Utetezi wa hoja za CAG ni batili

NTIGAHELA

JF-Expert Member
Jan 1, 2014
362
254
Serikali yatoa utetezi wake Bungeni zilipo Tshs1.5 trn!

Nimemsikia Naibu Waziri akitoa taarifa. Kwanza nilitegemea ufafanuzi utatolewa na aliyekagua au kamati husika, yaani CAG au PAC.

Pili naelewa hadi Report inaandaliwa na CAG, tayari wahusika wa masurufu wa Wizara wamekwisha hojiwa mbele ya Kamati ya Bunge PAC na LARC. Hivyo sikuona sababu ya Serikali kutoa ufafanuzi wa peke yake ambayo labda inaweza kukinzana na CAG Report na PAC pale watakapoamua kutolea ufafanuzi wao.

Tatu ieleweke hoja iliyopo ni ya Tshs1.51trn kutoonekana kwenye mahesabu ya matumizi. CAG ameweka wazi, inawezekana imetumika kwenye matumizi mengine yaliyo nje ya Bajeti, ndipo akawataka Wabunge waihoji Serikali hiyo pesa ipo wapi??! Na kwanini haionekani kwenye mahesabu ya matumizi ya Serikali??!!
Matumizi yote ya Serikali ni LAZIMA yapitishwe na Bunge! Hiyo ni Sheria.
Inashangaza kuona Wizara ikipokea pesa ndogo chini ya 40% ya bajeti iliyopitishwa, lakini kuna matumizi yasiyo rasmi yakipewa umuhimu wa malipo!

Nne, Naibu Waziri atambue CAG Professor Assad ni Mtaalam aliyebobea kihasibu na amefundisha IPSAS Accrual System. Sasa ninashangaa maelezo ya Naibu Waziri kuaminisha kwamba Professor hakuliona hili?!!! Naona yeye Naibu Waziri ameongea kisichokuwapo.

Tano, Mheshimiwa Naibu Waziri, CAG Report sio siasa bali ni ukaguzi wa kilichoonekana. Ukijibu kisiasa, ni kukiuka utaalam wa kihasibu ambao unasomewa na kutambulika. Hoja za CAG zinajibiwa kwenye vikao vya kamati ya Bunge na wataalam kitaalam, huo ufafanuzi wako leo ni kisiasa zaidi.

Mwisho sikupenda kauli ya Naibu Waziri kudai kwamba wanaozusha kupotea Tshs1.5trn ni wale wasioitakia mema nchi yetu na Serikali yake!
Hii inamaanisha kuhoji zilipo Tshs 1.5trn ni kuitakia mabaya nchi!
Mheshimiwa Naibu Waziri, hakuna aliyezusha, bali wametoa maoni kulingana na CAG Report na hiyo ni haki yao kuhoji.
Jambo la muhimu maelezo ya ufafanuzi toka kwa CAG au PAC ndio yatakayotoa picha zaidi kuliko maelezo ya Serikali peke yake.
Maelezo ya Serikali yanakuwa na lugha ya Kitalaam na sio vijembe vya kisiasa, vinginevyo hivyo vijembe vikijibiwa na vijembe patakuwa hapatoshi na tutagawanyika zaidi!
Kauli hizi za mipasho ziachiwe vyama vya siasa na washabiki.

Hii ni nchi yetu sote na wananchi wote wanaitakia mema nchi yao. Kuhoji ni wajibu wa Raia yeyote Mzalendo. Usiangalie sura, chama wala jina la anayetoa hoja, muhimu thamini hoja yake kwa maslahi ya Taifa.

Mungu Ibariki Tanzania.
 
watawala bwana, wanataka kujipa vyeo vya uzalendo wakati ni wapigaji na ukihoji eti unavuruga amani hahahaha
 
ili jambo lipite salama iundwe tume huru ichunguze jambo hili. hata EPA serikali mwanzoni ilikanusha hivohivo baadaye ikaja kugundulika siyo.....
 
Wamekuwa wakali hao hatari, mpaka sasa ndiyo tumeanza kupata wasisi zaidi kuwa si zimetumika nje ya bajeti Bali wamezipiga kabisa wamegawana kama za escrow kwenye masandarusi.
 
Umeandika very polite and very professional hadi raha kusoma. Mtaalam anakumbushwa na mwanasiasa mambo ya Accrual System!! Yaani ukamweleze Dr kuwa Dr pamoja na kwamba Vipimo vinasema nina malaria lakini Naamini Nina UTI Sio malaria....
 
Na muda si mrefu, kujadili hili jambo itageuka kuwa uchochezi. Zitto anaweza kuingia matatani na kutiwa kashkash ili kunyamazisha wengine kuendelea kuhoji.

Na endapo bunge litanyamazia matumizi yasiyoizinishwa bila kuchukua hatua...watakua wamemuonea tu Pascal Mayalla kumuita na kumhoji kwa ile kauli yake.

Hapo ndio watakua wameondoa alama ya kiulizo kisha tutabakiwa na BUNGE LINAJIPENDEKEZA.
 
Nchi hii ukiwa mjinga na mpumbavu ukiwa si mtu wa kuhoji basi wew ni mzalando ila ukiwa mtu wa kuoji na kupambanua hoja wee si mzalendo uwo upumbavu wa viongozi wa afrika mtaji wao mkubwq ni watu mazwazwa wasio na elimu lakini ukiwa muelewa na mpinzani wew ni adui mkubwa wa chama tawala nchi hii inaitaji maombi nakubwa
 
Wasioitakia mema nchi yetu inakua kama kibwagizo sasa hivi mtu akianza kuhoji vitu kuhusiana na nchi yetu.
Mkuu unadhani hiki kibwagizo ni kipya? Ni zilipendwa hizo... Wakati wa mfumo wa chama kimoja ilikuwa akitokea mwanachama wa CCM anakuwa na mawazo tofauti au kuhoji, kibwagizo kilikuwa ni hiki, "wewe unatumiwa na maadui wasiyoitakia mema nchi yetu".
 
Back
Top Bottom