Utendaji kazi wa Jeshi letu la Polisi unatia mashaka

Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
15,484
30,162
Kwenye mfumo wa siasa wa vyama vingi, vyombo vyetu vya ulinzi na usalama havitakiwi kujihusisha na mambo ya siasa na vinatakiwa viwe neutral visivyofungamana na chama chochote cha siasa na vyombo hivyo vinatakiwa visionyeshe upendeleo kwa chama chochote na kuvionea vyama vingine.

Ingawa kinadharia vyombo hivyo vya ulinzi na isalsma huwa vinadai viko neutral na haviegemei upande wa chama chochote cha siasa, lakini sisi wananchi tunaofuatilia mwenendo wa vyombo vyetu hivyo vya ulinzi na usalama, hususani Jeshi letu la Polisi tumekuwa tukiliona Jeshi hilo likifanya upendeleo wa wazi kwa chama tawala cha CCM na kuwanyanyasa vyama vya upinzani hususani chama kikuu cha upinzani nchini cha Chadema.

Nitatoa mifano michache katika kuthibitisha kauli yangu.

Ingawa kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, Ibara ya 3(1) inaeleza kuwa nchi yetu itakuwa ya mfumo wa vyama vingi na katika utekelezaji wa shughuli zao vyama hivyo havipaswi kuingiliwa na chombo kingine chochote. Hata hivyo tumekuwa tukishuhudia Jeshi letu la Polisi likiingilia waziwazi shughuli za vyama vya siasa hususani katika uendeshaji wa mikutano ya kisiasa.

Tumekuwa tukishuhudia Jeshi letu la Polisi likivizuia Mara kwa Mara vyama vya siasa vya upinzani nchini. hususani chama kikuui cha upinzani cha Chadema kufanya mikutano yake huku Jeshi hilo hilo likiruhusu Chama cha CCM kufanya mikutano na shughuli zake bila kuzuiwa!

Nitatoa mfano mmojawapo kuonyesha namna gani Jeshi letu la Polisi linavyoonyesha upendeleo wa wazi kwa chama cha CCM.

Mbunge wa Chadema Esther Bulaya wa Jimbo la Bunda alienda kwenye Jimbo la mbunge mwenzake wa Chadema John Heche wa Jimbo la Tarime kwenda kushiriki harambee ya ujenzi wa shule ya Nyamongo na yeye mbunge Esther Bulaya akatoa mchango wake wa mifuko 100 ya cement.

Mbunge huyo baada ya kumalizika mkutano huo alikamatwa na Jeshi la Polisi na kwenda kulazwa kwenye selo za Polisi na wakati wowote kuanzia sass atafunguliwa mashitaka mahakamani ya uchochezi!

Hata hivyo mbunge Elibariki Kingu wa CCM wa jimbo la Singida Magharibi alifanya "the same thing" na kwenda Jimbo la Singida Mashariki la mbunge Tundu Lissu wa Chadema na akaendesha harambee ya ujenzi wa shule, hajakamatwa na Jeshi la Polisi!

Tumeshuhudia pia mbunge wa viti maalum wa CCM Tulia Ackson akienda Jimbo la Mbeya mjini la mbunge Sugu wa Chadema naye akishiriki harambee kuchangia ujenzi wa soko lliloungua la Sido, naye hajakamatwa na Polisi!

Tunachojiuliza sisi wananchi ni kwanini Jeshi letu la Polisi linakuwa na double standard na kutekeleza majukumu yao kwa ubaguzi kwa kukipendelea waziwazi chama tawala cha CCM na kuvinyanyasa na kuvionea vyama vya upinzani, hususani chama kikuu cha upinzani cha Chadema?

Iwapo Jeshi letu la Pokisi linataka kurejesha imani ya wananchi kuwa ni Jeshi linalowatumikia wananchi wote bila upendeleo ni lazima lijirekebisje na kuepuka kufanya ubaguzi katika utendaji wake wa kazi kwa kupokea maagizo toka kwa watawala wetu na kuyatekeleza.
 
Tumreshuhudia pia vitendo vya kutekwa kwa wananchi, kuteswa, na wakati mwingine kuvamiwa wananchi bila kuliona Jeshi hilo likiwakamata watuhumiwa na kuwafungulia mashitaka mahakamani.

Nitatoa mifano michache.

Tulishuhudia siku za nyuma kituo cha Clouds media kikivamiwa usiku wa manane na askari wenye silaha za moto na watangazaji wa kituo hicho wakitishwa, lakini hadi leo hatukulions Jeshi letu la Polisi likiwakamata watu hao na kufunguliwa mashitaka!

Tulishuhudia pia msanii Roma Mkatoliki akitekwa na kupelekwa sehemu isiyojulikana na kuteswa na watu wasioujulikana, lakini baadaye tulimsikia mkubwa mmoja wa jiji hilo la Dar ambalo msanii huyo alitekwa akiutangazia Umma wa watanzania kuwa msanii huyo atapatikana kabla ya Jumapili na kweli msanii huyo alipatikana kabla ya Jumapili kama tulivyoahidiwa na mkubwa huyo, lakini cha kushangaza hatukiliona Jeshi letu la Polisi limkamate mkubwa huyo ili alisaidie kwa uchunguzi!

Tulishuhudia pia aliyekuwa Waziri wa habari akitolewa bastola na kitishwa pale Protea Hotel na mtu ambaye picha zilimtambulisha kuwa ni nani, hata hivyo hadi leo hatujaliona Jeshi letu la Polisi likimkamata mtu huyo na kumfungulia mashitaka ya jinai ya kumtolea bastola Nape Nnauye na kumtishia kumuua!
 
Tumeshudia pia siku chache zilizopita watu wasiojulikana wakisadikika kuvalia sare za Polisi wakiwa na silaha za moto na wakavamia ofisi za mawakili wa IMMMA na kutega madumu ya petroli na kuzilipua ofisi hizo

Lakini tukizingatia experience ya matukio ya siku za nyuma ambayo yanafanana "design" yake na tukio hilo, yapo matumaini finyu kama kweli Jeshi letu la Polisi litakuwa na "ubavu" wa kuwakamata watuhumiwa hao na kuwafungulia mashitaka......
 
Wakuu hii utube ya jamaa aliyemchana dikteta uchwara kwanini humu haitakiwi kuwepo? Imekuwa ni gumzo kubwa nchini lakini hapa kwenye forum ya kiongozi wa habari nchini video hiyo haitakiwi.
 
Wakuu hii utube ya jamaa aliyemchana dikteta uchwara kwanini humu haitakiwi kuwepo? Imekuwa ni gumzo kubwa nchini lakini hapa kwenye forum ya kiongozi wa habari nchini video hiyo haitakiwi.
JF wanahofia wasije lipuliwa na madumu ya petroli......:D:D
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Polisi, Time ya Uchaguzi, hawa ni matawi ya CCM

Wamempiga Mbunge Haonga kosa Uchaguzi wa Mwenyekiti wa Halmashauri ili Diwani wa CCM ashinde.Na bado Mahakama ikipelekewa kesi ushindi watapewa hao hao CCM waliovuruga uchaguzi.

Sikumshangaa Kaimu Jaji akiitetea Polisi.Hata Mahakama kwa sasa ni Tawi Mdogo la CCM Mkoa wa Mahakama.
 
Tuna katiba mbovu sana
Ndiyo maana hao maccm waliikataa ile Katiba nzuri iliyoandaliwa na Tume ya Warioba ili tubaki na hii Katiba mbovu itakayowabakiza madarakani CCM hadi mwisho wa dunia!
 
Wakuu hii utube ya jamaa aliyemchana dikteta uchwara kwanini humu haitakiwi kuwepo? Imekuwa ni gumzo kubwa nchini lakini hapa kwenye forum ya kiongozi wa habari nchini video hiyo haitakiwi.
naomba title ya hiyo youtube,niisikilize
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Mwalimu Nyerere wakati wa uhai wake katika moja ya hotuba zake alifafanua ifuatavyo kuhusu kwanini Afrika Kusini waliitwa makaburu.

Aliongea maneno yafuatayo:-

Hatukuwaita wazungu wa Afrika Kusini makaburu kutokana na rangi yao nyeupe, bali tuliwaita makaburu kutokana na tabia yao ya kibaguzi, yeyote anayefanya mambo ya kibaguzi whether ni mweupe au mweusi wote ni makaburu tu" mwisho wa kunukuu.

Kama kweli tunataka kumuenzi Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere kwa vitendo na kutokana na vitendo vya kibaguzi vinavyofanywa na Jeshi letu la Polisi kwa kuipendelea waziwazi CCM na kuvibagua vyama vya upinzani, hususani Chadema, naamini tutakuwa sahihi kabisa kama tutawaita kuwa wao nao ni makaburu tuu.........
 
Back
Top Bottom