Utenzi wa Chujio

Raia Fulani

JF-Expert Member
Mar 12, 2009
10,880
2,758
Wadau nimeonelea
Jukwaa kulitembelea
Chujio kulisemelea
Wasione laelea

Chujio litazame
Lilivyo kifalme
Ndo nikaona niseme
Hadi niwe mkame

Chujio lile la tui
Kama ulikuwa hujui
Chujio sio adui
Ni rafiki wa uhai

Halina gharama asilani
Bali lina thamani
Kama chumvi mezani
Kwa chakula kinywani

Alitumia mwanamke
Japo si lake
Alifanyia makeke
Chakula kiwe mwake

Chujio lavutia
Kwa kuliangalia
Umbole maridhia
Ndo wanavolisifia

Wanawake mlithamini
Popote litunzeni
Kabatini na sirini

Liwape tui makini



:violin:
 
mafumbo yako ni mengi, twaomba tufumbulie
sikiliza ndugu kingi, tafasiri tupatie
tumekikwaa kigingi, naomba tusaidie
chujio unalosema, maana yake ni nini.
 
Nyie watu wazima bwana. Mlipaswa kusoma katikati ya mistari kupata maana. Kama vipi nitawatafsiria baadae sana
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom