uteketezaji wa maliasili zetu....

Resi

Member
Aug 29, 2007
73
17
mimi nina uchungu:-

1) chui, simba, duma (cheetah), na paka wa aina nyingine. kila wataalamu wa wanyama wanasema hawa wanyama ni "endangered species" katika dunia nzima. yako maeneo mengine ambamo wamemalizwa kabisa. serikali yetu bado inatoa leseni kwa watu fulani kutoka nje ya nchi yetu, waje kuwinda hawa wanyama kwa malipo ya pesa.

2) miti (misitu) yetu pia, inayotuletea mvua na faida zingine nyingi, serikali yetu inatoa vibali kwa watu kuivuna, pia kwa pesa. serikali hiyohiyo inafanya blah blah za eti kampeni ya kupanda miti, japo ni wazi haiko makini katika suala hili.

wana-jamii: tupaaze sauti juu ya hii ishu, ni MUHIMU sana. serikali yetu haina haki wala sababu ya kutapanya maliasili hizi muhimu sana kwa maisha yetu ya sasa na ya vizazi vya baadaye.
 
Back
Top Bottom