Uteuzi: Katibu mkuu bakwata ateua kamati kuandaa maadhimisho miaka kumi ya Mufti Shehe mkuu Abubakar Bin Zubeir

Uteuzi: Katibu mkuu bakwata ateua kamati kuandaa maadhimisho miaka kumi ya Mufti Shehe mkuu Abubakar Bin Zubeir

Uzalendo wa Kitanzania

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2020
Posts
4,188
Reaction score
9,165
KATIBU MKUU BAKWATA ATEUA KAMATI KUANDAA MAADHIMISHO YA MIAKA KUMI YA YA UONGOZI MAKINI NA IMARA WA MHES
MUFTI...........

Mh. Katibu Mkuu wa Baraza Kuu la Waislamu wa Tanzania (BAKWATA) Alhaj Nuhu Jabir Mruma Ashighatiiniy Almwangawiy ameteua kamati maalum kuandaa maadhimisho ya miaka kumi ya uongozi makini na imara wa Mh. Mufti na sheikh Mkuu wa Tanzania Mujaddidul Asr, Al-allaama, Alhaj, Dr. Sheikh Abubakar Zubeir Ali Mbwana Al-mukarram yatakayofanyika mchana wa Tarehe 9.9.2025 na kilele chake ni usiku wa kuamkia tarehe 10.9.2025.

Kwa mujibu wa taarifa maalum ya katibu Mkuu iliyotolewa leo jiji Dodoma Alhaj Mruma amemteua Alhaj Muharrami Pembe kuwa Mwenyekiti wa kamati hiyo ni Dr. Harith Nkussa kuwa mratibu wa Maadhimisho hayo ambayo yanatarajiwa kuwa ya kipekee.

Kwenye taarifa hiyo alhaj Mruma amewataja wanakamati wengene ambao ni :-

✔️ Mh. Rashid Jongo - Makamu Mwenyekiti
✔️ Mh Hajjat Neema Maumba - Katibu.
✔️ Mh. Juneid Murtazali Hassan - Naibu katibu

Aidha taarifa hiyo ya alhaj Mruma imesema wajumbe wa kamati hiyo ni :-

1. Hajjat Mariam Dedes
2. Hajjat Zubeda Sway
3. Hajjat Batuli Suleimani
4. Hajjat Fatma Dachi
5. Mh. Masoudi Nduvini.

Alhaj Mruma amewataka wanakamati hao kuandaa vyema tukio hilo muhimu la kipekee na kufanya kazi usiku na mchana wakiwa wamoja huku waki.tanguliza Mwenyeezi Mungu mtukufu.

"Kipindi hiki kifupi tuna Maulid na hivi karibuni tulitoka kwe mahafali ya Daarul Maarif na hapa katikati kabla ya Maulid tutakuwa na jambo kubwa ambalo pia linalomuhusu Mufti wetu. Yote hayo ni yetu na yanasimamiwa na kamati zinazojitegemea. Jambo la muhimu ni kutambua majukumu na mipaka yenu na Allah atasaidia"

Amsema na kuongeza "Muhimu zaidi ni kwa viongozi wa BAKWATA ngazi zote kuanzia makao makuu, Mikoani mpaka misikiti na waislamu kwa ujumla kuhudhuria tukio hilo muhimu la kujivunia"

Alhaj Mruma amesema huko nyuma kulikuwa na fukra potofu kwa waislamu kwamba BAKWATA haifanyi makubwa na kuna baadhi ya watu hawajaondokana na mawazo hayo yaliyopitwa na wakati.

"Maadhimisho haya ni jukwaa kubwa kuonyesha ukubwa na umubimu pamoja na wingi wa mamabo mema yanayofanywa na BAKWATA pamoja na miradi mikubwa inayoendelea kutekelezwa na BAKWATA kote nchini chini ya jemedari wetu Mh. Mufti Dr. Abubakar Zubeir ambaye malipo pekee tutakayompa siku hiyo kwa mambo makubwa aliyofanya ni pongezi na dua" Amesema.

Mheshimiwa Mufti na sheikh Mkuu wa Tanzania aliteuliwa kuwa kaimu Mufti mara baada ya kifo cha Mufti sheikh Issa Simba kwenye kikao cha Baraza la Ulamaa kilichofanyika Bagamoyo saa tatu asubuhi ya tarehe 22.6.2015 na kuchaguliwa kuwa Mufti na sheikh Mkuu wa Tanzania kwenye mkutano mkuu wa uchaguzi uliofanyika Dodoma siku ya Alhamisi tarehe 10.9.2015
............

Dr. Harith Nkusss
Msemaji Maalum wa Mufti
Jumatano 27.8.2025
Mtumba. Dodoma
 
Huu utaratibu umeanza lini? Wale wengine wanazo taratibu za jubilei za miaka 10, 20, 25, nk. Hili ni jambo jipya.
 
Back
Top Bottom