Utekaji,utekaji,utekaji mnapata faida gani?

Utekaji,utekaji,utekaji mnapata faida gani?

Zee la madawa

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2022
Posts
1,728
Reaction score
4,075
Shirika la Amnesty International kwa kushirikiana na Chama cha Mawakili nchini Kenya (LSK) pamoja na Jeshi la Polisi nchini Kenya, wamefanikiwa kumuokoa mwanaharakati kutoka Tanzania, ndugu Mshabaha Hamza, kutoka mikononi mwa watekaji wanaodaiwa kutoka nchini Tanzania.

Taarifa ya Amnesty International inaeleza kuwa Watekaji hao walimteka Mshabaha na kumlisha madawa ya kulevya kwa lengo la kumrudisha kwa nguvu nchini Tanzania, lakini polisi mjini Nairobi na makachero kutoka ofisi ya DCI walifanikiwa kuzuia gari yao na kuwakamata watekaji hao.

Watekaji hao wametambuliwa kwa majina ya Aziz Hamad, raia wa Tanzania; Edward Mwangi Mwai, raia wa Kenya anayeishi Afrika Kusini; na Nelson Wanjohi Kirika, raia wa Kenya na dereva wa gari lililohusika katika jaribio hilo la utekaji.

Mshabaha ni mtetezi wa haki za binadamu kutoka Tanzania ambaye anaishi uhamishoni nchini Kenya kutokana na tishio la maisha yake. Amekuwa akijihusisha na utetezi wa haki za binadamu, demokrasia na uwajibikaji nchini Tanzania. Ni mwanachama wa Pan-African Solidarity Network, mtandao unaopinga utawala wa kiimla barani Afrika.

Katika taarifa iliyotolewa na Rais wa Chama cha Wanasheria nchini Kenya, Wakili Faith Odhiambo, ametaka Jeshi la Polisi kufanya uchunguzi wa wazi wa kesi hiyo na kukamata magenge yote ya "utekaji" yaliyopo nchini Kenya na nchi zingine yanayolenga kuteka na kuwadhuru watetezi wa haki za binadamu walioomba hifadhi katika nchi hizo.

Chama hicho pia kinataka kuwepo uwazi katika upeleezi wa shauri hilo, ili jamii ya Wakenya na Jumuiya ya kimataifa ijue watu hao wametumwa na nani, kwa malengo gani na ni nani anayefadhili shughuli hizo za kiharamia.!
 
Duuuh wasije wakawa walimbaka tu huko maana ndio michezo yao wakaikuteka cha kwanza ndio hicho, muulize Nondo
 
Back
Top Bottom