Utendaji mbovu wa Shirika la TANESCO: Kwanini nisubiri zaidi ya miezi 6 kuunganishiwa umeme ulio mlangoni kwangu Gongo la Mboto?

Ahsante kwa ushuhuda wako

Tafadhali tusaidieni taarifa kamili tupo kuwahudumia
Tunashukuru vile umekuja na kujibu maswali kwa wakati.

Unatakiwa kufanya nini ili kubadilishiwa tarrif? Mimi nimeunganishiwa umeme mwezi Januari 2020 nikapigwa tariff 1 nafikiri (ile ya elfu 10 unit 28), matumizi yangu kwa mwezi ni wastani wa unit 60, ninaona ninastahili kuwa katika tarrif ya matumizi madogo (tarrif 4 nafikiri - sina uhakika, kama nakosea nirekebishwe) nipo Kiluvya.
 
Tafadhali onyesha namba ya mita tuhakiki
 
Pamoja na maelezo marefu.
Nikuambie tu hiyo laki 6 umepigwa gharama ya kuunganisha umeme ndani ya mita 100 haifiki laki 6. Pia tambua nguzo za Tanesco haziuzwi. Wana mtindo wanakuambia nguzo moja bure ya pili unalipia. URONGO.

AU NASEMA UONGO NDUGU YANGU TANESCO
 
Wanataka jina ili wakawaambie wenzao anaeleta chokochoko zote hizi ni pombe kali
 
Wanataka jina ili wakawaambie wenzao anaeleta chokochoko zote hizi ni pombe kali
Taarifa kamili ndio huduma mpendwa mteja wetu

Unapolalamika unalenga kuhudumiwa na unapohitaji huduma onyesha taarifa kamili maana wakati mwingine unakuta ni vishoka wanafatilia kazi za watu na hawana taarifa kamilo.hivyo kama ni mteja halali unaogopa nini kutuma taarifa hata inbox uhudumiwe
 
Vishoka tunaomaanisha ni wateja wanaojifanya wanafatilia kazi za wateja au kujifanya wafanyakazi ili wajipatia fedha isivyo kihalali

Nchi ina miaka 60 ya Uhuru lakini bado mnafanya kazi kizamaniiii. Yani hamuwahudumii watu mpaka walalamike, lipite zogo, vurugu za maongezi dah!, Mtu analipia huduma kumpa sasa haki yake ya kimsingi ya kile alicholipia mpaka lipite zogo.
Ni shirika lenye watu wavivu msio na mfano, miezi 6 toka mtu alipie mnazurura tu, Pesa yake mmekula kumpa huduma majanga.
Ningekuwa Jiwe au Waziri anaehusika na hii mamlaka yenu aisee ningeanza na wewe uliepo humu. Upo humu kila siku lakini malalamiko hayaishi, maana yake ni kwamba hata wewe ni mvivu. Uwepo wako humu ilitakiwa liwe ndio suluhisho la ucheleweshaji. Sasa kama upo humu kuwahudumia wale wanaolalamikia huduma yenu Vp wale ambao hawajajiunga humu huku wakicheleweshewa huduma, wao walalamike wapi ili kilio chao kisikike???
Tunasoma habari za shirika lenu mpaka tunasikia aibu. Mnatutia aibu kwa wageni. Kuna wageni wapo humu wanaojua Kiswahili, wanatusimanga wanaposoma malalamiko ya wateja wenu. Makazini humu na matusi kututukana huku wakitoa mifano ya shirika lenu kuwa lina mijitu mivivu.
Jirekebisheni bana.
 
Tunashukuru sana mteja aliyelalamika hakutoa taarifa kamili tuone hicho alicholalamikia hivyo nie vema kuacha atoe ushirikiano tuone taarifa kwenye mfumo na kumuhudumia
 
Tatizo Janja Janja nyingi TANESCO dawa yenu kuwaripoti kwa mkuu, maana bila kuchangamshwa hamfanyi kazi

Hivi siku mkipata mshindani si mtafilisika nyie? Acheni hizo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…