Utenzi wa Chujio

Raia Fulani

JF-Expert Member
Mar 12, 2009
10,848
2,669
Wadau nimeonelea
Jukwaa kulitembelea
Chujio kulisemelea
Wasione laelea

Chujio litazame
Lilivyo kifalme
Ndo nikaona niseme
Hadi niwe mkame

Chujio lile la tui
Kama ulikuwa hujui
Chujio sio adui
Ni rafiki wa uhai

Halina gharama asilani
Bali lina thamani
Kama chumvi mezani
Kwa chakula kinywani

Alitumia mwanamke
Japo si lake
Alifanyia makeke
Chakula kiwe mwake

Chujio lavutia
Kwa kuliangalia
Umbole maridhia
Ndo wanavolisifia

Wanawake mlithamini
Popote litunzeni
Kabatini na sirini

Liwape tui makini



:violin:
 
katika ukweli wa nafsi yangu huwa nakaa na kufikiri ni vipi kwa kaz kama hii mtu anashindwa kutoa maoni kwa namna yoyote tu. hata wadau hamuulizi kilichofichwa kwenye hiyo mistari?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom