Utekelezaji wa miradi moi wafikia wastani asilimia 78.5

Utekelezaji wa miradi moi wafikia wastani asilimia 78.5

Joined
Apr 15, 2025
Posts
91
Reaction score
174
b7b6d837-d35d-43c6-8783-810a932516f8.jpeg

Kasi ya utekelezaji wa miradi minne ya maendeleo katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) imefikia wastani wa asilimia 78.5, hali inayowasha taa mpya ya matumaini ya uboreshaji zaidi wa huduma kwa wagonjwa.

Meneja Milki, Mazingira na Matengenezo wa MOI Bw. Victor Kamagenge ameeleza leo Januri 28, 2026 kuwa kwa sasa taasisi hiyo inatekeleza miradi minne ya kimkakati ambayo ipo katika hatua mbalimbali za utekelezaji.

“Mradi wa kwanza ni ukarabati wa lililokuwa jengo la hospitali ya Tumaini ambayo ukikamilika utatoa huduma jumuishi za matibabu ya kibingwa kwa wananchi, mradi huu kwa sasa upo asilimia 95… mradi mwingine ni utengenezaji wa wodi ya wagonjwa mahututi (ICU) ya watoto ambayo umefikia asilimia 98, kwa mara ya kwanza watoto watakuwa na ICU yao” amesema Mhandisi Kamagenge

Ameongeza kuwa “Pia tuna mradi wa wodi binafsi za kisasa yenye vyumba 25 ambao utekelezaji wake umefikia asilimia 90, kukamilika kwa mradi huu kutavutia zaidi utalii tiba na mradi wa Nne ni ujenzi wa jengo la wagonjwa wa nje (OPD), hadi sasa tumefikia asilimia 35, mradi huu ukikamilika utaondoa kero ya msongamano wa wagonjwa katika kliniki ya sasa na hivyo kuboresha huduma kwa wagonjwa”

Amesema kwa ujumla wake utekelezaji wa miradi yote umefikia wastani wa asilimia 78.5 na kwamba ikikamilika itaongeza kasi na ufanisi ya kuhudumia wagonjwa mbalimbali wa mifupa, ubongo, mgongo na mishipa ya fahamu na kuleta matokeo chanya ya huduma hizo
 
Pongezi kwa raisi yetu kipenzi, kazi yake inaonekana!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom