuwa Balozi. Kabla ya uteuzi huo alikuwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TANTRADE

View attachment 1909697
Kila la kheri Bi. Latifa kwa majukumu mapya
 
Nakiri kusema tuna safari ndefu sana. Mungu tusaidie. Mungu tusaidie. Mungu tusaidie. Wewe pekee waijuwa kesho yetu sisi watanzania. Tuna watu wana akili sana hili taifa ila wote wamefunga vinywa vyao. Je kesho yetu itakuwaje. Wewe wajuwa Baba. Zaidi twawaombea hekima na akili walio ktk madaraka. Amen.
Bado sijakuelewa mzee funguka
 
Si alikuwa naibu wake? Angetoka nje pia si ingekuwa haijakaa poa kama naibu ana uezo jamani? Si promotion within? Kwa nini ionekane kitu tata?
Usijiulize yote ni chuki tuu isiyo na sababu za msingi.
 
Mkuu 'macho', ingependeza zaidi kama wasifu wake ungeambatana na picha yake.

Hii picha pekee haisaidii chochote kumfahamu mteuliwa huyu kama anazo sifa za kushika nafasi hiyo au hana.

Moja ya mambo ambayo taifa letu limeyakumbatia na wala hayatusaidii chochote ni hizi teuzi za kishikaji tu bila ya kuwa na sifa stahili zinazotakiwa katika utendaji wa mtu anayeteuliwa.

Jambo hili CCM imelishikilia sana, na linaturudisha nyuma sana kama taifa.
 
Uongozi wa Jamii forums uwe makini na uzi zenye masuala ya udini Kama huu.Tusipoziba ufa tutajenga ukuta.

Kila Mtanzania ana haki ya kuteuliwa ili mradi awe na sifa,masuala ya dini tuyaepuke ndugu zangu tutende mema hapa Duniani tunaishi kwa muda mfupi sana,tujitahidi tuwe na matendo mema.

Ni Mimi ndugu yenu katika bwana wetu Yesu Kristo.
 
Wenzetu wanaongelea UBUNIFU wazidi kuishi vyema sisi tunaangaliana WAJIHI ,DINI NA MAKABILA duuuh 🤣🤣
Haya unapashwa kuwaeleza hao wanaoteuwa, yanawahusu sana.

Hao ndio wanaoturudisha nyuma sana sana kama taifa kwa matendo yao ya kutoona umuhimu wa mtu kuwa na viwango stahiki wakati anapoteuliwa kwenye nafasi yoyote ile, bila kujali hayo mengine unayoyaandika hapa.

Mimi nadhani pamoja na uhitaji mkubwa wa uwepo wa katiba mpya, pana haja pia ya kutazamwa taratibu za teuzi na ajira mbalimbali katika nafasi serikalini.

Wat waajiriwe/wateuliwe kwa sifa zinazoendana na kazi wanazotakiwa kuzifanya.
 
Uongozi wa Jamii forums uwe makini na uzi zenye masuala ya udini Kama huu.Tusipojenga ufa tutajenga ukuta.

Kila Mtanzania ana haki ya kuteuliwa ili mradi awe na sifa,masuala ya dini tuyaepuke ndugu zangu tutende mema hapa Duniani tunaishi kwa muda mfupi sana,tujitahidi tuwe na matendo mema.

Ni Mimi ndugu yenu katika bwana wetu Yesu Kristi.
Exctly, na Wakristo wanamchukia Rais sababu ya dini yake tu, wanataka teuzi zote wateuliwe wao tu, hata Gwajima taperi, hizo kelele zake zotee,sababu Rais Ni muislamu, walitaka awe kafiri mwenzao hapo sawa,
Samia tunae Hadi mwaka 2035, asiyetaka ahame nchi, na akitoka muislamu,anaingia Tena muislamu
 
Back
Top Bottom