Utendaji VS Elimu

mwanawao

JF-Expert Member
Aug 18, 2010
3,164
5,689
Katika dunia ya leo elimu ni muhimu sana katika utendaji wa kazi mbalimbali. Lakini siyo kila mwenye elimu anao uwezo wa kutenda kama wengi wanavyowez kutarajia.

Ni mara nyingi sana unaweza kukutana na mtu ana degree lakini utendaji wake wa kazi unapitwa hata na mtu mwenye certificate. Vivyo unaweza kuta mtu ana Phd lakini utendaji wake wa kazi anazidiwa na mwenye degree moja au hata diploma.

Elimu ambayo haiwezi kukusaidia kukabiliana na mazingira unayoishi ni sawa na bure.

Ndo maana mashirika mengi ya kimataifa wanaangalia sana performance yako katika kazi na siyo Elimu. Unaweza kuwa na Masters utendaji wako.ni mdogo ukazidiwa mshahara na mwenye degree moja coz wenzetu wanaangalia zaidi performance yako ipoje.

Kwa hiyo ndugu zangu tuache sana kuvalue elimu ya kuonyesha makaratasi na vyeti,tupime elimu zetu katika vitendo.

Unakuta mtu amekazana kusoma masters, phd ukimuuliza why unasoma masters, phd.sana sana atakujibu niongezwe mshahara au nipate cheo.

Nategemea sana mtu akisoma masters au phd awe kweli ameona tatizo au upungufu katika sehemu anayofanyia kazi na anataka kutatua hilo na siyo tu kusoma kwa sababu fulani kasoma au unataka kupata mshahara mkubwa.

Tuacheni kukimbazana na elimu za makaratasi ambazo hazina msaada kwa Taifa letu
 
Back
Top Bottom