kunena
JF-Expert Member
- Nov 29, 2016
- 506
- 717
Leo Mkuu wa mkoa wa Arusha Mh. Mrisho Gambo yupo ziarani wilayani Monduli lengo ikiwa ni kuzindua miradi na kukagua miradi mbalimbali wilayani humo.
Mh Gambo aliwasili makao makuu ya wilaya hiyo majira ya saa nne asubuhi na kupokelewa na mkuu wa wilaya ya Monduli Mh. Kimanta ambapo Mh Gambo alisomewa taarifa ya maendeleo ya wilaya hiyo.
Katika hotuba yake Mh Gambo ametoa mwito kwa jamii wilayani humo kutilia mkazo vita juu ya madawa ya kulevya ambapo amemtaka mkuu wa wilaya hiyo kuandaa mpango wa kutoa elimu juu ya madawa ya kulevya hasa mashuleni na ikiwezekana kuwe na picha za mfano wa waathirika wa madawa ya kulevya ili kujenga hofu kwa watoto juu ya mwisho na mwonekano wa waathirika wa madawa.
Pia amemtaka kamanda wa Polisi wa wilaya kuwashughulikia kikamilifu wauzaji na wasambazaji wa madawa wilayani humo kwa kuzingatia sheria na kanuni.
Mh Gambo amemtaka mkurugenzi wa Halmashauri ya Monduli kuweka mkazo katika ukusanyaji wa mapato kwani mpaka mwezi huu wa pili wamekusanya shilingi bilioni 1.1 sawa na asilimia 46% bado wapo nyuma ya lengo la ukusanyaji wa shilingi bilioni 2.4 kwa mwaka wa fedha 2016/2017. Katika hilo amekumbusha kuwa maelekezo ya serikali ni kuwa halmashauri yoyote itakayokusanya chini ya asilimia 80 itafutwa hivyo ametoa wito kwa halmashauri kuliangalia hilo kwa umakini.
Mh Gambo amewaomba watumishi wa Halmashauri kujiunga na mfuko wa bima wa CHF japo wana kadi za NHIF lengo ikiwa ni kutoa hamasa kwa wananchi kujiunga na bima hiyo na ametoa mfano kuwa yeye mwenyewe ana kadi ya NHIF na bado amekata kadi ya CHF,na ametoa mwito wa uharaka wa utoaji wa kadi hizo ili kuondoa manung'uniko kwa waliolipia.
Leo ni siku ya kwanza ya ziara ya Mh Mrisho Gambo katika wilaya ya Monduli,ziara hii ni ya siku tano.
Mkuu wa mkoa wa Arusha Mh Mrisho Gambo
Mh Gambo akipokea kadi ya bima ya Afya ya CHF ikiwa ni uhamasishaji wananchi kujiunga na mpango huo